Haji Manara kwa Simba sasa muda wake umeisha

Kwa akili hizi lazima umkubali....maana mnawaza mle mle.... Ndege wa rangi moja huruka pamoja.


Katika Hao Mapimbi wewe Ni Namba moja ingawa unatamani uitwe msomi.

Wewe unataka Watu Wajibu Hoja Kisomi! Je Hapa ndiyo umeniquote Kisomi??

Amakweli "Empty vessel makes more noise "...
Mdogo Wangu Usipate tabu! Wivu wenu utawauwa Bure Haji Hamutamuondoa Kwa Kelele za Mitandaoni...

Kila Ninapoona Nyinyi Mashabiki Wa Yanga munaojifanya Simba Fake Munamchukia Haji Manara! Basi Nazidi Kuthibitisha Kuwa Manara Anafanikiwa Katika Kazi Yake Kwani Siku zote ukiona Mpinzani Wako Anakuchukia basi Juwa upo sawa.

Kwasasa Yanga Mtu wanaemchukia Zaidi Ni Haji Manara! Na Ndiyomana Munatumia Kila Mbinu Kujifanya Nyinyi Ni Simba Eti Haji Afukuzwe!!
Mukiulizwa Sababu gani Afukuzwe? Eti munajibu Hajui Mpira!!! Alaa! Kwani Mumesikia Haji Manara Ni Kocha??? Au mumesikia Anashiriki Kwenye Benchi la Ufundi Timu? Au Mumesikia Yeye Ndiye Anayesajili Wachezaji? Sasa Mambo Ya Kujua Mpira au Kutokujua Yanahusikaje Na Idara ya Habari Ya Simba??

Hebu Nipe Sifa Za Kuajiriwa Ukuu Wa Idara Ya Habari ya Simba CV Yake inatakaje? Na Je elimu gani inahitajika Kuweza Kuwa Kwenye Idara Ya Habari Ya Simba? Je Elimu aliyonayo Haji Manara hawezi Kuwa Kwenye Idara ya Habari Ya Simba?

Acheni Wivu Wa Kike Huo Munapoona Mwanamme Mwenzenu anapiga Kazi.
 
zama ximebadilika mkuu,,sasa hivi mpira ni biashara/ pesa, mambo ya utani wa jadi yamepitwa na wakati, ndio maana mchezaji leo yuko Yanga, kesho Simba....Manara anadhani bado ule unazi wa kizamani wa Simba na Yanga upo...Leo hata Simba akiifunga Yanga hakuna anaeumia wala kujali...Watu wanaangalia mechi za kimataifa unafanya nini
 
Mimi ni Simba kulia lia lakini huyu Manara hakika ni tatizo. Club kubwa kama hii haihitaji kuwa na PR officer kama huyu! Bogus kabisa jamaa! Ukifuatilia anayoandika kwenye mitandao ya kijamii unabaki unashangaa! Magumu wanayopitia Yanga leo yanamuhusu nini kama msemaji wa Simba! Kweli kuna utani wa jadi lakini huu ni too much! Halafu jamaa anatabia ya kunyanyapaa watu, mfano kuna wakati aliwashambulia wanawake wanene na kuandika maneno ya kashfa bila kujiangalia naye watu wakimnyanyapaa uanajisikiaje
! Kimsingi, jamaa ni limbukeni wakupitiliza
 

Haina Shida! Milango ipo wazi Nenda Yanga ambako Kuna Msemaji Wa Timu Mstaarabu Na Msomi.

Sisi Ambaye Tunamkubali Tutaendelea Kufurahia Kuwepo Kwake.

Manake hii Mitandao Ya Kijamii imekuwa Chaka la Kila Mtu sikuhizi... Unamkutia Msukuma Katoka Shinyanga Kaja Bongo Kwa Kusoma Halafu Anamwita Mtoto Wa Mjini Mzaramo Halisi Aliyezaliwa Kinondoni Haji Manara Kuwa Mshamba au Limbukeni. Ridiculous!!!
 
Mhhh unauhakika mkuu na wale wanaocolapse na kulia taifa siku za simba na yanga kwa matokeo ni nani.
Hizi derby huwa haziishi upinzani kuna mifano kibao Al Ahly vs Zamalek ambazo ni most successful club in africa lakini zikikutana ni upinzani mkali hadi watu wanafia uwanjani regardless umefanyaje kwenye ligi au kimataifa. Pia Barca vs maldrid( hii ni ligi ndani ya ligi) hivo advancement ya ligi au timu haiondoi utani/ushindani wa hawa rivals
 
Mmeanza kuelewa somo. Ila mnajifunza 'the hard way'.

Tuliwaambiaga zamani kuhusu Jerry Muro hamkuelewa sasa hivi ndio mnajifanya wazee wa busara. Tulieni tu dawa iingie
 
Wengi hawalifaham hili. Mpira ni ajira,ni biashara. Siyo utani wa simba na yanga.

 
huyo Haji Manara ana ujanja gani?
 
Andika kiswahili sanity basi. Hiki kiswahili cha wapi? Khan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…