Haji Manara baadae atasema aliombwa na Waziri aombe msamaha?!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Kumsaidia Haji ni kumuambia UKWELI pale anapokosea tu, wanaomzunguka HAWAMPENDI kwakuwa hawawezi kumuambia ukweli mchungu ambao ni tiba kwa tabia zake.

Tunaoonekana hatumpendi ndio kiuhalisia TUNAMPENDA ila kwakuwa anazungukwa na WAHUNI ambao wanamuelekeza shimoni na yeye kajivika upofu ndiyo maana ndani ya siku 3 anaomba msamaha mara 2.

Ukimuambia ukweli wewe ni adui na WAPAMBE watakuandama sana kwa maneno, lakini leo masikini ya Mungu anahangaika pekeyake na misamaha isiyoisha.

Haji HACHUKIWI ingawa yeye mwenyewe hajipendi na wanaomzunguka hawajahi kumpenda.

Wanashangilia anguko lake kwa kumvika Ufalme hewa na yeye anajiona mfalme kweli kumbe anajiingiza kwenye lindi la matatizo.

Tunaomuambia ukweli ni vile tunaochukizwa na tabia zake ambazo sio za kiuanamichezo anazozionyesha kila uchao kwa watu tofauti tofauti.

Nakukumbusha tu kumuomba msamaha Waziri na ukakiri kukosea hadharani ni vyema sana. Lakini pia unadhihirisha kwamba ulipomkosea Waziri ulifanya kosa la KIMAADILI.

Kosa la kimaadili linaweza kuishi hata miaka 10 likafufuliwa na ukashitakiwa nalo na ukaadhibiwa. Wanaokuchukia hawawezi kukuambia hivi. Sisi tunaokupenda pekee ndo tunakupa ukumbusho huu jadidi.

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)

My Take
Haji alipewa adhabu ya kumtukana Rais Karia. Hili la kumsema uongo Waziri ni kosa lingine kabisa. Mamlaka zichukue hatua kali ili iwe fundisho kwa Waropokaji na Machawa wote mfano wa Manara. Mbali na adhabu pia apimwe akili
 
Huyu JEMEDARI ni kweli jemedari,yule mzungu pori ktk watu wanaompatia bila kurukuta ni huyu mwamba
 
Akihojiwa na Kitenge kwenye kituo cha EFM, alikiri kabisa kuwa aliingia kichwa kichwa kwa Kauli yake kuwa Waziri alitoa maelekezo kwa TFF.

Na akasema ile press ya wazee wa Yanga na viongozi wa matawi ilisababisha yeye kumkosoa Waziri.

Je..? Hivi wale wapuuzi walikuwa wakisema Haji anaonewa tu kupewa adhabu, sijui wana lipi kwa sasa..!
 
Haji manara Anaharibu mpira wa Tanzania.

Ni adui MKUBWA WA maendeleo ya mpira.
1. Matusi.
2.Maneno Mengiiiii.
3.Ugomvi.
4. Ushirikina.
5.Ujuaji.
6.
 
Watetezi wake siwaoni humu baada ya jamaa yao kutema ndoano 😹😹
 
Adhabu itaisha ataendelea na majukumu yake kama kawaida. By the way si bado analipwa na Jiesiemu?
 
Mwenzenu yupo anaingiza pesa kwa mnavyo mjadili... Nyie mnaishia kujifanya mnamjua sana... He's there kwasabab ya hicho msichokipenda ila yeye kinampa ugali watoto wanaenda shule... WaTz ni wajinga sana mngekua hamtoi airtime mnadhan msiowapenda wangesikika..? All in all muacheni albino wa watu ainjoi maisha aliyojichagulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…