Haji Manara: Yanga SC itakuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kutwaa taji la CAFCL

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Ndugu Haji Sunday Manara leo kwenye Press Conference Klabu bingwa ya kihistoria ametanabaisha kuwa kwa mipango aliyoishuhudia ndani ya klabu hiyo anaamini kuwa kama kuna klabu yeyote Afrika Mashariki inatwaa Ubingwa wa CAFCL basi klabu hiyo itakuwa ni YANGA SC.

Hayo ameyasema akiwa anasukumwa na mambo mbalimbali na mipango ya muda mrefu na mfupi iliyowekwa klabuni hapo.

Aidha, Manara ameweka wazi kuwa kutokana na mazingira mazuri ya mabadiliko ya kuliuendeshaji klabu yaliyofanyika klabuni hapo yanampa kiburi zaidi kuamini kuwa hata wapinzani wao (SIMBA SC) hawana uwezo wa kufanya vyema kwa sababu kuna ubabaishaji mwingi katika namna wanavyo endesha klabu yao.
 
Ninachojua mimi ubingwa hauji kwa matamko ya watu fulani, ila kama mnahisi huu ubingwa mmeupata kwasababu ya ujio wa manara kwenye team yenu basi hata CAFCL mtashinda msimu ujao.

KEY POINT
"Kama mnaamini huu ubingwa mmeupata kwasababu ya ujio wa manara" , vinginevyo mna kazi kubwa ya kufanya maana mbio za CAFCL na CAFCC ni tofauti kwa 100% na zile za ligi.
 
Na Yanga itakuwa timu ya kwanza kuwa na mashabiki wajinga kupitiliza wasio jifunza kupitia makosa kwa kuamini mdomo wa manara ambao miezi kadhaa iliyopita mdomo huo huo uliongea uongo kuhusu Yanga kushiriki CAF hatua ya awali.
 
Manara yupo sahihi

Yanga itakuwa timu ya kwanza kutwaa caf champions legue kutoka africa mashariki kama gsm akiendelea kutoa hela zaidi na zaidi mbeleni.. ila sio msimu huu wala ujao. Sio kwa kikosi hiki cha sasa.

Mimi mwanayanga ila natambua bado hatujawa tayari kutwaa caf champions league kwa kikosi cha sasa hivi.

Ni ngumu sana kutwaa ubingwa huo kwa kutegemea beki mwenye umbo kama la kibwana shomari. Kiungo kama Fei Toto na mshambuliaji kama mayele sio level za kutwaa caf champions league.

Mtu naemwona yupo tayari ni mmoja tu ambaye ni goal keeper ila wengine wote waliobaki hawawezi kutufanya yanga tutwae caf champions league.
 
Manara ni mtu ambaye yuko tayari kufanya chochote kumfurahisha boss.

Tangu yuko klabuni hapo tayari kaishatengeneza matabaka kwa kuvuruga mahusiano baina ya wafanyakazi aliowakuta na boss mkuu.

Mashabiki wa Yanga wanamuona manara ni mtu anayewafaa kwasababu timu yao imewapa kile walicho kitaka.

Na ndio maana huu muda ambao Yanga imechukua kombe unamuona manara anatumia muda mwingi kuipamba Yanga na kuinanga Simba

Anafanya hayi ili kitengeneza backup pale ambapo siku imetokea Yanga imefanya vibaya basi mashabiki wataoanza kulaumu swala la manara kuletwa klabuni wakose nguvu kwasababu kuna references zipo zinaonyesha jinsi jamaa alivyokuwa na mahaba ya kweli na timu katika kipindi ambacho timu inafanya vizuri.
 
Mwishoni nilijua utamalizia kwa kuandika "natania"

Yani kuchukua kombe ligi kuu ndio umejipa confidence ya viwango vya CAF?

Yani umepiga vi pushups viwili tayari umeanza kutembea kifua wazi unatanua ki chest unajiita the rock?

Eti GSM aweke hela.... Achilia mbali ubingwa niambie huyo mjasiliamali ana hela gani gani ya kuifadhili yanga mpaka tu wakafika nusu fainali?

Hatuongei tu kwasababu hatupendi kuwaona mkiumia nyoyo zenu, ila ukweli ni ngumu sana kwa timu ambayo haijawahi kufika robo fainali ya CAF kupewa advantage kwa kufikiriwa kuwa itakuwa timu ya kwanza kubeba ubingwa wa CAF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…