Haji Manara: Ahmed Ally ni shabiki kindakindaki wa Yanga

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Posts
941
Reaction score
2,062
Katika muendelezo wa tambo mbali mbali za Simba na Yanga pindi ukiotewa pale ambapo pana mshono hakika nawe lazima ukajipange kuja kurudisha mashambilizi.

Picha ya zamani ya Ahmed Ally akiwa ameshika kombe la Yanga sasa imetumiwa vizuri na Manara kwenye kuwaaminisha wananchi kuwa Ahmed naye pia ni mpenzi wa Yanga japo yupo Simba kwenye kujitafuta

Manara ameandika β€œNakiri kwamba hata mimi wakati najitafuta, niliibukia kuwa Mfuasi feki wa Madunduka, na ilifika mahali nikawa nawacharura mno Yanga hadi mimi mwenyewe ilikuwa inanikera, lakini ndio kujitafuta huko, ningefanyaje ndugu zangu? Na bila kufanya hivyo GSM wangenionaje? Ile Siku waliyoniambia rudi home sasa, ooohh ilikuwa siku kubwa sana kwangu, SITASAHAU

Basi bhana Wakulungwa, ndio story ya huyu kijana mkazi wa Tambuka Reli, kelele na kebehi zote anazosema dhidi yetu, ichukuliwe ni kwenye kujitafuta na kujipapatua tu, huyu anaumwa na Yanga yake, hali hata Chakula siku Wananchi wakiwa wanacheza, Kigosi na Jimmy Mafufu waliwahi kuniambia walikuwa wanampa hadi hirizi kuvaa, siku ya mechi ya Yanga.

Miaka ya nyuma ilikuwa kila asubuhi anaenda Jangwani kubusu na kupiga picha na Makombe yetu, na akifika tu anaamkia, Shikamoo Makombe[emoji12] na Wazee wetu pale klabuni walikuwa wanampenda kwa ule usafi wake wa kusafisha kila siku Makombe yetu, hadi Jiki alikuwa anayaoshea.[emoji2957]

Kwa hiyo msameheni Wanayanga, anajitafuta tu, ni kijana wetu mzuri na ana msaada mkubwa kwetu, Mtu wa maana sana na ni familia kabisa, Soon Mtanielewa Wananchi”

 
kelele na kebehi zote anazosema dhidi yetu,ichukuliwe ni kwenye kujitafuta na kujipapatua tu
Leo ndio nimejua kuwa kebehi za semaji la Simba huwakera 🐸🐸.

Nimejua pia Manara bado ana uchungu wa kuondolewa katika nafasi ya usemaji hapo Simba.

Madam Barbara popote ulipo ubarikiwe sana kwa kuchukua uamuzi wa kumfyekelea mbali huyo amphibian Manara 😁
 
Manara pamoja na kuzeeka lakini bado anaishi kwa kufitinisha watu. Hajifunzi kabisa kwa kuondoka Simba kwenda Yanga. Juzi tu alikuwa anafitinisha Mpenja na Ghalib Mzinga. Hili zee ni hopeless
Ndio anaishi mjini kwa namna hiyo. Kila siku jamaa anatafuta bifu na watu tu. Nimeona anapambana na kumshambulia Ally Kamwe sasa baada ya Kamwe kuwasiliana na Mpenja. Ye ni vita tu na kila mtu.
 
Ila hii picha inamuonesha kabisa huyu dogo ni Mwananchi eti!! Sema tu ndiyo hivyo! Ameamua kujitafutia mkate wake wa kila siku mahali pengine.

Yaani ni sawa na kusema eti Ali Kiba ni Simba!! Aisee nitakataa milele. Huko yuko kwa ajili ya pesa tu. Ila mapenzi yake yote yatabakia kuwa Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…