Haji Manara amuwakia vilivyo Shafii Dauda, amwambia asitafute ugomvi na wanasimba wote

Haji Manara amuwakia vilivyo Shafii Dauda, amwambia asitafute ugomvi na wanasimba wote

Kufungwa ufungwe na mwingine povu umtoleee mwandishi wa habari

Haji punguza hasira vichapo vingine vyaja ngoja ligi ianze
 
Haji ana propaganda ambazo wanasimba kwa umbumbu wao wanamuunga mkono walikosa ubingwa wakawaonyesha hadi parcel ya DHL kwenda Fifa;walifungwa akamfanya Malinzi ndio kishushia pressure then baadae Omog naona sasa hivi amempata Shaffih
 
da433997a1a5cdb5d27012a3db3f2846.jpg
Msemaji wa Simba anautwika mtindi.
 
Povu la Haji Manara kwa Shaffih Dauda

"Tunajua ww una ugomvi wako binafsi na baadhi ya viongozi wa Simba.lakini usitafute ugomvi na wanasimba wote,Sie kufungwa sio wa kwanza na hatutakuwa wa mwisho.unatumia muda mrefu kuittack Simba na post zako za kijinga.kumbuka ww upo kwenye chombo cha habari na klabu yetu inaiheshimu sana cloudstv na mabosi wake rugemutahaba na josephkusaga, na tunajua unajikomba kwa Yanga baada ya kutaka kukupiga kwenye issue ya Akilimali..jipime bro vnginevyo utavunja heshma yako na ya clouds media pia..ila ukiona vp endelea ila jua Simba ni klabu kubwa sana" - Haji Manara kupitia mtandao wa Instagram.
Inapofikia mchambuzi mmojawapo mkubwa wa soka ndani ya nchi analumbana na msemaji mmojawapo mkubwa wa klabu mojawapo kubwa ya soka nchini, tujue ni tatizo. Hali hii inatoa taswira sahihi ya soka la nchi yetu, kwamba hatuwezi kupata uongozi thabiti wa soka kwa sababu hatuna wadau thabiti wa soka. Lakini ajabu hao ndio wadau wanaotaka vilabu na timu zetu ziwe na viwango vya juu. Kama mwandishi uwezo wake ni kukosoa kila mdau wa mpira isipokuwa waandishi wenzake, na kama kiongozi wa klabu kazi yake ni kukosoa kila mdau wa mpira isispokiwa kiongozi mwenzake wa klabu, na kama kila shabiki wa mpira kazi yake ni kukosoa kila mdau wa mpira isipokuwa shabiki mwenzake kwenye timu, nani ataona na kuondoa kasoro za kweli kwenye soka letu? Na iwapo kila mdau anayekosolewa atapingana na kila analokosolewa, marekebisho kuelekea hatua ya juu zaidi ya soka letu yatafanyikaje? Mwandishi anamlaumu mchezaji kwamba hana mikakati ya kuenda Ulaya, kama kwamba changamoto zote za mchezaji kufikia huko ni za kiuchezaji tu. Shabiki anamlaumu mchezaji kwa kutomwona mwenzake aliye nafasi bora zaidi ya kufunga goli, ilhali yeye (shabiki) mwenyewe akitoka uwanjani anashindwa kuona alikoweka kipando chake mita chache kutoka alipoingia! Mwandishi anayepoteza muda kwa kupeana mipasho na kiongozi wa timu, atakuwa na muda wa kutafiti makala yenye tija? Kiongozi anayetamani kusifiwa kwa kulumbana na wakosoaji wa timu yake, atakuwa na muda wa kufuatilia mwenendo wa timu yake na kutoa mchango wenye tija? Tunataka uongozi makini wa soka nchini bila ya kujenga misingi makini ya uongozi wenyewe, si ndoto za Alinacha hizo?
 
Haji ana propaganda ambazo wanasimba kwa umbumbu wao wanamuunga mkono walikosa ubingwa wakawaonyesha hadi parcel ya DHL kwenda Fifa;walifungwa akamfanya Malinzi ndio kishushia pressure then baadae Omog naona sasa hivi amempata Shaffih
Wewe ndio mbumbumbu mpumbavu kabisa wewe huna adabu
 
Tatizo lingine linaloikumba Simba ni Haji Manara, huyu sio tu kwamba ni mbumbumbu bali pia ni mshamba wa viwango vya kigodoro.
Msemaji asiyetaka timu yake ikosolewe ila isifiwe tu hata pale inapoboronga, anataka katika kipindi hiki cha uwazi watu wasimpige picha Kichuya alipokacha benchi na kwenda zake kula mziki?
Ndo maana anamfagilia sana fid q wa chato
 
hivi kesi ya RUSHWA dhidi ya SHAFII DAUDA aliyokumbana nayokumbana nayo kule Mwanza wakati wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa TFF Iliishia wapi?
 
Back
Top Bottom