Haji Manara Awachokoza tena TFF

Haji Manara Awachokoza tena TFF

Hili hata sijui niliweke vipi, jana au juzi nimemuona Shaffih Dauda akizungumzia utambulisho wa Diamond kwenye kudhamini mashindano yake ya Ndondo Cup.

Ikumbukwe Shaffih naye aliadhibiwa na Kamati ya Maadili asijihusishe na shughuli za michezo.
Ndondo Sikh hizi zinasimamiwa na tff?????
 
Shirikisho la Mpira Tanzania linatakiwa kuchukua hatua kali zaidi kwa @hajismanara kwasababu ameendelea kukiuka adhabu aliyopewa ya kufungiwa miaka miwili. Hii ni dhihaka kubwa kwa chombo chetu cha kusimamia mpira nchini na kwa Wizara ya Michezo kwa ujumla wake, lakini inavuka na kudhalilisha utawala wa kisheria nchini.

Manara amefanya tukio la uvunjifu siku ya Wananchi wiki mbili zilizopita, Wakati TFF ikiwa tayari imemfikisha upya kwenye kamati ya nidhamu kwa mara nyingine, jana pia amekiuka na kuendelea kuwa msemaji wa Yanga akiuzungumzia mkataba wa Yanga na Jackson Group.

Narudia tena kushauri mamlaka za soka nchini @tanfootball kwamba Mpira huu wasipodhibitiwa watu wahuni kama huyu Manara basi tusahau mageuzi na uwekezaji ulioanza kujitokeza sasa. Mpira ni biashara kubwa sasa, Ni sekta inayoajiri na kulipa vijana wengi zaidi na kwa haraka zaidi Tanzania na nje ya nchi.

Manara aondolewe kabisa katika mpira wa nchi hii kwakufungiwa maisha, Ni kijana anayekosa sifa za kuwepo mpirani, Michezo iko mingi Tanzania aende kwingine ambako hakuna kanuni na sheria.

TFF simamieni mpira, simamieni kanuni.

Credit,
YN
Tiketi za ndege analipiwa huyo
 
Ndondo Sikh hizi zinasimamiwa na tff?????
Mashindano yoyote ya Mpira wa Miguu Tanzania yako chini ya TFF. Hata UMISSETA na UMITASHUMTA pia.
 
Kwa hiyo TFF wanamiliki haki ya Manara kuongea? Acheni kutukuza binadamu wenzenu.
 
Dauda ameona hakuna kitu Haji amefanywa na ameendelea kuusemea mpira bila kujali! Pamoja na mapungufu ya viongozi wa TFF ( Kawaida kwa binadamu wote) lakini upo uwezekano wanasiasa wa juu wanaingilia haya mambo! Kiburi cha Haji si GSM tu, kuna sababu na hili sakata litakuja kuibua mengi.

Sasa TFF wamedharaulika na mpaka sasa hawajafanya lolote. Wengi tunasubiri kuona hili sakata litafia wapi. Tutawakumbusha hadi tuone mwisho.
Adhabu yeyote ya kumzuia mtu kufanya kazi wakati wewe sio ulio muajiri lazima itakiukwa....sasa hivi namtazama Tundaman live etc ana perform... nakumbuka adhabu yake ya miezi mitatu Kwa kuingia na jeneza Simba day....ukweli adhabu hizi ni za kipumbavu...wote Manara,Dauda na Tundaman nilijua watazi kiuka...adhabu stahiki ni faini Tu Kwa waajiri wao
 
Ngoja aendelee tu kuwanyoosha ili wakati mwingine mjifunze kuacha kutoa adhabu za mihemko, na za kumfurahisha Msomali wenu.

Kama mnaweza basi nendeni mkaufunge ule mdomo wake kwa gundi ya super glue. Kinyume na hapo, atawavuruga mpaka mjute kumfahamu
 
Kama wamemfungia hiyo miaka 2 na bado anaongea, hata wakimfungia maisha ataongea, je utashauri tff wafanye nn kingine?
 
Ngoja aendelee tu kuwanyoosha ili wakati mwingine mjifunze kuacha kutoa adhabu za mihemko, na za kumfurahisha Msomali wenu.

Kama mnaweza basi nendeni mkaufunge ule mdomo wake kwa gundi ya super glue. Kinyume na hapo, atawavuruga mpaka mjute kumfahamu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nilitaka kuona umeandika nn?? Bado maumivu yako pale pale. Poleeeeeeh.
 
Hili hata sijui niliweke vipi, jana au juzi nimemuona Shaffih Dauda akizungumzia utambulisho wa Diamond kwenye kudhamini mashindano yake ya Ndondo Cup.

Ikumbukwe Shaffih naye aliadhibiwa na Kamati ya Maadili asijihusishe na shughuli za michezo.
Ndondo cup haiko chini ya TFF
 
Shida nikwamba umemwambia MTU asijihusishe na mpira akiwa wapi unaweza ukalifungia gazeti kuchapwa kilasiku ukasahau kulifungia online
 
Back
Top Bottom