Haji Manara katudhalilisha Waislamu

Haji Manara katudhalilisha Waislamu

scatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,667
Reaction score
926
Toka majuzi nimekua nafuatalia mitandao ya kijamii hasa kwa habari za michezo na burudan. Tukio moja lililovuta hisia zangu ni lile la majibizano ya kimaneno baina ya ndugu Haji Manara na Jerry Muro hasa katika kipengele cha kufundisha elimu ya dini.

Kitendo cha Haji kujibu kudhalilishwa uislam ni hoja zisizo na maana na zinafaa kupuuzwa kwa sababu zifuatazo:

1. Walimu wa madrassa wote nchini wana hofu na Mungu muda wote na huwezi kukuta wanajishughulisha na mambo ya kidunia kwa muda mwingi.

2. Walimu wa madrassa ni kieleleza cha tabia za watoto kwani huwafundisha dini kuanzia wakiwa wadogo mpaka wanapokua hivyo kipingele cha maadili kinakuwa ni jukumu lao.

3. Fani ya ualimu wa madrasa ni lazima ukae chini usomee tena ukunje goti na uwe mnyeyekevu kwa Mashekh ili upate elimu yenye manufaa kwa jamii kwani unaweza kusoma elimu ya dini na ukashindwa kuitumia elimu yako kwa jamii na jamii ikakuchukulia kama mtu wa ajabu.hivyo ni elimu yenye weledi na ni ya KUJIVUNIA.

Kwa huyu ndugu manara kujitapa kwenye vyombo vya habari kua walimu wa madrassa wamedhalilishwa ni unafiki na ni uchochezi kwa sababu nilizoziweka hapo juu. Kama alikuwa ni mwalimu wa madrassa kwanini asijivunie badala yake anahisi ametukanwa?

Walimu wa madrassa wengi hawana mambo mengi ni hayo tu.
 
Haji, mtu wa ajabu sana! yaanai utani wa kwanye mpira, kaukimbizia kwenye dini, ili aonekane mwema sana, au Jerry aonekane mbaya. Kwanza afananii kuwa hata mwalimu wa madrasa.
 
Haji, mtu wa ajabu sana! yaanai utani wa kwanye mpira, kaukimbizia kwenye dini, ili aonekane mwema sana, au Jerry aonekane mbaya. Kwanza afananii kuwa hata mwalimu wa madrasa, kila siku na kina U....
Hata mimi namshangaa sana yule ni muhuni tu hata dini haijui
 
Sasa kosa la Manara hapo ni lipi?

Je, kama alisema kua dini imedhalirishwa kwa sababu yeye hafai kua mwalimu. Je, huoni kua ni kudhalirisha dini kusema mtu flani awe mwalimu wa madrasa wakati unajua kua hana vigezo hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kosa la Manara hapo ni lipi?

Je, kama alisema kua dini imedhalirishwa kwa sababu yeye hafai kua mwalimu. Je, huoni kua ni kudhalirisha dini kusema mtu flani awe mwalimu wa madrasa wakati unajua kua hana vigezo hivyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani ualimu wa madrass ni dhambi au ni kitu kibaya duniani?
 
Haji, mtu wa ajabu sana! yaanai utani wa kwanye mpira, kaukimbizia kwenye dini, ili aonekane mwema sana, au Jerry aonekane mbaya. Kwanza afananii kuwa hata mwalimu wa madrasa.
Nimeshawahi Mara kadhaa kusema humu kuwa Simba haikustahili kabisa kuwa na msemaji Kama Haji Manara. Kwanza kwa mujibu wa taratibu za tff siamini Kama cheo Cha msemaji kipo, kipo cheo cha ofisa habari. Haji ni hatari kwa soka la nchi. Kama taarifa zake mbalimbali zitatafsiriwa na kupelekwa FIFA ni wazi TFF itakuwa kikaangooni kwa kumlea mtu Kama huyo.
 
Mara nyingi nasema ubungo wa Hajj Manara una kasoro unawezaje kuingiza dini kwenye mazungumzo ambayo kila mtu alisikia sasa hao waislamu aliowahamisha alifikiri wana akili kama yake haya sasa wametulia aibu kwake halafu anataka kuihusisha hata serikali eti Rais atasema kitu na pia Jafo naye atasema kitu.

Huyu mtu ni hatari sana anataka kuwaingiza wote kwenye kitu cha kijinga kabisa yeye katukana mara ngapi yanga kamtukana Zahera kamtukana Bumbuli kawatukana wachezaji akina Morrison wakanyamaza kimya kaja kiboko yake anachachawa sasa ushauri kwa mtoe mtu huyu atakuletea matatizi makubwa mtu na akili zake anahamisha udini utafikiri yeye ndio atapona anasema yupi tayari kufa huku anatembea na walinzi.
 
Acheni wivu, Manara kaajiriwa Simba Kwa vigezo vyote na anamkataba wa kazi. Someni na nyinyi muajiriwe na sio kutaka Manara afukuzwe kazi bila sababu ya Msingi. Acheni wivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio dhambi, sasa amefhalirisha vipi uislamu ka anavyodai mtoa mada?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kwamba yeye anadai mtu ukiambiwa ukafundishe madrassa ni kitu kibaya sana na ubaya wake umedhalilisha uislamu. Sasa uislamu gani unadhalilishwa kwa kauli hizo. Uislam ni dini ya amani na upendo. Ucha mungu ni matendo yako yaliyo mema. Na kingine tujue kutofautisha kuwa muislam sio ndio umekua mcha mungu
 
Wewe scatter nafikiri itakua mshabiki wa kwasukwasu una chuki zako binafsi na Haji, umeweka shutuma hapa bila video, kwanini nisiamini hayo maneno umemlisha Haji? Weka video au audio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom