sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Bro Haji alama za nyakati zinaanza kukukataa kwenye game yako uliyoweza kuimasta kwa muda mrefu ya usemaji wa timu za mpira.
Kila nikitazama miaka mitatu mpaka minne sikuoni tena ukiwa na ule ushawishi kwenye timu za football.
Nakushauri ustaafu kabla haujastaafishwa kwa aibu.
Nimekuwa nikifatilia trend yako na timu yako ya sasa ni wazi wanashindwa tu kukwambia ujiongeze. Kuendelea kuwachokonoa wenzio kwenye timu tena wenye timu yao ni dalili ya kifo cha nyani miti yote inateleza.
Soma Pia: Eng. Hersi: Haji Manara sio Msemaji wa Yanga, tunaangalia majukumu mapya ya kumpa
Kwenye idara ya usemaji wewe ni masta ila wakati umeanza kukukataa wewe ni mtoto wa mjini jiongeze Yanga hawaoni tena umuhimu wako kama vile wewe unavyojipa umuhimu.
Na nje ya kuzisemea Yanga na Simba hakuna mtu atakupa tena attention utaenda kugombania milupo na kina Dulla makabila