Haji Manara: Mimi na kocha Gamondi hatusalimiani, aliwahi kunipa tuhuma nzito kutaka yeye afukuzwe Yanga

Haji Manara: Mimi na kocha Gamondi hatusalimiani, aliwahi kunipa tuhuma nzito kutaka yeye afukuzwe Yanga

KWAHAJI MANARA HAKUNA MTU MWEMA.

HAJI ANA ROHO MBAYA SANA, ROHO MBAYA MNO, ROHO YA KISWAHILI, ROHO YA KOROSHO.
 
  • Kicheko
Reactions: Tui
1731146371413.png
 
“Unajua nilifungiwa na nilichokitegemea baada ya kufunguliwa sicho nilichokikuta, kumbuka nilifungiwa kwasababu ya Yanga na nilitegemea support kutoka kwa Yanga ila ilikuwa tofauti lakini wakati mwingine ndio Binadamu ila ipo siku nitasema maana nilikuwa nalazimishwa kuomba msamaha na ilikuwa inatumiwa kama fimbo yake kunichapia”

- Haji Sunday Manara kupitia AMPLIFAYA ya @cloudsfmtz
 
Wakuu msikie Manara huko!

Anasema katika kipindi cha kuelekea katika kilele cha wiki ya mwananchi mwezi Agosti mwaka huu 2024 wakati ameenda kambi ya Timu ya Yanga kuongea na wachezaji na bechi la ufundi ili kuwapa plan ya siku hiyo ya wiki ya mwananchi, lakini siku yake ikaharibiwa na kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamond.

Kwa madai ya Manara anasema kocha Gamond alimwambia wewe Haji Manara nasikia ulipost Instagram kwamba mimi nifukuzwe unitaki niwepo Yanga. Manara alipigwa na mshangao baada kuyasikia hayo.

Na tangu hapo hawajawi kuongea na wala kusalimiana licha Manara anasema yeye anamkubali kocha na bado anastahili kuendelea kubaki Yanga zaidi.

Vipi hapo wadau huyu Manara alichesema

Sasa naiona Yanga inaelekea kujua walifanya kosa kubwa, siku za nyuma. Kuna miiba huwa inajua kuingia tu, kutoka ni lazima itoke na roho.

Wakati ule ilikuwa ni 'Manara Karibu Sana Yanga', ila sasa ni 'Yanga Karibu Sana kwa Manara'.

Ova
 
KWAHAJI MANARA HAKUNA MTU MWEMA.
HAJI ANA ROHO MBAYA SANA, ROHO MBAYA MNO, ROHO YA KISWAHILI, ROHO YA KOROSHO.
Haji ni mbinafsi. Anakupenda pale ambapo anajua anapata yeye maslahi. Pale ambapo hapati, anaenda kwenye media kuzungumza negatives. Hii si roho ya kibinadamu
 
Wakuu msikie Manara huko!

Anasema katika kipindi cha kuelekea katika kilele cha wiki ya mwananchi mwezi Agosti mwaka huu 2024 wakati ameenda kambi ya Timu ya Yanga kuongea na wachezaji na bechi la ufundi ili kuwapa plan ya siku hiyo ya wiki ya mwananchi, lakini siku yake ikaharibiwa na kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamond.

Kwa madai ya Manara anasema kocha Gamond alimwambia wewe Haji Manara nasikia ulipost Instagram kwamba mimi nifukuzwe unitaki niwepo Yanga. Manara alipigwa na mshangao baada kuyasikia hayo.

Na tangu hapo hawajawi kuongea na wala kusalimiana licha Manara anasema yeye anamkubali kocha na bado anastahili kuendelea kubaki Yanga zaidi.

Vipi hapo wadau huyu Manara alichesema

Yule albino fala sana sasa anasema kipindi hiki kigumu kwa kocha ili iweje , mnafiki mkubwa

USSR
 
Sasa nawaona Yanga wanaelekea kutambua kwamba walifanya kosa kubwa, siku za nyuma. Kuna miiba huwa inajua kuingia tu, kutoka ni lazima itoke na roho.

Lilikuwa kosa kubwa Haji kuingia yanga kosa kubwa sana

Ussr
 
Mpira wa bongo uswahili mwingi sana
 
BAADHI YA KAULI ZA HAJI MANARA LEO KWENYE MAHOJIANO YAKE

"Kwasasa sina mahusiano mazuri na Hersi, hatujazungumza
kama miezi miwili hivi. Sina la kuongea nae maana yetu alisema mimi ni Mwanachama tuu hivyo siwezi kumtafuta nalinda brand yangu"

"Tulikuwa verry close, Yeye ndiyo alisema mimi ni Mwanachama na Kutokana
na mazingira unakaa pembeni unatazama tu maana Yanga ni taasisi na sio
mtu"

"Mimi ni mkubwa kidogo na katika Mpira Nina uzoefu kidogo hasa katika eneo la Mpira, kuna watu wana uoga, unaweza ukawa na uwezo lakini ukakosa uzoefu, sipendi kuzungumzia inshu za watu Mimi ni mkubwa nishavuka huko, Mimi ni msemaji muekezaji,

Nimewekeza kwenye eneo Hilo la usemaji, wao wafanye kazi yao lakini siwezi kukaa na kuwajadili watu kama wao wanavyofanya" alisema Haji Manara

Cc #MillardAyo
 
“Simba imefika mpaka Nusu Fainali mwaka 1974 , hakuna kipya tunachokifanya sasa hivi ambacho huko nyuma hakikufanyika hakipo”

HAJI MANARA- Via Amplifaya ya Clouds Fm
 
Haji Manara ameeleza mahusiano yake na kocha Gamondi akidai kuwa "hatusalimiani, ni kocha anayependa vimaneno maneno".

Video: Millard Ayo
 
Hapa Bugatti kaongea fact, nimecheki body language yuko real, binafsi nampongeza, kaongea bila kupepesa, kupinga ukweli kwangu dhambi. Ila namsihi aache tabia ya visasi maana ni kujiumiza wewe mwenyewe.

Huyu jamaa Haji bado soka letu linamhitaji, nani mwenye influence kama yeye? Ukweli hakuna, maana akiongea kitu ukakereka ujue ana hoja na imekuchoma, nawasihi Yanga wawe positive, watafute namna ya kumtumia , Haji bado ana kitu kikubwa cha ku offer timu, si lazima kuwa msemaji, labda awe akienda uwanjani kuhamasisha na alipwe.
 
Back
Top Bottom