Haji Manara ni Mswahili anayecheza na akili za Waswahili wenzake

Sio uongo vilabu vya Simba au hata Yanga vina Waswahili wengi sana ambao % kubwa shule ni zero na wanacho penda ni kusikia wakikandiana, na kutambiana wachezaji, kutambiana makocha, ndo maana vijiwe vya mashabiki wa Simba na Yanga ambavyo almost asilimia 100 huwa ni waswahili swahili pale huwa ni kukandiana tu hakuna kingine wanacho jua na huwezi wakuta wanajadili hata Uwekezsji kwenye virabu vyao make hizo ni maada ambazo kamwe hawawezi hata ziongea kwa sekunde 7.

Mo ndo maana anawa buruza kwa sababu anajua mashabiki asilimia kubwa ni waswahili ambao shule ni hakuna.

Huyu sasa msemaji wa Simba ni Mtu mjanja mjanja mswahili anacheza na akili za waswahili wenzake, haiwezekani msemaji wa Clabu yeye kila siku ni mipasho kwa timu pinzani yaani huwezi kuta post zake zinazungumzia maendeleo ya Mpira wa Simba hapana yeye ni mipasho kwa Yanga, post zake kwenye page yake zimejaa mipasho tu. Huyu ndo MO anawataka wa aina hii waswahili, klabu za wenzetu huwezu kuta msemaji wa Clabu A anahangaika na mambo ya Clabu B make hayamuhusu ila huku Bonho kwa sababu ya aina ya mashabiki tulio nao uswahili ndo unaonekana dili.

Maendeleo ya soko hapa Tanzania yanarudiswa nyuma na aina za Mashabiki wa hizi virabu vikongwe, mashabiki waswahili ambao wanacho jua ni kufungana basi hawajui kingine. Ndo maana unakuta Mechi ya Simba lets say na JKT Oljoro utajuta Jezi zinazo uzwa pale ni za Yanga na Simba unajiuliza kulikoni?

Mashabiki wa Simba na Yanga ndo wanao rudisha nyuma soka la Tanzania, mashabiki waswahili vichwani zero kabisa.
Heri yako mzungu
 
Kwa asili ya soka la Tanzania, Simba na yanga ndiyo nguzo za ligi yetu, tuna derby moja tu, bila kuongeza ushwahili mwingi Kama wa haji manara hakutakuwa na ushindani.

Jiulize utawashawishi vipi watu wajaze uwanja wa taifa (60,000+) bila uswahili na matani ya kutambiana?

Usije ukalinganisha soka la Ulaya na Tanzania, hatutawafikia waliko ila wacha na sisi tuburudike.

Haji manara atabaki kuwa mswahili mwenye ushawishi mkubwa Sana katika soka la Tanzania kwani anasaidia Sana Simba kupata mapato na kuongeza mashabiki.

Big up Bugatti, Haji S. Manara
kwa taarifa yako mechi ya simba na yanga inajaza uwanja toka miaka ya 70's huko, hata huyo haji hajazaliwa, haji ana ushawishi kwa simba wenzake, sio soka la tanzania, ukae uelewe
 
Haji Manara hana ushawishi wowote kwenye klabu ya Simba au mpira wa Tanzania, Kinacho isaidia Simba ni MO kwakua ameweka fedha kwenye timu na timu inapata matokeo.

Mashabiki watakuja na watasafiri na timu inayo shinda tu.
Haji Manara alikua akiuza pafyum unajua Nini kilimtokea!! Anakesi ya Wizi wa kuaminika na pafyumu ziligoma kununuliwa. Kama ingekua ana ushawishi angeanza na pafyum zake kwanza. Angalia juzi aliposhindwa ku ujaza Uwanja na alidai watajaza viwanja viwili.
Simba na Yanga hazi itaji mpiga debe iyo hatua zilisha ivuka kitambo sana.
Teh teh 🎶 teh 🎶 teh teh 🤣 🤣haya maneno yamenifurahisha sana haaa haaaa...😃😃😃
 
Sio uongo vilabu vya Simba au hata Yanga vina Waswahili wengi sana ambao % kubwa shule ni zero na wanacho penda ni kusikia wakikandiana, na kutambiana wachezaji, kutambiana makocha, ndo maana vijiwe vya mashabiki wa Simba na Yanga ambavyo almost asilimia 100 huwa ni waswahili swahili pale huwa ni kukandiana tu hakuna kingine wanacho jua na huwezi wakuta wanajadili hata Uwekezsji kwenye virabu vyao make hizo ni maada ambazo kamwe hawawezi hata ziongea kwa sekunde 7.

Mo ndo maana anawa buruza kwa sababu anajua mashabiki asilimia kubwa ni waswahili ambao shule ni hakuna.

Huyu sasa msemaji wa Simba ni Mtu mjanja mjanja mswahili anacheza na akili za waswahili wenzake, haiwezekani msemaji wa Clabu yeye kila siku ni mipasho kwa timu pinzani yaani huwezi kuta post zake zinazungumzia maendeleo ya Mpira wa Simba hapana yeye ni mipasho kwa Yanga, post zake kwenye page yake zimejaa mipasho tu. Huyu ndo MO anawataka wa aina hii waswahili, klabu za wenzetu huwezu kuta msemaji wa Clabu A anahangaika na mambo ya Clabu B make hayamuhusu ila huku Bonho kwa sababu ya aina ya mashabiki tulio nao uswahili ndo unaonekana dili.

Maendeleo ya soko hapa Tanzania yanarudiswa nyuma na aina za Mashabiki wa hizi virabu vikongwe, mashabiki waswahili ambao wanacho jua ni kufungana basi hawajui kingine. Ndo maana unakuta Mechi ya Simba lets say na JKT Oljoro utajuta Jezi zinazo uzwa pale ni za Yanga na Simba unajiuliza kulikoni?

Mashabiki wa Simba na Yanga ndo wanao rudisha nyuma soka la Tanzania, mashabiki waswahili vichwani zero kabisa.
Maelezo marefu nonsense. Mswahili ni nani? Define it. Kweli ww POPOMA
 
Huyu manara ipo siku atawaambia waende uwanjani bila chupi, na hutoamini kukuta 99.9% hawajavaa kweli. Mbaya zaidi mijitu mingine ina elimu zao kubwa tuu lakini wanashikiwa akili na yule mtoto wa kiswahili..
 
Mkuu leo ndio nmeamini maana sikuwahigi kumfatilia Jana kampiga dongo la wazi Harmonize nmejiskia aibu mimi aisee, Sijawahi kuona msemaji Asiyejielewa majukumu yake kama Yule jamaa
 
Back
Top Bottom