Haji Manara kwa Simba sasa muda wake umeisha

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
binafsi sina tatizo na haji manara sababu simfaham na hanifaham pia physically. nimemfaham kwa kumwona kwenye media. lakini kutokana na mabadiliko makubwa ya kimuundo yanayofanyika katika klabu ya simba nadhan sasa wanahitaji kupata mtu ambaye ni msomi na mwenye taaluma ya PR kwa kiasi kikubwa. manara alifaa kipindi kile team inaendeshwa kiswahili akiendana na mwenzie jerry muro. lakini kwa sasa si mtu wa kufaa tena maana uwezo wake ni mdogo. hayafaham mambo, hana uelewa wa mpira wa mikuu lakini najua ni mshabiki wa simba mzuri.

asifukuzwe kazi moja kwa moja. mimi napenda aendelee kupeleka watoto wake chooni bila shida. ila apewe jukumu la yeye kuwa kiongoz wa kikundi flan cha ushangiliaji na pia kushambuliana na watu kwenye mitandao kwa lugha za kihuni au matusi. huko anaweza akaendelea na kazi hiyo maana kuna ambao kiukweli wanaendana na uelewa wake haji manara.

apatikane PR msomi mwenye kuelewa matumizi mazuri ya lugha, mwenye kuelewa mpira pia. mwenye akili kubwa na ambaye hatakuwa akikimbizana na watoto wa darasa la saba na form failures kwenye media. awepo mtu ambaye atakapokuwa anahojiwa ajue anaulizwa swali gani na ajibu kitu gani. mtu mwenye uelewa mkubwa pia kuwasaida waaandishi wetu wengi ambao pia ni vilaza.

so nasisitiza asifukuzwe kazi ila abadilishiwe majukumu kwa sababu majukumu aliyo nayo ni makubwa na club sasa imekuwa ya kisasa inahitaji mtu msomi na mwelewa.mtu mwenye ufaham wa kutosha na si wa mipasho na maneno ya hovyo hovyo. huu ni ushauri wangu kwa klabu ya simba. nakaribisha mapovu maana najua naye akiambia kuhusu hii thread atakuja kumwaga mapovu yake hapa akidhani nataka mchafulia kitumbua chake kwa mchanga.si lengo langu hata kidogo.

tukutane tarehe 8/8 simba day
 
Majuzi baada ya uteuzi wa Wakuu wa wilaya kuna (Sauti) ambayo inaelekea kuwa ya Haji Manara ilikuwa ikisambaa kuhusu teuzi zile huku ikionesha kumponda aliyekuwa hasimu wake kwenye mambo ya usemaji wa Klabu (Muro).

Ukisikiliza ile sauti vizuri utajua kuna zingine hazipo sawa kichwani.
hili wengi hawawez lielewa sababu ya uelewa wao kuwa unafanana nayeye. kwa watu wenye elimu ndo wanaona jamaa pale hapamfai hasa klabu inapokuwa ya kisasa.
 
dah.. kwa kweli sijafanikiwa kuipata hiyo kama unayo please iweke hapa. unajua mimi ni msimba hasa lakini kama nikisikia kuna kitu anakuja kuzungumza haji manara huwa nachange station/channel maana jamaa naona kama kiakili hayupo sawa. hii si aina ya wasemaji tunaowataka simba kwa sasa. tunataka wataalamu wa mpira na jamaa ukimwambie azungumzie hata kitaalamu mpira hawezi. kuzungumza ki taaluma hawezi. ni mtu wa kuzungumza vijiweni au sehemu ambazo si rasmi.sasa akili zake zilikuwa zinaendana na muro .. wote wawili mi sikuwa nikiwakubali.
 
Wekeni vigezo vya msemaji wa club!
NB: naamini wanaomsema hafai siyo wanaYanga
 
MLETA HOJA TUPO PAMOJA. SIMBA INAENDA KIMATAIFA SASA MPAKA NILISIKIA TETESI KUWA WANAMPANGO WA KUMLETA MTAALAMU WA KUCHAMBUA MECHI "MATCH ANALYZER".

KWA MTIZAMO WANGU NA HILI NILIWAHI KULIZUNGUMZA HAPA JAMVINI NIKAPINGWA SANA KUWA SIMBA HII YA KIMATAIFA HAIHITAJI MTU WA MIPASHO BALI INAHITAJI MTAALAM WA PR HASA. KWA SABABU TIMU ITAKUWA INATANGAZA BIASHARA ZA MAKAMPUNI MBALI MBALI VIPI KWA WALE WAPINZANIA UNAOWATUKANA AU KUWAKASHIFU WATAVUTIKAJE KUNUNUA BIDHAA ZINAZOTANGAZWA KWENYE JEZI? KWANZA WATAJENGA CHUKI NA TIMU HUSIKA THEN WANAJENGA CHUKI NA BIDHAA ZINAZOTANGAZWA NA HIYO TIMU. KWA KUWA MO NI MFANYABIASHARA NAJUA ANAFAHAMU VIZURI MADHARA NA FAIDA ZA PR KWENYE MARKETING NI MATUMAINI YANGU KUWA AIDHA ATAMFUNGA GAVANA MANARA AACHE USWAHILI AU ATATAFUTA MTAALAM ALIYEBOBEA KWENYE HII FANI KWANI MPIRA NI BIASHARA NA KWENYE BIASHARA UKIKOSEA KIDOGO TU BIDHAA ZAKO UTANUNUA MWENYEWE. ENZI ZA KUBISHANA NA JERRY MURO NA KULETA MIPASHO ZIMEPITWA NA WAKATI SASA KUNAHITAJIKA WELEDI WA HALI YA JUU KUIBRAND SIMBA KIMATAIFA.
 
KWA KIPINDI KAMA HIKI NILITEGEMEA MANARA KWA KUSHAURIANA NA UONGOZI ATANGAZE "BIKO" KWA WATU WATAKAOFANIKISHA KUKAMATWA KWA WATU WANAUZA AU KUTENGENEZA JEZI FEKI KWA MFANO MTU AKIKUTWA NA JEZI FEKI ALIYEMKAMATA AU ALIYEFANIKISHA HUYO MTU KUKAMATWA APEWA LABDA ELFU 10,000. ANAYEFANIKISHA MTENGENEZAJI AU MFANYABIASHARA MKUBWA KUKAMTWA APEWE LABDA ASILIMIA 10% YA THAMANI YA MZIGO ULIOKAMATWA.

BADALA YAKE YEYE ANABAKI KULALAMIKA KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUWA WATU WASINUNUE JEZI FEKI. LAKINI HASEMI NI MADUKA GANI AU NI SEHEMU GANI HIZO JEZI ORIJINO ZINAPATIKANA.
 
Haji Manara ni burudani tosha. Size yake Jerry Muro hayupo. Level ya Dismas Ten ni kitu kingine kabisa. Haji kapwaya, kabaki na uswahili swahili tu.
 
Yanga bwana eti manara ana mipasho,wakati jerry muro anawaita Simba wa mchangani mlikuwa mnafurahi sana na ilikuwa si mipasho.acheni kelele zenu ,manara ndie anaefaa kuwa msemaji wetu.kwa sasa nyinyi pambaneni na hali zenu msiipangie Simba eti nani wa kufaa na nani hafai.
 
Katika watu mabogus ni Haji Manara
....Hili jamaa halijui chochote kuhusu mpira....Simba ikicheza ikishinda au kufungwa lijamaa linatupa vijembe kwa Yanga....Haji anaifuatilia zaidi Yanga kuliko timu yake ya Simba
 
Katika watu mabogus ni Haji Manara
....Hili jamaa halijui chochote kuhusu mpira....Simba ikicheza ikishinda au kufungwa lijamaa linatupa vijembe kwa Yanga....Haji anaifuatilia zaidi Yanga kuliko timu yake ya Simba
Lazima aifuatilie zaidi Yanga maana baba zake ni Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…