wanaume wa hivyo hivi bado wanaexist??? he is a real man asee! khaaaaaaaaaaa!
Jana majira ya saa tatu unusu nikiwa najifanyia kazi zangu kwenye laptop, huku nikipitisha macho kwenye TV, ghafla nikaona kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV na kuongozwa Salama Jabir, kikianza na mhojiwa akiwa Haji Ramadhan.
Baada ya Mazungumzo ya muda fulani, Salama alimuuliza Haji kuwa kuna tetesi kuwa alipokuwa yupo kambini kwenye BSS, Mkewe Haji alipata mimba isiyo ya mumewe, Je hbr hizo zina ukweli? Haji alijibu kuwa habari hizo ni za kweli kuwa mkewe alishika mimba ya mwanaume mwingine yeye akiwa kambini Dar kwenye BSS, na hivi sasa amemsamehe mkewe na analea huyo mtoto asiye wake pamoja na watoto wake 2 wa kuzaa!
Sababu kubwa ya kumsamehe mkewe ni kuwa hakupenda watoto wake waje waishi maisha ya taabu bila mapenzi ya mama yao au kulelewa na mama mwingine. Kwa maana hiyo alikuwa tayari kusamehe yote kwa faida ya maisha ya baada ya wanawe.
Nini cha kujifunza?
Hatma ya ndoa ya mtu ipo kwenye mikono yake mwenyewe. Ni vyema kusameheana kwa makosa tunayofanyia ndani ya ndoa ili kunusuru maisha ya baadaye ya watoto wetu. Kama wanaume wote tungekuwa na huruma na upendo mwingi kama wa ndugu yangu Haji (Maana hata mimi HorsePower sijui kama nigeweza kusamehe, loh!), watoto wa mitaani wasingelikuwepo kabisa, maana isingekuwa taabu mtu kulea mtoto wa mwenzie, na pia kila baba angeweza kuwajibika kwa watoto wake.
Hongera sana Haji, umeonyesha ni namna gani umeweza kuwa baba unayetanguliza upendo wa familia mbele zaidi kuliko mambo mengine. Nashauri kwa kila mwenye MOYO wa AINA hii, aweze kusamehe kwa faida ya familia. Pia wadada msibwete na kuanza kuzaa hovyo nje mkijuwa kuwa mtasamehewa, acheni, mtakutana na akina HP watawapiga talaka bila hata kuangalia nyuma!
Swali kwa Wana JF?
Je, ungelikuwa wewe ndo umekutwa na haya, ungeweza kusamehe? Unaweza kuonyesha moyo wa kusamehe kwa mkeo kwa level hii?
***** Angalizo: Nimeandika haya hapa kwa kuwa Mhusika aliyazangumza wazi kwenye EATV jana. **********
Limbwata at work!!Hata mimi niliangalia kipindi, i see huyu kijana ni jasiri bwana. Sijawahi kusikia wala kuina, this is my first time kwa kweli.
Big up Haji Ramadhani.
Limbwata at work!!
itakuwaje pale baba mzazi atakapoomba ruhusa ya kumuona mwanae? au atamuasili?? haya maamuzi mengine ni magumu sana na yanahitaji kufikiri kwa mapana sana kabla ya kuamua. Miye kumfumania tu ni kosa kama dhambi ya kumdhihaki roho mtakatifu(haina msamaha) naye ataamua ikiwa atanifumania. khaaaaaaaaaaaaaaa??????????
Kunta Kinte, inawezekana kabisa isiwe limbwata. Moyo wa upendo tu na huruma kwa watoto.
Jana majira ya saa tatu unusu nikiwa najifanyia kazi zangu kwenye laptop, huku nikipitisha macho kwenye TV, ghafla nikaona kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV na kuongozwa Salama Jabir, kikianza na mhojiwa akiwa Haji Ramadhan.
Baada ya Mazungumzo ya muda fulani, Salama alimuuliza Haji kuwa kuna tetesi kuwa alipokuwa yupo kambini kwenye BSS, Mkewe Haji alipata mimba isiyo ya mumewe, Je hbr hizo zina ukweli? Haji alijibu kuwa habari hizo ni za kweli kuwa mkewe alishika mimba ya mwanaume mwingine yeye akiwa kambini Dar kwenye BSS, na hivi sasa amemsamehe mkewe na analea huyo mtoto asiye wake pamoja na watoto wake 2 wa kuzaa!
Sababu kubwa ya kumsamehe mkewe ni kuwa hakupenda watoto wake waje waishi maisha ya taabu bila mapenzi ya mama yao au kulelewa na mama mwingine. Kwa maana hiyo alikuwa tayari kusamehe yote kwa faida ya maisha ya baada ya wanawe.
Nini cha kujifunza?
Hatma ya ndoa ya mtu ipo kwenye mikono yake mwenyewe. Ni vyema kusameheana kwa makosa tunayofanyia ndani ya ndoa ili kunusuru maisha ya baadaye ya watoto wetu. Kama wanaume wote tungekuwa na huruma na upendo mwingi kama wa ndugu yangu Haji (Maana hata mimi HorsePower sijui kama nigeweza kusamehe, loh!), watoto wa mitaani wasingelikuwepo kabisa, maana isingekuwa taabu mtu kulea mtoto wa mwenzie, na pia kila baba angeweza kuwajibika kwa watoto wake.
Hongera sana Haji, umeonyesha ni namna gani umeweza kuwa baba unayetanguliza upendo wa familia mbele zaidi kuliko mambo mengine. Nashauri kwa kila mwenye MOYO wa AINA hii, aweze kusamehe kwa faida ya familia. Pia wadada msibwete na kuanza kuzaa hovyo nje mkijuwa kuwa mtasamehewa, acheni, mtakutana na akina HP watawapiga talaka bila hata kuangalia nyuma!
Swali kwa Wana JF?
Je, ungelikuwa wewe ndo umekutwa na haya, ungeweza kusamehe? Unaweza kuonyesha moyo wa kusamehe kwa mkeo kwa level hii?
***** Angalizo: Nimeandika haya hapa kwa kuwa Mhusika aliyazangumza wazi kwenye EATV jana. **********
Najiuliza japo kwa sauti, huyo jamaa aliyezaa nae wamegombana? Nini kitawafanya wasiendeleze huo mchezo? ndugu yangu mwanamke huyu nitakuwa na mashaka naye kila mara-sasa ni ndoa gani hiyo? wenzangu mna mapenzi kupitiliza, bahati mbaya (nzuri?) mimi hayo mungu hajanijalia!!!