Haji Manara alivyotoa chozi jana kuwalilia viongozi wake!

Atalia sana msimu huu kwa dozi watakazo pata kutoka jangwani
 
Nawaza tu.leo tarehe 30.mpaka tarehe 13 sio mchezo.
 
Wakati Manji anasulubiwa yeye kwake ilikuwa kicheko hakujua kuwa dunia haina mwenyewe. Mzee wa kaya ni noma. arejee klabuni akakomae na usajili wa NIYOO
 
Mimi ni tea Simba ila toka Huyu Manara ajitokeze kushadadia Suala la wanyama kupewa mtaa nilimwona mtu wa hovyo sanaaaa. Wacha waisome namba walizoea vya bure na kumpa MO team walikuwa wanapiga danadana tu ili wapate cha juu.
 
asilie mchezo 10% kwishney bado MO ajiandae kisaikolojia nae atanyooshwa soon walishaambiwa watafute team zingine waachane na simba na yanga hawasikii wamuulize Hans Pop yaliyomkuta
 
Kilio kinaashiriaga vitu vingi..labda posho ndio basi tena..

Pole Manara
 
Anavuta hisia pesa walivyokuwa wakizipiga
 
Mbona unaudanganya umma wa michezo Haji Manara siyo msemaji wa simba alishafungiwa kujihusisha na masuala ya michezo
 
SONG: JELA
ARTISTS: Aveva & Kaburu feat Han Pope
PRODUCER:TAKUKURU
STUDIO: JPM RECORDS


Tangu tufungwe siku ya tatu imefikaa.
Bora leo hii Hans Pope wetu umefikaa.
Tupe japo repoti za usajiri msimbazii.
Twasikia Ngoma ametuacha mdomo wazii.

Kusema kweli mambo sasa magumuu.
Haruna nae ata hapokei yetu simu.
Si unamkumbuka yule Tambwe mabaooo.
Naye kabaki Yanga sasa mwendo wa mabaoo.

Kwa hali hii sasa ubingwa hatupati tenaa.
Na mwaka huu watalibeba tena mapemaaa.
Mo afanye ile mipango yetu.
Ili japo tupate nafasi ya tatu.

Hivi ni kipi hasa kisa na mkasaa?
Kilicho fanya mpaka sasa mpo hapa?
Nasikia eti mpeiba nyingi pesa.
Hiyo ni kweli hatuwezi kubishaa.

KIITIKIO:
Iiiiiiiiiii manara nyamaza weweeee!!!!
Iiiiiiiiiii nyamaza acha kuliaa!!!!!
 
Mbona unaudanganya umma wa michezo Haji Manara siyo msemaji wa simba alishafungiwa kujihusisha na masuala ya michezo
Amepewa adhabu na hadhabu ikiisha atarudi kwenye majukumu yake.
Au Simba wamemfukuza kazi?
Maana bado anapokea mshahara wa Simba akiwa kama msemaji.
Au kiswahili mwenzetu kipo kushoto?
 
Nawaza tu.leo tarehe 30.mpaka tarehe 13 sio mchezo.
Wacha wapete cha moto hizi club kongwe zinakaribia kutimiza miaka 100 hazina Hata uwanja wa mazoezi kisa zinaongozwa na wanyonyaji na wezi? Kwa hili sina ushabiki wala upande kiongozi mwizi mnyonyaji fisadi awe simba au yanga hafai mahali pake ni jela. Tena hawa wa Simba wakipatikana na Hata Mali zao zichukuliwe zikajenge ule uwanja kule Bunju
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…