Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Nyerere aliwahi kusema kuwa Ikulu siyo pango la walanguzi. Kwa katiba hii tuliyonayo ambayo Rais ndiye Alfa na Omega na kwa Rasilimali tulizobarikiwa Tanganyika ukiwa Rais hata Elon Mask na Jeff Bonzos watakufahamu.
Kuna mengi tulipitia ambayo yaliharibu mchakato wa kuandaa watu kwa nafasi za juu. Baada ya vita ya Kagera 1978-79 miaka ya 80 Taifa lilishuhudia vifo vingi vilivyosababishwa na ugonjwa wa Ukimwi, enzi zile ukiitwa slim au Juliana. Akili nyingi ziliishia ardhini prematurely.
Baada ya hapo tuliendelea na tulijichimbia kaburi letu kama taifa taratibu. Mwalimu aling’atuka na mzee Ruksa bado akiwa na nidhamu ya kikoloni na kuamini uongozi ni dhamana lakini alifanikiwa kuuza Loliondo.
Kaka Stan Katabalo alifanya uchunguzi wa issue ya Loliondo na kutuletea habari nzima. Mauti yalimfika baada ya pale.
Tuliendelea kujichimbia kaburi na awamu ya tatu ikawa na sera ya ubinafsishaji. Huu mfumo unahitaji kulindwa na sera na kanuni imara za kuhakikisha wafanya biashara wanafanya yaliyokusudiwa nacwanalipa kodi.
Kila Raisi alikuja na lake hata la kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, na mwisho Yule aliyeenda zake aliamua kuiba mchakato mzima wa uchaguzi. Baada ya kwenda zake, aliyeapishwa aliambiwa wenzako waliopita walipita kibabe na wewe utapita tu.
Tumefika hapa, damu zinamwagika, wengine watatekwa na kuteswa, tutafungiwa kusafiri kwanda nchi za nje . Ninasikia hakuyapanga haya wakati anaapishwa.