tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Pamoja na kuwa muungwana na kuamua kujiuzulu nafasi yake ya uspika wa bunge la JMT, kuna uwezekano mkubwa Job Ndugai akajiuzulu nafasi yake ya ubunge wa jimbo la Kongwa kwa tiketi ya CCM kwani ubunge wake ndio ulipelekea kuchaguliwa na wabunge wenzake kuwa spika wa bunge. Hivyo basi, itakuwa jambo la busara, kheri na uungwana kwa Ndugai kuachia ubunge wake ili akae pembeni apate muda wa kujijenga kisiasa na kurudi mwaka 2025 akiwa kiumbe kipya.
Kwa hatua hii aliyofikia kisiasa, hakuna namna nyingine zaidi ya kujiuzulu ubunge kwa hiari na kwa roho safi kama ailivyofanya vema kujiuzulu nafasi ya uspika. Ni jambo la busara kwa mwamba huyu wa siasa za CCM afanye hima ajiuzulu ubunge ndani ya wiki hii ili kuokoa hadhi yake ya kisiasa. Akifanya hivyo atajijengea heshima kubwa si kwa Tanzania tu bali duniani kwa ujumla. Na akikaa pembeni umaarufu wake utapanda maradufu hivyo kushinda ubunge kirahisi katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Si ajabu ndani ya kipindi kifupi umaarufu wa Ndugai umeshuka kiasi kwamba hata mtoto mdogo anaweza kumpiga kofi hadharani na asimfanye chochote. Kwa ufupi ni kwamba amekuwa kama mtu aliyefunaniwa. Mfumaniwaji kwa kawaida huwa mpole kupitiliza na mara zote hufuata maagizo ya wafumanizi bila kujali udogo wao. Hata mtoto mdogo anaweza kumshika pumbu bila woga.
Kuna mifano ya viongozi wengi waliopoteza nafasi zao na kisha kuzirudisha na kufanikiwa zaidi kisiasa. Mfano halisi ni Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi ambaye wakati mmoja alijiuzulu nafasi ya uwaziri lakini hatimaye alijijenga upya kisiasa hadi kufikia kuwa Rais wa JMT kwa kipindi cha miaka 10. Job Ndugai hatakuwa wa kwanza kuachia kiti chake cha ubunge mara moja ajenge upya heshima yake ya kisiasa. Mtaalamu mmoja wa mambo ya siasa ametoa angalizo kuwa endapo Ndugai atakaidi kufanya hivyo kuna uwezekano jina lake likakatwa mwaka 2025 hivyo kuzikwa kabisa kisiasa. “Ni vizuri acheze karata zake vizuri sasa ikiwa bado anatamani kuwa kiongozi mkubwa zaidi katika nchi siku za usoni, hata ikibidi siku moja wananchi tumchague kuwa Rais wetu”. Alionya.
MAONI YANGUKwa hatua hii aliyofikia kisiasa, hakuna namna nyingine zaidi ya kujiuzulu ubunge kwa hiari na kwa roho safi kama ailivyofanya vema kujiuzulu nafasi ya uspika. Ni jambo la busara kwa mwamba huyu wa siasa za CCM afanye hima ajiuzulu ubunge ndani ya wiki hii ili kuokoa hadhi yake ya kisiasa. Akifanya hivyo atajijengea heshima kubwa si kwa Tanzania tu bali duniani kwa ujumla. Na akikaa pembeni umaarufu wake utapanda maradufu hivyo kushinda ubunge kirahisi katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Si ajabu ndani ya kipindi kifupi umaarufu wa Ndugai umeshuka kiasi kwamba hata mtoto mdogo anaweza kumpiga kofi hadharani na asimfanye chochote. Kwa ufupi ni kwamba amekuwa kama mtu aliyefunaniwa. Mfumaniwaji kwa kawaida huwa mpole kupitiliza na mara zote hufuata maagizo ya wafumanizi bila kujali udogo wao. Hata mtoto mdogo anaweza kumshika pumbu bila woga.
Kuna mifano ya viongozi wengi waliopoteza nafasi zao na kisha kuzirudisha na kufanikiwa zaidi kisiasa. Mfano halisi ni Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi ambaye wakati mmoja alijiuzulu nafasi ya uwaziri lakini hatimaye alijijenga upya kisiasa hadi kufikia kuwa Rais wa JMT kwa kipindi cha miaka 10. Job Ndugai hatakuwa wa kwanza kuachia kiti chake cha ubunge mara moja ajenge upya heshima yake ya kisiasa. Mtaalamu mmoja wa mambo ya siasa ametoa angalizo kuwa endapo Ndugai atakaidi kufanya hivyo kuna uwezekano jina lake likakatwa mwaka 2025 hivyo kuzikwa kabisa kisiasa. “Ni vizuri acheze karata zake vizuri sasa ikiwa bado anatamani kuwa kiongozi mkubwa zaidi katika nchi siku za usoni, hata ikibidi siku moja wananchi tumchague kuwa Rais wetu”. Alionya.
Ada ya mja hunena: muungwana ni vitendo. Kwa kuwa tayari ameonyesha uungwana wa kutosha amejiuzulu uspika haifai chochote ikiwa atang’ang’ania kuendelea na ubunge wake ilhali tayari heshima yake ya kisiasa ilishashuka mno. Hatakuwa tofauti na Profesa Muhongo ambaye tangu atenguliwa kutoka nafasi ya uwaziri amekuwa mpole kama kinda la ndege lililonyeshewa na mvua ya mawe. Ndugai naye amefikia hatua hii. Saa ya kufanya uamuzi ni leo, asisubiri kesho.