Haji Manara vs Ahmed Ally na Ally kamwe, nani ameweza kujaza uwanja wa Mkapa?

Haji Manara vs Ahmed Ally na Ally kamwe, nani ameweza kujaza uwanja wa Mkapa?

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Nakumbuka zile mechi za CAF za Simba kipindi Haji Manara Afisa habari wa Simba, alikuwa anajaza uwanja wa Mkapa alikuwa ana press nyingi sijui, atembee kwenye masoko, gereji, kariakoo n.k, Haji Manara kwenye uhamasishaji Yuko vizuri kuliko Ahmedy Ally na Ally kamwe

Ahmedy Ally kwenye uhamasishaji bado, labda ndio mwazoni tumpe muda atakuwa vizuri.

Ahmedy Ally na Ally kamwe wana mengi ya kujifunza kwa Haji Manara.
 
Haji ni promoter mzuri sana wa jambo, hao uliowataja wanafanya aliyokwisha fanya manara!. Manara amefanya watu waupende mpira, manara ni Kama mandonga leo Tz watu walio wengi wanafuatilia ndondi kisa mandonga...
 
Aseeee.......
IMG_20230308_142512.jpg
 
Watu wanaenda uwanjani kulingana na Ukubwa wa tukio.
Ukubwa wa mchezo husika na umuhimu wa huo mchezo.

Sijawahi kwenda uwanjani kwababu ya yoyote Katika hao.

Nilienda Mechi ya stars na Blazil.
Hakuna aliyenipeleka Bali tulio la kihistoria
 
Wacheze Simba/Yanga Vs Mtibwa alafu wape kazi hao jamaa wahamasishe mashabiki waje nusu tu ya uwanja uone jinsi mambo yalivyo.
 
Haji ni promoter mzuri sana wa jambo, hao uliowataja wanafanya aliyokwisha fanya manara!. Manara amefanya watu waupende mpira, manara ni Kama mandonga leo Tz watu walio wengi wanafuatilia ndondi kisa mandonga...
uongo
 
MACHIZI SOKA.

UWANJA UNAJAZWA NA WATU, WATIZAMAJI WA TUKIO HUSIKA.
 
Haji ni promoter mzuri sana wa jambo, hao uliowataja wanafanya aliyokwisha fanya manara!. Manara amefanya watu waupende mpira, manara ni Kama mandonga leo Tz watu walio wengi wanafuatilia ndondi kisa mandonga...
Hapana nakataa,
Kwamba haji amefanya watu waupende mpira?
Labda umezaliwa Jana.

Simba na yanga zimekua zikipendwa toka kabla ya uhuru.
Na soka ambayo wewe unaiita mpira kwa Tanzania imekua ikipendwa toka Nyerere akiwa bado hajaingia mjini DSM.
Hebu kua serious basi kidogo bana.
 
Back
Top Bottom