Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Naiona Tanzania ya kipekee sana baada ya Tundu Antipass Lissu kushinda uenyekiti Chadema.
Tundu Antipass Lissu aliyesoma shule ya vipaji maalum ya Ilboru na akasoma Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadae nchini Uingereza amethibitisha kuwa yeye ni zawadi ya kipekee kwa Watanzania kutoka kwa Mungu.
Ni mtu aliyenyooka sana, ambaye kamwe hawezi pindisha ukweli. Ni mtu anayeamini kwenye haki kweli. Ni mtu anayeweza kuutetea ukweli kwa nguvu zote na kwa gharama yeyote ile. Ushahidi ni hili ni namna alivyopata ulemavu wa maisha kutokana na kuutetea ukweli na haki.
Furaha yangu kuhusu Lissu kuwa Mwenyekiti wa Chadema katika kipindi ni kwa sababu najua Lissu ataenda kuongoza vuguvugu la Katiba Mpya nchini Tanzania. Katiba ambayo itaweka mustakabali mpya wa nchi kwa miaka mingi ijayo.
Nikimuangalia Lissu kila siku nasema neno moja tu " Mungu ni Mkuu ". Ingawa sina uhakika kama atakuja kuwa Rais wa Tanzania ila kwa hakika ninajua Lissu ni messenger wa Mungu kwa Tanzania na Mungu anaenda kumtumia kuipa Tanzania zawadi kubwa sana ambayo ni Katiba Bora yenye misingi na inayojenga mifumo imara.