Haji Manara: Yanga SC itakuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kutwaa taji la CAFCL

Haji Manara: Yanga SC itakuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki kutwaa taji la CAFCL

Attachments

  • FB_IMG_1655579378566.jpg
    FB_IMG_1655579378566.jpg
    31.8 KB · Views: 2
Kwani Tp Mazembee iko ukanda gani wakina uto?
 
Haji mjanja hajasema mwaka ambao yanga itachukua
 
Ndugu Haji Sunday Manara leo kwenye Press Conf ya Klabu bingwa ya kihistoria ametanabaisha kuwa kwa mipango aliyoishuhudia ndani ya klabu hiyo anaamini kuwa kama kuna klabu yeyote afrika mashariki inatwaa Ubingwa wa CAFCL basi klabu hiyo itakuwa ni YANGA SC.

Hayo ameyasema akiwa anasukumwa na mambo mbalimbali na mipango ya muda mrefu na mfupi iliyowekwa klabuni hapo.

Aidha, Manara ameweka wazi kuwa kutokana na mazingira mazuri ya mabadiliko ya kuliuendeshaji klabu yaliyofanyika klabuni hapo yanampa kiburi zaidi kuamini kuwa hata wapinzani wao (SIMBA SC) hawana uwezo wa kufanya vyema kwa sababu kuna ubabaishaji mwingi katika namna wanavyo endesha klabu yao.
Unaionhlgelea hii utopwinyo hii hii au kuna nyingine..? Afu why kila ka press keni mnaiongelea simba?? Simba hawana time ya kuongelea manyani kwenye press zao. Mjitambue kwanza. Kombe la CAF au La CUF ya lipumba tujuzane. Maana hayo mashindano mwaka huu unaoanza mpaka simba anaanza kucheza nyie msharudi kidimbwi
 
Manara yupo sahihi

Yanga itakuwa timu ya kwanza kutwaa caf champions legue kutoka africa mashariki kama gsm akiendelea kutoa hela zaidi na zaidi mbeleni.. ila sio msimu huu wala ujao. Sio kwa kikosi hiki cha sasa.

Mimi mwanayanga ila natambua bado hatujawa tayari kutwaa caf champions league kwa kikosi cha sasa hivi.

Ni ngumu sana kutwaa ubingwa huo kwa kutegemea beki mwenye umbo kama la kibwana shomari. Kiungo kama Fei Toto na mshambuliaji kama mayele sio level za kutwaa caf champions league.

Mtu naemwona yupo tayari ni mmoja tu ambaye ni goal keeper ila wengine wote waliobaki hawawezi kutufanya yanga tutwae caf champions league.
Hapo kwa Mayele bosi tafakari tena.
Kwa mfano wale Pirates wangekuwa na mtu kama Mayele ile confederation wangechukua. Mayele ni goal getter. Hilo halina ubishi kwa sasa
 
Yani Simba kufika robo fainali hizo mara kadhaa imefanya hadi timu ambazo hazijawahi kuvuka group stage ya CAFCL kuanza kuota ubingwa. Sio rahisi kiasi hicho, focus yenu iwe kufika makundi kwanza.
 
Hapo kwa Mayele bosi tafakari tena.
Kwa mfano wale Pirates wangekuwa na mtu kama Mayele ile confederation wangechukua. Mayele ni goal getter. Hilo halina ubishi kwa sasa

Hoja yangu imeongelea caf champions league wewe unatoa mfano wa confederations cup, kumbuka Mayele kacheza champions league sana na club yake ya zamani.. alifunga magoli mangapi caf champions league.

Kufunga magoli mengi ligi ya Tanzania sio sababu ya kumuona mtu bora . Makambo alifunga sana ligi yetu kuliko mayele ila caf champions league alichemsha sana tena na timu kalii kama horoyaa kila msimu inafika robo ama makundi.. ila makamboo alifeli sabab beki za caf champions league sio kama za ligi ya Tanzania.

Kina bocco nao ligi yetu wamefunga sana ila kwenye caf wanachemsha sababu beki za caf sio sawa na beki za ligi yetu
 
Yani Simba kufika robo fainali hizo mara kadhaa imefanya hadi timu ambazo hazijawahi kuvuka group stage ya CAFCL kuanza kuota ubingwa. Sio rahisi kiasi hicho, focus yenu iwe kufika makundi kwanza.
ni kama kitaani unakaa na washkaji mtaani ila ukiingia chimbo unakaza unatoboa. sasa washakaji wanajitia ujinga wanaona easy tu
 
L
Ndugu Haji Sunday Manara leo kwenye Press Conference Klabu bingwa ya kihistoria ametanabaisha kuwa kwa mipango aliyoishuhudia ndani ya klabu hiyo anaamini kuwa kama kuna klabu yeyote Afrika Mashariki inatwaa Ubingwa wa CAFCL basi klabu hiyo itakuwa ni YANGA SC.

Hayo ameyasema akiwa anasukumwa na mambo mbalimbali na mipango ya muda mrefu na mfupi iliyowekwa klabuni hapo.

Aidha, Manara ameweka wazi kuwa kutokana na mazingira mazuri ya mabadiliko ya kuliuendeshaji klabu yaliyofanyika klabuni hapo yanampa kiburi zaidi kuamini kuwa hata wapinzani wao (SIMBA SC) hawana uwezo wa kufanya vyema kwa sababu kuna ubabaishaji mwingi katika namna wanavyo endesha klabu yao.
Labda kombe la bilauri....yaan iyo group stage tu kwanza kuicheza mwakq jana walishindwaa walitolewa mapemaa
 
Ndugu Haji Sunday Manara leo kwenye Press Conference Klabu bingwa ya kihistoria ametanabaisha kuwa kwa mipango aliyoishuhudia ndani ya klabu hiyo anaamini kuwa kama kuna klabu yeyote Afrika Mashariki inatwaa Ubingwa wa CAFCL basi klabu hiyo itakuwa ni YANGA SC.

Hayo ameyasema akiwa anasukumwa na mambo mbalimbali na mipango ya muda mrefu na mfupi iliyowekwa klabuni hapo.

Aidha, Manara ameweka wazi kuwa kutokana na mazingira mazuri ya mabadiliko ya kuliuendeshaji klabu yaliyofanyika klabuni hapo yanampa kiburi zaidi kuamini kuwa hata wapinzani wao (SIMBA SC) hawana uwezo wa kufanya vyema kwa sababu kuna ubabaishaji mwingi katika namna wanavyo endesha klabu yao.
Kwani haisemei Yanga mpaka aitaje Simba?

Ukiona mke anakutaja taja sana, tambua anakupenda. Ana mahaba nawe.
Haiwezekani, kila jambo aliongealo, lazima aitaje Simba!! Anawashwa washwa huyu eee!!
 
Ukimsikiliza manara ndo unajua kweli kaumia kuondoka simba wakaamua kuweka kambi mbele ya jengo la simba ili simba wafanye vurugu ila simba wana akili sio kama utopolo wanaoenda airport kupokea wageni simba wakakausha kama hakijatokea kitu.
Nilishangaa sana siku ile waliyoweka standi pale Msimbazi. Yaani utafikiri mawifi wanaokwenda kufanya vurugu kwa mke mwenza!! Halafu kuna watu wana PhD kule. Ila kwa vile mwenyewe alishasema kuwa kuna wawili tu, basi.
 
Tunadanganywa kwenye siasa na kwenye mpiea pia nako wanatudanganya.
 
Hapana.

Hawajazoea vya kuiba.

WanaJangwani wanatamaduni ya kulipa gharama ya kile wanachokihitaji.
Tumesikia wataomba CAF waanzie away waje wamalizie home! Sawa, mipango mizuri. Ila....!
 
Back
Top Bottom