dahhh, mwj1 nilipitiwa na kausingizi kidogo hapa...ngoja nikujibu ifuatavyo...
kesi ya 1stleft- arusha, nilishawahi muonya soulmate wangu mimi sio mtu wa
bar na pubs... sasa yeye akanilazimisha ati tukienda huko nitapata mtori safi kabisa...
matokeo yake nikajikuta namshangaa dada poa alivyokuwa ananishangaa...
sijui alinifananisha?
kuhusu mdada kukatazwa kuongea na shoga wake wa miaka nenda rudi, huwezi jua bana...
nitakupa mfano mmoja. mimi nawe tupo kwenye mahusiano...halafu nikakutambulisha kwa
best wangu ambaye pamoja na sifa zake za ucheshi, nakwambia nimetoka naye mbali sana huyu...
hata mademu wote alikuwa ananiunganishia yeye, ndio mtunza siri wangu huyu...
utaniruhusu kwa roho nyeupe niendelee nae urafiki bila mashaka?