Haji Manara: Simba siyo baba wala mama yangu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Msemaji mkuu wa klabu ya Simba amesema Simba siyo baba wala mama yake.

Manara amesema anaweza kujipatia riziki yake kupitia vyanzo vyake vingine vya mapato na si lazima iwe klabuni hapo.

Manara amenikumbusha sana mwalimu JK Nyerere japokuwa muktadha ni tofauti.

Chanzo: Clouds TV

Usiku mwema
Maendeleo hayana vyama!

=====

Afisa Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amewatolea povu watu wote wanaomtukana mitandaoni pale tu klabu ya Simba inapofungwa.

Manara amesema kazi yake ni kuisemea timu na kutoa taarifa zote zinazohusu klabu hiyo na si vinginevyo, hivyo kitendo cha watu kumtukana kama vile yeye ndiye Mchezaji au Kocha kinamkwaza sana.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara amefunguka kuchukizwa na kitendo cha mashabiki wa klabu hiyo kumtukana baada ya timu hiyo kupoteza nafasi katika michuano ya SportPesa Cup.

Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara.

Manara ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari leo Januari 26, ambapo amesema kuwa anasikitishwa na kitendo cha mashabiki hao kuingilia maisha yake binafsi.
"Nimechukizwa sana na mashabiki wa Simba kunitukana kwenye mitandao, kufikia hatua ya kunitukania mama mzazi kisa klabu kufungwa hawataki nifanye vitu vyangu binafsi, wanahoji kwanini nazindua bidhaa zangu wakati timu imefungwa", amesema Manara.

Ameongeza kuwa, "Haiwezekani kutofanya fanya shughuli zangu kisa Simba imefungwa, hiki ni kipato changu maana nina maisha yangu, waambieni kuwa sijawahi sema Simba nitaishi milele, nitabaki kuwa shabiki milele lakini sio kwenye kufanya kazi na tusichukuliane poa".

Baada ya Simba kutolewa na Bandari FC katika nusu fainali ya michuano ya SportPesa kesho itacheza na Mbao FC ili kusaka nafasi ya tatu.
 
Mm sina kusema

Chagua kusuka au kunyoa
 
Baada ya kupita maneno mengi kati ya Mkuu wa kitengo cha habari cha Simba SC na Mchambuzi wa soka Shaffih Dauda. Haji manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Unajua nini kilitokea kule Kinshasa baada ya kipigo kile? Nawaibia siri kidogo, jamaa immediately akapost dhihaka moja ya kutuumiza, akaja hotelini kwetu.

Nilikuwa zaidi ya chui nilipomuona, ila mambo ya kispoti na yanaisha pale pale, na siku zote tukiparurana mitandaoni si kwamba tunachukiana ila kila mmoja anatetea mkate wake, yeye anatafuta followers na mimi natetea Simba yangu.

Muelewe mimi sina nogwa langu limeisha hivyo. Karibu Mr Underdog".

Sent using Jamii Forums mobile app
 

hiyo kauli imenifanya nikumbuke richmond na maazimio ya kamati teule, kweli hii nchi hatujifunzi kutokana na makosa.
 
Ukitoa madhaifu machache ambayo ni kawaida kwa kila binadamu lakini anafanya vizuri sana. Huyu ni moja ya watu ambao wananifanya nitafakari sana swala la vyeti hapa Bongo. Elimu yetu ina matatizo makubwa sana. Mtu kama haji manara anatusua hapa town kwa mbinu za kisomi anazozitekeleza kwa akili ya kawaida tu bila vyeti huku PHDs zikitia aibu!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
babake si ndo yule alikuwaga wanamwita eti computer??.. simba inakuwaje babake?? aache kuweweseka yule..
 
Niliwahi kusema hapa,kwenye uzi wangu,anashindwa kutofautisha kati ya haji km personality na haji km msemaji wa simba.
Bodi ya simba mwangalieni kwa jicho la pili...

Sent using Jamii Forums mobile app
Msemaji wa klabu!!Huyu Ni Afisa Habari wa Simba Asiyejuwa hata kutumia Computer Hana Taalauma yoyote kwenye IT Ni Zero Brain Utoto wa mjini tu unamlinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Manara ana ndimi mbili moja ya kuelezea ufundi na utaalam wa wachezaji wa Simba pamoja na beberu (ndevu) Aussems lakini nyingine ya kuruka Kimanga na kuwalaumu na kuwabeza mashabiki simba wanao mhoji kuhusiana na kile alicho waaminisha tena kwa majigambo makubwa huyu " mbunge" mtarajiwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…