Haji Manara atakiwa kulipa Tsh. Milioni 10 ndani ya siku 30

Haji Manara atakiwa kulipa Tsh. Milioni 10 ndani ya siku 30

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamati ya Rufaa na Maadili ya Shirikisho la Soka nchini TFF chini ya Mwenyekiti wake Richard Mbaruku imempungizia adhabu Msemaji wa klabu ya Yanga, Haji Manara kutoka Tsh. Milioni 20 hadi Milioni 10.

Adhabu ya kifungo cha miaka miwili ya kutojihusisha na masuala ya Mpira ndani na nje ya nchi inaendelea.

Manara ameagizwa kulipa dola 4361.10 au Tsh. Milioni 10 ndani ya siku 30 kuanzia leo Septemba 14, 2022.
 
Hawa TFF hawajielewi, wakiwa na kigugumizi cha aina hii kwenye hukumu zao ndio inasababisha watu wawadharau, sioni sababu ya kupunguza adhabu, hiyo maana yake wamethibitisha wanaotoa adhabu huwa wanakurupuka, na hii itawafanya walalamikiwe zaidi mbele ya safari kwenye hukumu zao.
 
Hiyo pesa sio lazima Manara alipe, na hakuna watakachomfanya sababu hiyo kamati ya TFF sio mahakama ya kiserikali...

Kutojihusisha na mchezo wa mpira wa miguu hakuwezi mfanya mtu ashindwe kuishi...
 
Hawa TFF hawajielewi, wakiwa na kigugumizi cha aina hii kwenye hukumu zao ndio inasababisha watu wawadharau, sioni sababu ya kupunguza adhabu, hiyo maana yake wamethibitisha wanaotoa adhabu huwa wanakurupuka, na hii itawafanya walalamikiwe zaidi mbele ya safari kwenye hukumu zao.
Hizi Kamati zinatakiwa ni External Committee Ili Ziwe Free kwenye Decision Zao.
.
Wajumbe wote wa Kamati hizo za Tff Wanateuliwa na Karia na Jopo lake, How comes wawe Against Nae.
.
Hakuna Haki Kwenye hizo Kamati Maana hawako neutral Kwenye decision Zao.
 
Hiyo pesa sio lazima Manara alipe, na hakuna watakachomfanya sababu hiyo kama ya TFF sio mahakama ya kiserikali...

Kutojihisisha na mchezo wa mpira wa miguu hakuwezi mfanya mtu ashindwe kuishi...
Yes Adhabu Zao haziko executed Kwa Sababu Wao Sio Judicial board
 
Wanapunguza faini kutoka 20M mpaka 10M na deadline juu ya 30 days huku Adhabu ya msingi ya kifungo cha kutokujihusisha na soka kwa miaka miwili kipo pale pale!!

Je,asipolipa hyo PESA ndani ya hzo siku 30 nini kitatokea??Kamati imeweka wazi au itakuja kukaa tena??
 
Manara anakosa kazi kwa miaka miwili halafu wao wanataka walipwe hizo pesa atatoa wapi ? Huyu alshabab tumbotumbo hanaga akili kabisa

Sent from my CPH1823 using JamiiForums mobile app
Mpira sio siasa CAF na FIFA faini zao na vifungo vyao ni vikubwa mno ,ulimwengu wa mpira unajitegemea kufungiwa maisha ni jambo la kawaida ,kama hautaki nenda CAS na ukuenda huko ni walewale tu.
 
Umekuwa msemaji wa msemaji Manara

Ukweli ndio huo, TFF na kamati yake uwezo wa mamlaka yake umeishia hapo tu...

Hiyo pesa anaweza asilipe, na akaachana kabisa na ishu za soka...
 
Back
Top Bottom