Haji Manara hafai kuwa Msemaji wa Simba SC

Haji Manara hafai kuwa Msemaji wa Simba SC

king joniva

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2018
Posts
262
Reaction score
296
#NIONAVYO MIMI: HAJI MANARA HAFAI KUWA MSEMAJI WA SIMBA SC.

kwanza kabisa napenda kukiri wazi kuwa Mimi ni shabiki wa chama la wana SIMBA SC, pili nina muheshimu kaka yangu Haji Manara na nina heshim mchango wake kwa klabu yetu.

Wakati wa kuanzishwa kwa klabu hii 1936, timu hii imepitia vipindi kadha wa kadha ikijumuisha majina mbalimbali kama vile queens na Sunderland SC. Baadae wazee wetu wakaja na jina jipya SIMBA SC. Hawakuchagua jina hili kwa bahati mbaya wala si kwa kukurupuka, walijua jina litasadifu sifa nzuri za mnyama simba yule wa mbugani, sifa hizo ni pamoja na:-

1. Maisha ya umoja baina ya jamii ya wanyama hawa
2. Matumizi ya akili katika uwindaji wao
3. Ujasiri wakupambana mpaka tone la mwisho katika maisha yao

Ipo wazi miongoni mwetu kuwa miongoni mwa mambo yanayo vutia mbugani ni lile tukio la simba kuwinda, hakurupuki ovyo pia hutumia akili na ujanja mwingi kumtia nguvuni mnyama yeyote aliyemtia kwenye radar zake. Simba anapo winda swala si sawa napale anapo muwinda nyati. Atatumia utulivu mkubwa kwa swala ila kwa nyati atatumia ujasiri na nidhamu. Hii ndio sifa ya mnyama SIMBA wa mbungani na sifa hizi ndio hujenga falsafa za timu yetu SIMBA SC.

HATA SIKU MOJA SIMBA HAWINDI WINDO LAKE HUKU AKIPIGA KELELE" huwinda kwa utulivu na nidhamu kubwa bila kujali ukubwa au udogo wa windo lake. Na hii ndio sifa adhimu ya SIMBA SC tangu kale.

Brother HAJI MANARA ama hajui au anajua madhara ya aina aliyo chagua kuisemea SIMBA SC. Hasa pale anapo isemea timu katika mashindano ya ndani. Kwa wachunguzi wanatambua kwamba MANARA anapoisemea SIMBA SC katika mashindano yakimataifa ni tofauti na vile anapoisemea katika mashindano ya ndani.

Katika mashindano yakimataifa Haji Manara hutoa heshima kwa wapinzani huku akihamasisha wachezaji wetu kupambana kupata matokeo mazuri wakitambua wapinzani ni bora zaidi yao. Ila hali ni tofauti pale anapoisemea SIMBA SC katika ligi na mashindano ya ndani. Hukebei wapinzani na kujigamba kuwa SIMBA SC ni bora zaidi ya wengine, husifu na kuwapamba wachezaji wa timu yetu na kuwadharau wale wa timu pinzani. Mfano kuwaita wachezaji wa timu ya Young Africans "takataka" juzi.

Usemaji wa manara hasa huu anaotumia kwa mashindano ya ndani huwafaidisha wapinzani na kugeuka sumu kwa timu yetu, hii ni kwasababu mpira wa sasa hutegemea ujenzi wa saikolojia zaidi huku uwanjani ni matokeo tu yakile kilicho fanywa ndani ya saikolojia ya timu husika. Wapinzani hutumia kauli za kejeri na kebehi za MANARA kupandisha morali za timu zao huku upande wa SIMBA SC hujaza overconfidence kwa timu yetu.

Sote tunatambua kuwa ni vigumu kuishinda timu ambayo ipo kwenye morali kubwa hata kama hawana ubora. Jeshi lenye ubora na overconfidence linapokutana na jeshi lenye morali hata kama halina siraha nzuri vita huwa ngumu upande wa jeshi lenye overconfidence tu.

Wapinzani hucheza jihadi dhidi yetu kama sehemu ya kulipa kisasi dhidi ya kauli za kebehi za msemaji wetu dhidi yao. Tunajua kwamba falsafa za uchezaji wa timu yetu ni kama zile za mnyama simba nilizo eleza hapo juu. Simba tunacheza mpira wa kuonekana na utulivu na sio vurugu, hivyo tunapokutana na timu zinazo cheza jihadi hujikuta katika wakati mgumu sana jumlisha overconfidence iliyojazwa kwa kauli za MANARA kwa wachezaji wetu ndio sumu inayotumaliza kabisa.

MANARA hana upeo wa kutosha kutumia usemaji wake kuwateka wapinzani wetu kisaikolojia kwa manufaa ya SIMBA SC. Hajui kuchagua aina ya lugha kulingana na aina ya mechi ambayo timu yetu inakumbana nayo ni kama simba kutumia mbinu za kuwinda swala wakati wa kumuwinda nyati. SIMBA SC tupo katika level za kimataifa hivyo tunatakiwa kuziishi falsafa za timu yetu na zile za kawaida za kimpira ikiwemo ujenzi wa saikolojia rafiki kwa timu.

Mfano:
Kaizer chief ni moja ya timu bora zaidi ya SIMBA SC, kwa kutambua umuhimu wa saikolojia rafiki kwa timu yao waliamua kuichota SIMBA SC kisaikolojia ili tu kupata matokeo wanayo yataka wao. Kwanza walijenga urafiki wa muda na timu yetu kisaikojoia hasa pale walipo tumia mitandao ya kijamii kuwa karimu SIMBA SC pili walitengeza zengwe kabla mechi kuonesha hawapo vizuri kiufundi kwa matokeo mabaya waliyopata kwenye ligi hasa pale mashabiki wao walipo andamana. SIMBA SC wakajikuta wakidharau kaizer chief na huku kaizer wakitumia mwanya huo kupandisha morali kwa timu yao. Baada ya mechi wote tunajua nini kilitokea ". Hii ni kuonesha jinsi gani saikolojia ni muhimu kwa timu ya mpira wa miguu ambao sisi SIMBA SC hatujawekeza ipasavyo.

Kabla ya mechi ya watani wa jadi iliyochezwa 3 july 2021 na SIMBA SC kufungwa 0-1. Manara alikaririwa akikebehi na kubeza wapinzani kiasi cha kukera sana. Ni kweri wapinzani hawakuwa bora kama SIMBA SC. Kauli zake ziligeuzwa mbolea ya samadi na wapinzani wetu kustawisha morali ya upambanaji kwa timu yao huku kwetu sisi SIMBA SC ikigeuka sumu ya overconfidence kwa timu. Wapinzani timu yao ilicheza kwa bidii kujibu kebehi na dharau dhidi yao, timu yao ilicheza ikitambua wanadeni kwa mashabiki zao huku upande wa SIMBA SC kutokana na kujazwa sifa lukuki na MANARA wakajikuta wao ni bora na hawana deni kwa mashabiki wao kwani wameshafanya kila kitu kwa mujibu wa sifa wanalizopewa na MANARA.

Matokeo ya jambo hili linathibitishwa kwanza na uchezaji wa timu hizi hasa kipindi cha kwanza na ukweri wapinzani walipata matokeo chanya. Pili ni ishara zilizooneshwa na wachezaji wa upinzani baada ya mechi kuisha kwa kuamua kuokota takataka uwanjani. Hii ili maanisha nguvu ya uchezaji wao katika mechi hiyo ilichangiwa na kauli ya msemaji wetu kuwaita wao 'takataka".
Ili wezekana kabisa MANARA kuwa jaza sifa wapinzani na kuonesha uungwana kwa manufaa ya timu yetu kama vile Kaiser chief walivyo fanya kwetu mechi ya kwanza robo fainali klabu bingwa. Hii ingelisaidia angalau kuruhusu timu pinzani icheze mpira wa kawaida na sio jihadi na hivyo kuweka unafuu kwa SIMBA SC kupata matokeo rafiki kabisa.

Turufu alikuwa nayo mikononi mwake hasa ile kauli ya vyombo vingi vya habari kuwa SIMBA SC katika mechi tatu mfululizo hajapata matokeo dhidi ya mpinzani wake. Angeamua kuikubari na kuitumia makusudi kujenga hali ya upambanaji kwa wachezaji wetu huku wapinzani wangejiona nao ni bora hivyo wasingelikuwa na haja yakukamia kwani wao wanarekodi nzuri dhidi ya SIMBA SC.

Mimi nadhani usemaji wa MANARA unafaa kama utatumika kwa timu zenye tabia za kucheza mpira aina ya Prison Sc nasio aina ya uchezaji wetu SIMBA SC. Kwasababu timu aina hii hutumia nguvu na sio akili hivyo uchezaji wao hauathiliwi na uchezaji wa wapinzani wao. Ila uchezaji wetu SIMBA SC unaweza kuathirika hasa pale mpinzani anapochagua kucheza jihad.

Usemaji wa MANARA unahujumu falsafa za timu yetu na hauna faida kwa timu kwa sasa hasa huu usemaji anaotumia kwa ligi za ndani au pale simba anapocheza na timu dhaifu. Ubaya ni kwamba kaka HAJI MANARA ni MTU asiyependa kukosolewa. Hapendi kabisa timu yetu kukosolewa hata kumkosoa yeye mwenyewe mfano ni reaction yake kwa mwandishi aliye jaribu kumrekebisha wakati wa press conference kabla ya mechi hiyo na mtani.

Manara anajenga chuki kwa baadhi ya timu dhidi yetu kwa kauli zake hivyo kuchangia kukamiwa kwa mechi zetu. Pia uhasama na waandishi wa habari ambao unachangia SIMBA SC kutazamwa vibaya. Mfano, kwasasa habari hasi za SIMBA SC huandikwana kushabikiwa sana kuliko zile chanya hii ni kwavile tu waandishi wengi wamewahi au wameumizwa na aina ya kauli za msemaji wetu dhidi yao ama taasisi zao. Mahusiano ya MANARA na waandishi wa habari yameathiliwa kwa kauli zake dhidi ya waandishi na inachangia SIMBA SC kukosolewa zaidi na vyombo vingi vya habari. Hii inatukosesha ustawi bora wa timu hasa katika kuongeza washabiki wapya kwani tunasemwa vibaya zaidi ya kusemwa vyema.

"SIMBA SC ikifanya vibaya ni habari kubwa sana kwenye radio, magazetini, mitandaoni na vyombo vingine vya habari hii ni kutokana na kauli za majigambo, kebehi na kiburi za MANARA".

Kama SIMBA SC tunafanya mabadiriko basi idara yetu ya habari ni muhimu kufanyiwa mabadiriko pia. Content za kauli zetu kama taasisi zinatakiwa zifanane na falsafa zetu pia. Kama timu zetu uwanjani zinacheza (pira biriani) mpira mzuri basi inapaswa kuwa hivyo pia kwa idara zote ndani ya taasisi hii kubwa nchini.

"HAJI MANARA AKUBARI AKATAE, KAULI ZAKE HAZIENDANI NA FALSAFA ZA SIMBA SC".

Anatakiwa kubadirika ama SIMBA SC tumbadirishe kwa manufaa ya timu yetu.

#KUTOKA kwa mdau wa SIMBA SC

#KWENDA kwa wadau wa mpira wa miguu Tanzania, SIMBA SC, Mo dewji, Barbara Gonzales, Vyombo vya habari Tanzania, wanachama na mashabiki wa mpira Tanzania

ASANTE SANA! #Nguvumoja
 
Huna hana sifa hata ya kuwa msemaji wa familia yake! Bora hilo jukumu akakbidhiwa mke wake au watoto wake!

Ila kwa bahati mbaya ndiyo hivyo tena, ana mbumbumbu wake eti wanamuunga mkono.
 
Yote haya sababu simba imefungwa. Kama wachezaji wanasubiri mpaka Manara ahamasishe ndio wapambane basi hao wachezaji hawafai. Halafu kama upambanaji unaendana na kuhamasishwa basi Manara ndie anafaa sana sababu simba ndio yenye matokeo bora hapa Tz kuliko klabu zote na ni bingwa mtarajiwa. Kwa hiyo humtaki anaeleta upambanaji mpaka klabu inakuwa bingwa kisa tu imefungwa kwenye derby?
 
Umeandika andiko refu na nimejaribu kulisoma ila sijalimaliza lote ila itoshe kusema HEADLINE yako imemaliza kila kitu.

Manara anaishi katika kuamini kuwa usemaji ni kejeli, kelele na ujinga mwingine kama huo kumbe hajui lolote. Hizi propaganda za kutusi na kukebehi watu zimepitwa na wakati. Msemaji gani kifua chake kidogo hawezi kupambana na mambo makubwa. Mfano majuzi suala la Prisca Kishamba liliendelea kumvua nguo kijana huyu, anaenda kuongelea mambo personal kwenye mkutano aliouitisha kwa jina la klabu! Je watu wakiamini kuwa kile alichofanya kwa Prisca Kishamba ni Simba Sc imefanya ataweka taswira gani kwa timu?

Simba ifumue kitengo cha habari na kukisuka upya, watafute watu wenye kujua IN & OUT kuhusu Public Relation ili kutengeneza picha nzuri kwa klabu na jamii. Wenzetu Yanga wamejitahidi kwenye kitengo cha habari na majuzi hapa wametoa ripoti namna app yao ilivyoingiza pesa. Siku moja nilipata nafasi ya kukaa na Bumbuli na moja ya kitu alichokuwa anasifia ni pamoja na App ya Yanga ambayo yeye anasema inaingiza zaidi ya Milioni 1 kwa siku. Haya ndiyo mambo ambayo tunataka kuona siyo makelele na kupayuka hovyo pasipo mpangilio.

Simba tutafute njia nzuri ya kusemea klabu siyo kwa aina hii ya usemaji iliyopo kwa sasa.
 
Msimamo wako ungeendelea kuwa ni huu endapo Simba angeshinda mechi dhidi ya Yanga ?
 
Yote haya sababu simba imefungwa. Kama wachezaji wanasubiri mpaka Manara ahamasishe ndio wapambane basi hao wachezaji hawafai. Halafu kama upambanaji unaendana na kuhamasishwa basi Manara ndie anafaa sana sababu simba ndio yenye matokeo bora hapa Tz kuliko klabu zote na ni bingwa mtarajiwa. Kwa hiyo humtaki anaeleta upambanaji mpaka klabu inakuwa bingwa kisa tu imefungwa kwenye derby?
Tatizo una ushabikiNoga, huyu mdau aliyetoa article naamini ni mwanachama/Shabiki was Simba kabisa ila amebase on Facts.. Soma vizuri article na ulielewe si kubwabwaja tu.. Always kila action inayofanyika katika maisha inachagizwa na result ya kitu Fulani.. Sasa unashangaa nn mdau kuzungumzia hili hali ya kuwa negative impacts za usemaji/usenge wa Manara tumeziona..!!
 
Usemaji wa Manara unaakisi jamii kubwa ya mashabiki wa soka Tanzania ambao huongozwa na jazba na hisia kuliko uhalisia wakati wakielezea timu zao. Hivyo aendelee tu kwani anakonga nyoyo za washabiki wa timu yake wanapowakoga wapinzani wao.
 
Wamtafutie njia nyingine ya kumfanya apate riziki kama lengo ni kumsaidia kutokana na his physical challenges.

Kuna njia nyingi za kuweza kumsaidia kama wana nia ya kufanya hivyo kuliko kumuacha kwenye hiyo nafasi ambayo haina maana yoyote kwa klabu na sasa anaitumia negatively.
 
Yote haya sababu simba imefungwa. Kama wachezaji wanasubiri mpaka Manara ahamasishe ndio wapambane basi hao wachezaji hawafai. Halafu kama upambanaji unaendana na kuhamasishwa basi Manara ndie anafaa sana sababu simba ndio yenye matokeo bora hapa Tz kuliko klabu zote na ni bingwa mtarajiwa. Kwa hiyo humtaki anaeleta upambanaji mpaka klabu inakuwa bingwa kisa tu imefungwa kwenye derby?
Sijakataa kwamba Manara huwa analeta upambanaji kwa wachezaji, ila hilo hutokea hasa kwenye mashindano ya CCL au tunapo cheza na timu kubwa zaidi yetu but inapokuja tuna cheza na timu za kiwango kidogo zaidi yetu au ligi ya ndani manara hutoa kebehi na kejeli zinazo sababisha wapinzani wacheze jihad ili tu kum-prove wrong manara
 
Wamtafutie njia nyingine ya kumfanya apate riziki kama lengo ni kumsaidia kutokana na his physical challenges.

Kuna njia nyingi za kuweza kumsaidia kama wana nia ya kufanya hivyo kuliko kumuacha kwenye hiyo nafasi ambayo haina maana yoyote kwa klabu na sasa anaitumia negatively.
Nimeona Leo pia katoa tamko la kuwa tuhum wachezaji et walicheza chini ya kiwango kasahau kuwa yeye ndiye aliye wapa overconfidence, nadhani anataka kuivuruga timu yetu kwa sasa!!
 
Umeandika andiko refu na nimejaribu kulisoma ila sijalimaliza lote ila itoshe kusema HEADLINE yako imemaliza kila kitu.

Manara anaishi katika kuamini kuwa usemaji ni kejeli, kelele na ujinga mwingine kama huo kumbe hajui lolote. Hizi propaganda za kutusi na kukebehi watu zimepitwa na wakati. Msemaji gani kifua chake kidogo hawezi kupambana na mambo makubwa. Mfano majuzi suala la Prisca Kishamba liliendelea kumvua nguo kijana huyu, anaenda kuongelea mambo personal kwenye mkutano aliouitisha kwa jina la klabu! Je watu wakiamini kuwa kile alichofanya kwa Prisca Kishamba ni Simba Sc imefanya ataweka taswira gani kwa timu?

Simba ifumue kitengo cha habari na kukisuka upya, watafute watu wenye kujua IN & OUT kuhusu Public Relation ili kutengeneza picha nzuri kwa klabu na jamii. Wenzetu Yanga wamejitahidi kwenye kitengo cha habari na majuzi hapa wametoa ripoti namna app yao ilivyoingiza pesa. Siku moja nilipata nafasi ya kukaa na Bumbuli na moja ya kitu alichokuwa anasifia ni pamoja na App ya Yanga ambayo yeye anasema inaingiza zaidi ya Milioni 1 kwa siku. Haya ndiyo mambo ambayo tunataka kuona siyo makelele na kupayuka hovyo pasipo mpangilio.

Simba tutafute njia nzuri ya kusemea klabu siyo kwa aina hii ya usemaji iliyopo kwa sasa.
Fact, usemaji huu hauendani na level ya SIMBA SC ya sasa
 
Simba wanaogopa wakimfukuza wataambiwa wanawanyanyapaa watu wa aina nyingine wanaamua kuvumilia
 
Usemaji wa Manara unaakisi jamii kubwa ya mashabiki wa soka Tanzania ambao huongozwa na jazba na hisia kuliko uhalisia wakati wakielezea timu zao. Hivyo aendelee tu kwani anakonga nyoyo za washabiki wa timu yake wanapowakoga wapinzani wao.
Na bila hivyo kwa bongo, mambo hayaendi
 
Yaani Yanga kufunga goli moja basi wanajiona kila kitu cha simba ni dhaifu dhidi yao, Lakin ukweli ni kuwa Yanga bado ni mbovu sana japo kushinda mmeshinda ila kimpira haku na kitu kabisa ukilinganisha na simba shabikieni goli lenu na furahieni ushindi wenu ila mengine yaachane bhana
 
Back
Top Bottom