Point The Boss, swala la talaka, hasa pale mwanamke anapotaka kuachana na mumewe, mara nyingi linakuwa na kizungumkuti, kwa mwanaume ni rahisi kuamua na kutekeleza, lakini pia kunakuwa na ugumu zaidi hasa kama wahusika watahusisha mali walizochuma kipindi cha ndoa, kama mwanaume ndiye aliyekuwa mchumaji mkuu, swala la kutoa talaka kwake litakuwa gumu kwa maana ya kujali zaidi zile mali. kwani moja kwa moja atajua kuwa kuna kugawana mali na kwa mwanamke kama yeye ndiye aliyekuwa mchumaji mkuu, atawaza 'yaani niondoke halafu hizi malia aje kuafaidi mwingine'
Lakini hata pale mke atakapoonesha kutojali hizo mali na kutaka kuachana na mume, bado kutakuwa na usumbufu wa hali ya juu, wote tunajua jinsi maswala ya kisheria yalivyo magumu hapa nchini na ndio maana wengine hufikia kuondoka na kwenda kuanza maisha upya. Je akipata mume mwingine ndio asiolewe?.............. Bado nauliza sheria inamlindaje huyu mwanamke.