Haji Manara anapaswa kumuachia Ally Kamwe kuwa msemaji mkuu wa Yanga sc, kwa maana wakati wake umeisha (umepita)

Haji Manara anapaswa kumuachia Ally Kamwe kuwa msemaji mkuu wa Yanga sc, kwa maana wakati wake umeisha (umepita)

Mbona kazi ya Afisa habari na Msemaji ni tofauti kabisa.
Afisa habari haiishii kuisemea Clabu kwa mdomo tu.
Ni Bosi wa Habari zote za kwenye majarida na mitandaoni.
Msemaji ni muongeaji tu chini ya Afisa habari.
Tatizo ni kwamba wote wawili wanapenda waonekane hadharani. Ukijipa uboss ukawa ni msimamizi tu, ni camera chache tu zitakazokumulika na kukusambaza mitandaoni. Ni suala la maslahi binafsi tu hapo
 
Kila kitabu na zama zake , Haji Manara alikua moto sana kipindi anashindana na Murro wakati Haji akiwa Simba sc na Muro akiwa msemaji wa Yanga hakika nilishuhudia na kusikia maneno yenye mbwembwe na kejeli humo humo ndani yake hakika gemu ilichangamka mno tena mno na hiyo yote kwa kua walikua wanaendana.

Kwa sasa Manara karudi ni kama vile Leonel Mess arudi laliga bila ya Ronaldo kisha aanze kushindana mwenywe pasipo kuwa na upinzani huo ni mfano simaanishi kuwa Manara ni mkali sana la hasha bali nasema Manara zama zake zimepita sasa atafute shughuli zingine pale Yanga mambo ya usemaji amuachie Ally Kamwe.

Naambatanisha sababu kuu maalumu za kusema kuwa Haji Manara apumnzike na kumuachia Ally Kamwe

(1) Wakati wake umekwisha, nilimtazama Manara mwananchi day kwa jicho la tatu niligundua jamaa anafosi tu lakini hakuna kitu, Ally Kamwe alishawaandaa mashabiki na tayari wamemuelewa kurudi kwa Manara ni kama vile kaja kuanza kutengeneza upya .

Mbwembwe za Ahmedy Ally na Ally Kamwe zimeendana na ndiyo kitabu kipya kwenye soka la bongo na siyo haji Manara kuja kubishana na Ahmedy Ally ni vitu viwili tofauti kwa ufupi Manara kitabu chake kimepita amuachie Alli Kamwe.

(2) Manara anafanya kazi kwa kisasi, hili lipo wazi jamaa anafanya kazi kwa kulipiza kisasi tena mambo yake binafsi anayoyajua mwenyewe huko alikotoka sasa hii siyo nzuri katika taasisi kubwa kama Yanga akiropoka neno ni kama yanga ndiyo imeropoka na inakua haileti picha nzuri kwa viongozi wa yanga na taasisi nzima, kwa hili amuachie bwana mdogo tu halina ubishi.

(3) Anapiga dili binafsi za kipuuzi na kitoto kupitia platform ya Yanga, labda mjinga tu ndiyo hakuelewa kwa nini hamisa alitajwa sana pale jukwaani na kuitwa apande juu avalishwe jezi ya yanga na azizi k hiyo ni biashara kati ya Hamisa na Haji na ndiyo maana Azam waliikata hawakutaka kuonesha upuuzi kama huo usiokuwa na faida kwao, kiufupi huo ni ujinga wa hali ya juu kufanyika kwenye jukwaa kubwa kama lile kisa tu mtu kabeba pesa ya maji ya kunywa ili amtaje taje mtu.

Natumia jukwaa hili kubwa la wanamichezo kufikisha ujumbe huu kwa viongozi wa Yanga sc kuwa wamtafutie Haji Manara kazi nyingine ya kufanya usemaji wamuache bwana mdogo Ally kamwe aendeleze gurudumu la kutuburudisha wanayanga kwani tunahitaji damu changa na vijana wabunifu kama Ally Kamwe.
Umeongezeka wa 4 mwenye akili kule utopoloni
 
Mbona kazi ya Afisa habari na Msemaji ni tofauti kabisa.
Afisa habari haiishii kuisemea Clabu kwa mdomo tu.
Ni Bosi wa Habari zote za kwenye majarida na mitandaoni.

Msemaji ni muongeaji tu chini ya Afisa habari.
Kumaanisha Kamwe ni Boss wa Manara. Kitu ambacho Manara anakipinga.
 
Manara is in denial. Alichotarajia kukipata kimapokezi ni kinyume kabisa na alichokutana nacho.

Miaka 2 ya kukaa nje ya game yamedhihirishia game kuwa haikuwa ikimuhitaji Manara.

Manara had been obsolete for long lakini mazingira hayakumpa wasaa wakudhihirika u obsolesce wake mpaka pale alipofungiwa.

Manara yupo jopo moja na kina Mzee Magoma, hawataki kukubali kuwa wakati umebadilika na hawahitajiki tena.
NAUNGA MKONO MKUU
 
Umedadavua vema...!

Na Kwakua Kila atakayekuja kuchangia hii hoja atasema namuunga mkono mtoa Mada.!


Naomba huu Uzi mods Wauhifadhi Kwa Marejeo, Waugonge Muhuri halafu Waufunge!

Kuna Nyakati Wana Yanga Akili huwa zinawarudia ee.! Sio kama alivyosema Manara kuwa Walibakiaga Wawili tu Wenyenazo.!
UMEANZA VIZURI LAKINI UMEMALIZA VIBAYA 😁
 
Back
Top Bottom