Haiwezekani Wasabato kuhubiri neno la Mungu bila kutaja Kanisa Katoliki? Au ni mafunuo? au mbinu za kupata na kutunza wafuasi?

Hoja ya msingi ilipaswa kuwa "WOKOVU".

Hakuna kanisa litakalompeleka mtu kwa Mungu bila yeye binafsi kuwa na uhusiano chanya na Mungu wake.

Hayo mengine kama ushoga, uzinzi n.k ni maovu yanafanywa na baadhi ya wafuasi wa kila imani wakiwemo wasabato.

Ukiokolewa kwa neema na kuishi katika usafi wa kiroho na nafsi hapo ndo uko salama.
Wokovu siyo mali ya wasabato pekee wala kundi flani kwa njia ya kujihesabia haki.

Madhehebu ni kama magari tu ya kusafiria ila mbinguni hayapo.

Hivyo, tutafute kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao pasipokuwa nao hatutaurithi ufalme wa MUNGU.
 
Nani kakuambia yote hayo?
 
Huwezi kuwa mtu wa MUNGU bila sabatho.waebrania 4;9 imesalia raha ya sabato kwa watu wa MUNGU. Je km huna sabatho unaweza kuwa mtu wa MUNGU? JIBU NI HAPANA kwa sababu tumeonya tusije tukaasi sabatho waebrania 4:10
Tafuta WOKOVU usitafute sabato.

Mungu hafungwi na siku.

Kol 2:16-17​

Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
 
Huwezi kuwa mtu wa MUNGU bila sabatho.waebrania 4;9 imesalia raha ya sabato kwa watu wa MUNGU. Je km huna sabatho unaweza kuwa mtu wa MUNGU? JIBU NI HAPANA kwa sababu tumeonya tusije tukaasi sabatho waebrania 4:10
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,

20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,


21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.


22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
Wagalatia 5:19- 23
 
Hivi hakuna wasabato wenye dhambi? Au usabato nao unafurahia dhambi?
 
Ndio mana wakaitwa wasabato hiyo ndio identity yao ni wapinzani wa ukatoliki,wasabato wanajihesabia haki hawanayofauti na mafalisayo.
 


14 Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Wagalatia 5:14
 
Wasabato wanazingua kuwashambulia RC. Wangejikita kueneza imani yao kugusa imani ya wengine. Sema kwa upande ukiwatazama RC nao ukakasi mwingi sana. Imagine watu waliokuwa wakiungama kwa padri aliyeshiriki mauaji ya mtoto Albino? RC acheni watu waungame kwa Mungu moja kwa moja na sio kupitia kwa hawa binadamu wenzetu wanaonuka dhambi. Pia RC ni kama tu serikali... wana TISS yao inaitwa Jesuits. Hili kanisa lina mambo mengi sana mengine ya kutisha. Hakuna kiongozi chini ya jua anayeweza kumzingua Papa wa RC. Hata hawa mapadri na maaskofu tu ni ngumu kuzinguliwa na serikali kwenye nchi walizopo. RC wanawadharau SDA kwa sababu SDA haenei hata kwenye kiganja endapo RC ataamua kujibu mapigo.
 
Wewe ,wewee, narudia , weweee.

Mungu Si mwanadam wala utawala wake sio wa kidemokrasiaa.

Yeye ni mfalme, Bwana wa Mabwana , akisema amesema.

Wala Agizo lake halihitaji kujadiliwa.
 
Wewe husomi biblia takatifu?? Kama husomi ,huwezi mjua Mungu.

Mungu ni msabato kabisaaa nayeye anajiita Bwana wa Sabato.
Duuh Mungu ni msabato? Hivi unaelewa maana ya sabato wewe? Umesoma vizuri kwa nini Yesu alisema yeye ndiye Bwana wa Sabato?

By the way kwenye Biblia sabato haikutajwa kama dini,wala dhehebu (sasa unavyosema Mungu ni msabato nashangaa),Sabato maana yake ni siku ya kupumzika yaani ni PUMZIKO. (Kutoka 20:11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo,) akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Halafu kasome Biblia vizuri utaona jinsi Mafarisayo walivyokuwa wameifanya Sabato kama mzigo yani walistaajabu jinsi wanafunzi walivyovunja masuke wakala, na pia Yesu alivyomponya yule mtu aliyekuwa amepooza kwa kuwa ilikuwa ni sabato, Lakini je yesu alwajibu nini? Kasome Matahayo sura ya 12 utaelewa ndiyo maana yesu aliwaambia yeye ni Bwana wa Sabato.

Halafu ukisoma( Kutoka 12:16] Siku ya kwanza kutakuwa kwenu na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa kusanyiko takatifu; haitafanywa kazi yo yote katika siku hizo, isipokuwa kwa hiyo ambayo kila mtu hana budi kula, hiyo tu ifanyike kwenu.) Utaelewa kwa nini wengine wanasali jumapili maana zote Mungu aliagiza ziwe siku ya sabato,, Sasa ninyi mnaowasema wanaosali jumapili hivi mnafikiri Mbinguni tutaenda kwa madhehebu?

Tuache dhambi ,tutende mema, tupendane,tushirikiane kuujenga mwili wa kristo na tuache kuabudu makanisa, Yesu anasema ufalme ukifitinika juu ya ufalme mwenzake hauwezi kusimama..Sasa kama ukristo unaanza kufitinika juu ya ukristo hapo je,tunaujenga mwili wa kristo? Tuungane kukemea dhambi na siyo kujiona kuwa huyu ni bora kuliko mwenzake..Yesu hakuja kutukomboa kwa ajili haya tunayofanya.
 
Alafu hata hawajibiwi.

Inauma sana ukijipanga kwa vita kwa silaha kibao alafu adui yako anakudharau.

I think what they do not know, is the Catholic church was the first church and with her, the church has the advantage of knowing the knowledge which they claim to know better.
If you look well into catholism, they have started a lot of things that others have copied in science, culture, and other social settings.
When Martin Luther rejected catholic teachings, a lot in Europe thought it was the beginning of the end. But with big surprises, the strength of the church continued with innumerabile worth and power.
Even now, when the enemy has penetrated its element with the Catholic church, some souls will face eternal damnation. But not the Catholic faith.
 
Nilikuwa nina kademu kanasali Sabato.
Duh kana masheria kama yoote.
Kanalalamika kutumiwa na kuacha
Kajuaji,ukikarekebisha kanaongeaa hakoo
Nimedumu nako miezi 5, nimepiga chini
 
Wewe umejaa chuki dhidi ya Wasabato. Post zako zote ni kuwasimanga wasabato na kuwanenea mabaya. Acha kueneza chuki. Wasabato wanahubiri kilichopo kwenye Biblia, kwa nini wewe uumie?? Acha chuki, haitakusaidia katika imani hako
 
Nimewasikiliza, unalosema si kweli. Wana mafundisho mengi sana bila kutaja ukatoliki. Kama, hukumu, zaka na sadaka, Uungu wa Yesu, Ubatizo, kifo, Roho mtakatifu nk. Ila walipofundisha Sabato walitaka aliyebadili na kuiweka Jumapili, siku ya ibada ya upagani. Usipowaelewa utaona wanakashifu ila wanasimamia ukweli wa maandiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…