BILIONI (3) na MILIONI (750) !!
July 8, 2021,, Mtendaji mkuu wa Azam media Tido Mhando na mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dkt. Mshindo Msolla walisaini mkataba wa mashirikiano ya MAUDHUI baina ya Yanga SC na Azam TV (MEDIA PARTNERSHIP).
Thamani ya mkataba huo ni Tsh 41.64 BILIONI kwa miaka kumi (10).
Yanga watapokea Tsh 34.8 BILIONI kutoka AZAM TV baada ya makato mbalimbali. Yanga na Azam Tv watashirikiana kuandaa na kurusha MAUDHUI ya klabu ya Yanga kama ;
[emoji3502] Mazoezi ya timu.
[emoji3502] Maandalizi ya mechi
[emoji3502] Mechi za kirafiki na Exclusive mbalimbali za klabu ya Yanga kama usajili, Interviews na vitu vingine.
.
.
Klabu ya Yanga itakuwa ikipokea Tsh 200 Milioni kila mwezi kuanzia msimu huu (2021-22) hadi (2030). Pesa hiyo itakuwa ikiongezeka kila msimu.
.
.
[emoji419] Kupitia mkataba huu klabu ya Yanga itapokea BONUS ya Tsh (3) BILIONI KILA INAPOSHIKA NAFASI YA (1) AU YA (2) kwenye ligi kuu Tanzania bara.
.
.
Yanga wataendelea kupata Bonus kila wanapofanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali.
______________________________________
.
.
Ukiacha Mkataba huo wa MAUDHUI, Yanga wakiwa MABINGWA watapata Tsh 500 Milioni kutoka kwenye mkataba wa 'TV RIGHTS' ambao Azam TV waliingia na (TFF)
Pia kwenye mkataba wa Sports pesa na Yanga SC kuna kipengele kinachoeleza kuwa, kampuni hiyo itatoa Bonus ya Tsh 100 Milioni ikiwa Yanga watatwaa ubingwa.
Vilevile katika mkataba wa (GSM) na Yanga wa utengebezaji na usambazaji wa jezi kuna kipengele cha Bonus ya Tsh 100 Milioni iwapo Yanga wakitwaa UBINGWA wa ligi kuu.
Haikuishia hapo, katika mkataba wa Yanga na Taifa Gas kuna kipengele kinachoeleza kuwa, Taifa Gas watatoa Tsh 50 Milioni iwapo Yanga watatwaa UBINGWA wa ligi kuu.
Ukijumlisha pesa hizo unapata jumla ya Tsh 3 BILIONI na Milioni 750 ambazo Yanga watapata wakiwa MABINGWA wa ligi kuu.
____________________________________
Hivyo ndivyo mikataba iliivyo, sio kwamba naandika tu from no where. Mimi huwa siandiki kitu hapa bila kufanya utafiti.
Niliandika post jana ikieleza Yanga watapata Tsh 3 BILIONI na Milioni 750 iwapo wakiwa MABINGWA, baadhi ya watu wakawa wanakejeli wakidai nawalisha matango pori.
.
.
Chukua hiyo kutoka kwangu [emoji116]
Mjinga ni yule asiyejua kitu fulani lakini akielezwa ANAELEWA. MPUMBAVU ni yule anayejifanya anajua wakati hajui na hajui kuwa hajui.
[emoji368] Tom cruz