Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,046
- 3,971
Uongozi wa klabu ya Simba umesema hauna mpango wa kumtimua kocha Joseph Omog kama inavyovumishwa hivi karibuni.
Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba, Haji Manara alisema Omog anatimiza kile wanachokihitaji kwake hivyo hawawezi kuivuruga timu kwa kumtimua.
"Kabla ya mechi yetu jana dhidi ya Mwadui FC, Rais wa klabu ya Simba alikutana na kocha Omog na kumfikishia ujumbe kutoka kamati ya utendaji kuwa tuna imani naye na tunamsapoti kwa kila anachokifanya.
Taarifa kuwa timu imempa Omog mechi tano sio za kweli na hatuna mpango wa kumtimua kwa sababu anafanya vizuri," alisema Manara.
Manara alisema Simba haiwezi kuendeshwa na kelele za mashabiki na badala yake iko makini katika maamuzi na utendaji wake wa kila siku.
CHANZO: Mwananchi