Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,775
- 29,746
Shirikisho la Mpira Tanzania linatakiwa kuchukua hatua kali zaidi kwa @hajismanara kwasababu ameendelea kukiuka adhabu aliyopewa ya kufungiwa miaka miwili. Hii ni dhihaka kubwa kwa chombo chetu cha kusimamia mpira nchini na kwa Wizara ya Michezo kwa ujumla wake, lakini inavuka na kudhalilisha utawala wa kisheria nchini.
Manara amefanya tukio la uvunjifu siku ya Wananchi wiki mbili zilizopita, Wakati TFF ikiwa tayari imemfikisha upya kwenye kamati ya nidhamu kwa mara nyingine, jana pia amekiuka na kuendelea kuwa msemaji wa Yanga akiuzungumzia mkataba wa Yanga na Jackson Group.
Narudia tena kushauri mamlaka za soka nchini @tanfootball kwamba Mpira huu wasipodhibitiwa watu wahuni kama huyu Manara basi tusahau mageuzi na uwekezaji ulioanza kujitokeza sasa. Mpira ni biashara kubwa sasa, Ni sekta inayoajiri na kulipa vijana wengi zaidi na kwa haraka zaidi Tanzania na nje ya nchi.
Manara aondolewe kabisa katika mpira wa nchi hii kwakufungiwa maisha, Ni kijana anayekosa sifa za kuwepo mpirani, Michezo iko mingi Tanzania aende kwingine ambako hakuna kanuni na sheria.
TFF simamieni mpira, simamieni kanuni.
Credit,
YN