scatter
JF-Expert Member
- Feb 15, 2013
- 1,667
- 926
Toka majuzi nimekua nafuatalia mitandao ya kijamii hasa kwa habari za michezo na burudan. Tukio moja lililovuta hisia zangu ni lile la majibizano ya kimaneno baina ya ndugu Haji Manara na Jerry Muro hasa katika kipengele cha kufundisha elimu ya dini.
Kitendo cha Haji kujibu kudhalilishwa uislam ni hoja zisizo na maana na zinafaa kupuuzwa kwa sababu zifuatazo:
1. Walimu wa madrassa wote nchini wana hofu na Mungu muda wote na huwezi kukuta wanajishughulisha na mambo ya kidunia kwa muda mwingi.
2. Walimu wa madrassa ni kieleleza cha tabia za watoto kwani huwafundisha dini kuanzia wakiwa wadogo mpaka wanapokua hivyo kipingele cha maadili kinakuwa ni jukumu lao.
3. Fani ya ualimu wa madrasa ni lazima ukae chini usomee tena ukunje goti na uwe mnyeyekevu kwa Mashekh ili upate elimu yenye manufaa kwa jamii kwani unaweza kusoma elimu ya dini na ukashindwa kuitumia elimu yako kwa jamii na jamii ikakuchukulia kama mtu wa ajabu.hivyo ni elimu yenye weledi na ni ya KUJIVUNIA.
Kwa huyu ndugu manara kujitapa kwenye vyombo vya habari kua walimu wa madrassa wamedhalilishwa ni unafiki na ni uchochezi kwa sababu nilizoziweka hapo juu. Kama alikuwa ni mwalimu wa madrassa kwanini asijivunie badala yake anahisi ametukanwa?
Walimu wa madrassa wengi hawana mambo mengi ni hayo tu.