Haja ya kubadili Katiba ya Kenya

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Nawapongeza sana raia wa Kenya kwa kuwa mawazo dynamic kuhusu katiba yao. Siyo kama katiba ya Tanzania ambayo inaonekana kama untouchable pamoja na mapungufu yake.

Nawapongeza sana raia wa Kenya kwa kuwa mawazo dynamic kuhusu katiba yao. Siyo kama katiba ya Tanzania ambayo inaonekana kama untouchable pamoja na mapungufu yake.

Katiba ya ufipa tu haijabadilika mwenyekiti ni yuleyule miaka kumi na kitu ... halafu mnataka katiba ya nchi ibadilike mtakavyo nyinyi
 
Katiba ya ufipa tu haijabadilika mwenyekiti ni yuleyule miaka kumi na kitu ... halafu mnataka katiba ya nchi ibadilike mtakavyo nyinyi
Majibu ya kipumbavu kama haya lazima yanatoka kwa mtu ambaye kichwa chake kimejaa maji ya nazi. Mimi nimeleta link ya Voice of America inayoongelea Katiba ya Kenya, na nikaweka comment yangu kuwapongeza kwani ni kweli Katiba ya Kenya iliandikwa upya miaka michache tu iliyopita, na tayari wamesheona mapungufu na wanataka wayashughulikia mara moja. Katiba ya Tanzania iliandikwa miaka 42 iliyopita na kufanyiwa viraka vidogo mwaka 2005, na dunia imebadilika lakini bado katiba ni ile ile. Sasa badala ya kunijibu mimi binafsi kwa kutokana comment yangu hiyo, ananiletea lugha ya blanket inayoashiria uoga wa hoja kwa kusema "mnataka;" kwani ni wangapi tulioweka post hiyo? Wala sikusema ninataka, nili-comment kuhusu taifa kubadili katiba kulingana na mazingira. Halafu katiba ya ufipa inahusianaina nini na post yangu? Ana mzigo mkubwa sana huyu wa kubeba madebe matupu juu ya shingo lake.
 
Basi kichwa kilikuwa kinafaa kuwa 'haja ya kubadili katiba ya Tanzania' au vipi kaka?
 
Basi kichwa kilikuwa kinafaa kuwa 'haja ya kubadili katiba ya Tanzania' au vipi kaka?
Hiyo inaweza kuwa sawa lakini mimi nilililteta kwenye jukwaa la Kenya kwa ajili ya kuwapongeza wakenya, na nilitumia heading ile ile ya Voice of America. Nilchhoongezea ni kujilinganisha nao, tena kwa sentensi moja tu.
 
Me najifunza, kubadilisha katiba sio overall solution. So I support magufuli kwa kuwa muwazi na kusema hatoshughulika nayo.
Na kwanini libadilishwe lote badala ya kubadilisha vifungu vyenye changamoto kwenye hali ya kisiasa ya sasa.
 
Ukisikia mabadiliko ya katiba, kwa lugha za wanasheria nadhani wanasema Constitutional Amendment, maana yaks ni kuichukua Katiba iliyopo na kuipitia upya note. Vifungu Vibaya vinarekebishwa an vile vizuri vinabaki. Hata Kenya walipoandika katiba yao upya Kuna vifungu vingi ambavyo hawakubadilisha, kwa mfano bado uchaguzi mkuu ni baada ya miaka mitano, na amiri jeshi mkuu bado ni Rais.
 
Hahaha ufipa wana tetemekaa wakishikiliwa na ndugu zao wa kenya
 
Mleta mada una point. Kwenye katiba mpya ya Kenya 2010, kuna vifungo humo ndani ambavyo vinaeleza kuhusu marekebisho kwenye katiba, jinsi ya kufanya marekebisho, sheria ambazo lazima zizingatiwe wakati wa kufanya marekebisho n.k., n.k. Katiba lazima iendane na nyakati, iwe ni katiba mpya au ya zamani kama ya Tz. Katiba sio sheria kama zile ambazo zilichongwa kwenye mawe na kukabidhiwa Musa akiwa mlimani.
 
Acha kumuita mwenzie Mpumbavu kabla hujaona Upumbavu wako wenyewe
Kama ulitaka Izungumziwe Kenya Umeitaja Tanzania yanini
Katiba ni katiba iwe ya Nchi au chama
Kwa Tanzania Bado vyama ndio vinaleta viongozi Asa kama Vyama vinaongozwa kiboya boya unategemea nini!!
Rais atoke kwenye chama chenye Katiba yahovyo Si ataharibu hata aiming hiyo unayo izungumzia!
Hebu jiulize Katiba yao Kenya inamiaka michache sana leo wanaiona Haifai huo si ufujaji wa pesa ya umma!
Kwa Africa bado sana Kila mmoja anauchu wa madaraka akiona Katiba inambana lazima aipinge
 
Kenya inanuia kufanya ammendments(marekebisho) kwenye katiba, sio kutupilia kabisa katiba mpya ya Kenya. Naona porojo zimeanza kuenezwa, na wale wajuaji wa kawaida kwenye jukwaa hili.
 
(1) Na wewe uko kama yeye? (2) Kwako wewe kuboresha kitu chako huwa unachukulia kuwa ni kupoteza hela?
 
Sikujua kuwa Millenials wa Kenya mnaongea kiswahili kizuri sana. Nilikaa Nairobi kwa muda mfupi sana miaka ya tisini na bado nakumbuka kiswahili kilichokuwa kinaongewa hapo. Leo hii nimewasikieni mnaongea kiswahili utadhani mko kwenye mitaa ya Dar-es Salaam. Hongereni sana sana; ni kweli kuwa mna uwezo kabisa wa kufundisha kiswahili huko nchi za nje.
 
Kenya inanuia kufanya ammendments(marekebisho) kwenye katiba, sio kutupilia kabisa katiba mpya ya Kenya. Naona porojo zimeanza kuenezwa, na wale wajuaji wa kawaida kwenye jukwaa hili.
Kwani kuna tofauti gani za kimsing kati ya marekebisho na mabadiliko?
 
Kwani kuna tofauti gani za kimsing kati ya marekebisho na mabadiliko?
Hamna, ila kuna comment moja hapo nimeona wakisema kwamba tayari wakenya wanaona katiba yao haifai. Eti na ni ufujaji wa pesa za umma kutupilia mbali katiba mpya kama ya Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…