Kinachoendelea uwanja wa Benjamin Mkapa ni AIBU KWA Mamlaka za soka (TFF).
Tafsiri ya kwanza ni kwamba TFF haina NGUVU zozote mbele ya Yanga SC ambaye ni mwanachama wake.
Yes, unamfungia kiongozi wao, unawapa hukumu na barua ya maelekezo, halafu HAWAJALI wanaendelea na maisha kama kawaida.Manake TFF leo imevuliwa NGUO hadharani mchana kweupeee.
Ile dhana ya kwamba Yanga ni timu ya SERIKALI ambayo Haji aliwahi kuisema akiwa Simba leo imedhihiri kwa hiki kinachoendelea.
Wilson Oruma aliandika kwenye ukurasa wake kwamba ni HATARI SANA KUAMINI VIONGOZI VIJANA, kwa hiki kinachoendelea leo hakuna shaka alikuwa sahihi kabisa. Sidhani kama Mwenyekiti bado angekuwa Mshindo Msola angekubali UPUUZI huu utokee.
Niliwahi kusema mahala kwamba kesi ya Haji ni mtihani na kipimo cha mwanzo cha Uongozi mpya ambacho wameanza kwa KUFELI. Yanga ni kubwa jamani hawa vijana hawana busara za kutosha kuiongoza, tuliposema hivi tulionekana hatuwapendi, leo imedhihiri mchana kweupe.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga ni mwajiriwa wa serikali na mteule wa Rais wa Zanzibar, hivi kweli HAJUI NAMNA YA KUHESHIMU MAMLAKA? Vijana mnatutia AIBU kwa kuendekeza ushikaji.
Viongozi wanaweza Sema kwamba walikuwa VVIP, lakini baada ha kuliona tukio wamechukua hatua gani? Wasingeweza kuteremka na kumuondoa wakaomba radhi?
Manake ni kwamba Yanga wako na Haji na HAWAKUBALIANA na lolote hata kwamba alikosea pale Arusha. Kama ni kweli Rais wa Yanga kwanini ALIUONGOPEA Umma kwenda na Haji kuomba msamaha kwa Karia?
Juzi nimesema wasiompenda Haji ni wengi kuliko tunaompenda, kama wangekuwa wanampenda WASINGEKUBALI afanye alichofanya leo. Manake kama TFF wako makini lazima atarejea Maadili na kibano kitakua KIKUBWA ZAIDI.
TFF wasipochukua hatua kwa hili wanapaswa KUWAJIBIKA kama ambavyo Viongozi wa Yanga waliomruhusu Haji wanapaswa kuwajibika au kuwajibishwa.
Kama wangekuwa na Kamati ya Utendaji yenye NGUVU na maadili, leo hii watu wangewajibika kwa UPUUZI huu.
NB: Kuna wahuni kwenye mpira, ila mpira sio mchezo wa Kihuni. Tuheshimu mamlaka.
BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless )