Haji Ramadhan, maamuzi yako yanahitaji pongezi za dhati!!!

Haji Ramadhan, maamuzi yako yanahitaji pongezi za dhati!!!

Kwa kweli hata mimi nilimfuraia huyu dogo, manake ile nafika home nilikuta kipindi hewani, nilipenda sana comment za binti yangu kuhusu hii issue, lakini pia nilishangaa kwasababu ni jana tu asubuhi nilitoka kushauriana na mtu mwingine kuhusu issue inayofanana na hii. Hongera sana inataka moyo na inatia moyo. Katika madhaifu yetu Tunabaki kuwa Binadamu tu.
 
Ashakhum si matusi.... furaha kwanza..maamuzi magumu baadae... siendekezi hiyo machezo....aletwe kifaranga si changu...?!!mwisho wa muneno..
 
Jana majira ya saa tatu unusu nikiwa najifanyia kazi zangu kwenye laptop, huku nikipitisha macho kwenye TV, ghafla nikaona kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV na kuongozwa Salama Jabir, kikianza na mhojiwa akiwa Haji Ramadhan.

Baada ya Mazungumzo ya muda fulani, Salama alimuuliza Haji kuwa kuna tetesi kuwa alipokuwa yupo kambini kwenye BSS, Mkewe Haji alipata mimba isiyo ya mumewe, Je hbr hizo zina ukweli? Haji alijibu kuwa habari hizo ni za kweli kuwa mkewe alishika mimba ya mwanaume mwingine yeye akiwa kambini Dar kwenye BSS, na hivi sasa amemsamehe mkewe na analea huyo mtoto asiye wake pamoja na watoto wake 2 wa kuzaa!

Sababu kubwa ya kumsamehe mkewe ni kuwa hakupenda watoto wake waje waishi maisha ya taabu bila mapenzi ya mama yao au kulelewa na mama mwingine. Kwa maana hiyo alikuwa tayari kusamehe yote kwa faida ya maisha ya baada ya wanawe.

Nini cha kujifunza?
Hatma ya ndoa ya mtu ipo kwenye mikono yake mwenyewe. Ni vyema kusameheana kwa makosa tunayofanyia ndani ya ndoa ili kunusuru maisha ya baadaye ya watoto wetu. Kama wanaume wote tungekuwa na huruma na upendo mwingi kama wa ndugu yangu Haji (Maana hata mimi HorsePower sijui kama nigeweza kusamehe, loh!), watoto wa mitaani wasingelikuwepo kabisa, maana isingekuwa taabu mtu kulea mtoto wa mwenzie, na pia kila baba angeweza kuwajibika kwa watoto wake.

Hongera sana Haji, umeonyesha ni namna gani umeweza kuwa baba unayetanguliza upendo wa familia mbele zaidi kuliko mambo mengine. Nashauri kwa kila mwenye MOYO wa AINA hii, aweze kusamehe kwa faida ya familia. Pia wadada msibwete na kuanza kuzaa hovyo nje mkijuwa kuwa mtasamehewa, acheni, mtakutana na akina HP watawapiga talaka bila hata kuangalia nyuma!

Swali kwa Wana JF?
Je, ungelikuwa wewe ndo umekutwa na haya, ungeweza kusamehe? Unaweza kuonyesha moyo wa kusamehe kwa mkeo kwa level hii?

***** Angalizo: Nimeandika haya hapa kwa kuwa Mhusika aliyazangumza wazi kwenye EATV jana. **********

Hata mimi niliangalia kipindi, i see huyu kijana ni jasiri bwana. Sijawahi kusikia wala kuina, this is my first time kwa kweli.

Big up Haji Ramadhani.
 
hapo ni talaka tuu, naweza kusamehe cheating lakini kuletewa mtoto :<, haikubaliki, aende zake huko. Hata dini zinaruhusu ndoa kuvunjwa iwapo mmoja atasaliti.
 
Mimi nisingesamehe, ingawa mimi ningependa kusamehewa!
 
Haji ramadhani kipindi ulichofanya jana kimetoa somo gumu sana na muhimu kwa wanume wenzio maana wengi walizoea ni baadhi ya wanume wamekuwa wakizini nje kila uchao na kuleta watoto na si mtoto lakini wake zao wamekuwa wakiwapokea na kuwalea bila kuwapa talaka lakini leo wao wanakuhukumu kwa kutoa msamaha kwa mkeo? Kweli baadhi ya "nyani hawaoni kundule"
haji nakupongeza sana na mungu azidi kukujalia maisha marefu na moyo wa huruma wa kuweza kupambana na milima na mabonde najua pia wapo watakaoendelea kukudhihaki tena hadharani ila piga moyo konde mpende mkeo na wanao usijali yasemwayo ila zidi kuongeza ibada na kumwombea mkeo roho ya uzinzi imtoke aridhike na wewe na kuwa mvumilivu asije kuongeza tena mtoto, maana imeonyesha pia alikuwa na mapenzi yasiyouwa na kinga inaaman hajali mardha achilia mbali mimba tena nje ya ndoa ila nadhani ulishamshauri na kumuasa vya kutosha.
Jamani naomba haji asihukumie kwani alieleza sababu ni nyingi zilizomfanya amsamehe mkewe kwanz ani utu, pili mkewe ni yatima na alikuwa hana pa kwenda, pili ni mzazi mweziwe na mwisho hakutaka watoto wake walele na mama wa kambo naye kwa sasa hayuko tayari kuongeza mke au kuoa mwingine kwani anajiheshimu na anamapenzi ya dhati kwa mkewe, sasa kuanza kumtusi kuwa si mwanaume kamili au hajui imani yake hatumtendei haki bali tungemponngeza na kuzidi kumtia moyo ili asahu yaliyotokea na kuzidi kusonga mbele.
Haji keep it up thawabu yako utaipata kwa muumba usijali wasemayo. Hongera sana kwa maamuzi sahihi na somo kwa wanume wengine wasiojua kutoa msamaha kwa wake zao hata wakiunguza chakula tu mateke na matusi achilia mbali kupewa talaka, wakati wao wakiwa na nyumba ndogo lukuki na ukizubaa hata hapohapo ndani wanatoka na mdada wa kazi wa ndani ya nyumba sasa hapo hata heshima kw amkewe hana wadhani leo ataweza kutoa msamaha?
 
Ikiwa alibakwa na kupata ujauzito huo, nitamuelewa, vyenginevyo haikubaliki. Angekwenda
 
itakuwaje pale baba mzazi atakapoomba ruhusa ya kumuona mwanae? au atamuasili?? haya maamuzi mengine ni magumu sana na yanahitaji kufikiri kwa mapana sana kabla ya kuamua. Miye kumfumania tu ni kosa kama dhambi ya kumdhihaki roho mtakatifu(haina msamaha) naye ataamua ikiwa atanifumania. khaaaaaaaaaaaaaaa??????????
 
Tusiwe wepesi kuhukumu, japo swala lenyewe kweli ni very interesting.

MWAKILALI sijajua jinsia yako, but km ni mwanaume jiulize ni mara ngapi umewah kumcheat either mkeo au girlfriend wako?
Na ni wanaume wangapi waneshazaa nje ya ndoa na kualetea wake zao watoto?
 
anachezea makofi ya nguvu, alafu namtwanga talaka tena 3 zote. Na watoto nlozaanaye nampa na siwahudumii. Maana huenda nao sio wangu.
 
Kunta Kinte, inawezekana kabisa isiwe limbwata. Moyo wa upendo tu na huruma kwa watoto.

Najiuliza japo kwa sauti, huyo jamaa aliyezaa nae wamegombana? Nini kitawafanya wasiendeleze huo mchezo? ndugu yangu mwanamke huyu nitakuwa na mashaka naye kila mara-sasa ni ndoa gani hiyo? wenzangu mna mapenzi kupitiliza, bahati mbaya (nzuri?) mimi hayo mungu hajanijalia!!!
 
Jana majira ya saa tatu unusu nikiwa najifanyia kazi zangu kwenye laptop, huku nikipitisha macho kwenye TV, ghafla nikaona kipindi cha Mikasi kinachorushwa na EATV na kuongozwa Salama Jabir, kikianza na mhojiwa akiwa Haji Ramadhan.

Baada ya Mazungumzo ya muda fulani, Salama alimuuliza Haji kuwa kuna tetesi kuwa alipokuwa yupo kambini kwenye BSS, Mkewe Haji alipata mimba isiyo ya mumewe, Je hbr hizo zina ukweli? Haji alijibu kuwa habari hizo ni za kweli kuwa mkewe alishika mimba ya mwanaume mwingine yeye akiwa kambini Dar kwenye BSS, na hivi sasa amemsamehe mkewe na analea huyo mtoto asiye wake pamoja na watoto wake 2 wa kuzaa!

Sababu kubwa ya kumsamehe mkewe ni kuwa hakupenda watoto wake waje waishi maisha ya taabu bila mapenzi ya mama yao au kulelewa na mama mwingine. Kwa maana hiyo alikuwa tayari kusamehe yote kwa faida ya maisha ya baada ya wanawe.

Nini cha kujifunza?
Hatma ya ndoa ya mtu ipo kwenye mikono yake mwenyewe. Ni vyema kusameheana kwa makosa tunayofanyia ndani ya ndoa ili kunusuru maisha ya baadaye ya watoto wetu. Kama wanaume wote tungekuwa na huruma na upendo mwingi kama wa ndugu yangu Haji (Maana hata mimi HorsePower sijui kama nigeweza kusamehe, loh!), watoto wa mitaani wasingelikuwepo kabisa, maana isingekuwa taabu mtu kulea mtoto wa mwenzie, na pia kila baba angeweza kuwajibika kwa watoto wake.

Hongera sana Haji, umeonyesha ni namna gani umeweza kuwa baba unayetanguliza upendo wa familia mbele zaidi kuliko mambo mengine. Nashauri kwa kila mwenye MOYO wa AINA hii, aweze kusamehe kwa faida ya familia. Pia wadada msibwete na kuanza kuzaa hovyo nje mkijuwa kuwa mtasamehewa, acheni, mtakutana na akina HP watawapiga talaka bila hata kuangalia nyuma!

Swali kwa Wana JF?
Je, ungelikuwa wewe ndo umekutwa na haya, ungeweza kusamehe? Unaweza kuonyesha moyo wa kusamehe kwa mkeo kwa level hii?

***** Angalizo: Nimeandika haya hapa kwa kuwa Mhusika aliyazangumza wazi kwenye EATV jana. **********

Mimi si Haji Ramadhani na nashukuru kuwa hayajanitokea yaliyomtokea yeye. Hadi sasa nasema nisingekuwa na moyo huo kwani naogopa huko mbele huyo mtoto tutamtendea haki kweli?
 
Najiuliza japo kwa sauti, huyo jamaa aliyezaa nae wamegombana? Nini kitawafanya wasiendeleze huo mchezo? ndugu yangu mwanamke huyu nitakuwa na mashaka naye kila mara-sasa ni ndoa gani hiyo? wenzangu mna mapenzi kupitiliza, bahati mbaya (nzuri?) mimi hayo mungu hajanijalia!!!

Sikulaumu Kunta Kinte, tumepewa mioyo na karama tofauti.

Kusamehe pia ni kipaji, na si rahisi wote tukawa na roho moja au mafikara yanayofanana.

Na kwa ishu ya Haji, ni jambo la kumpongeza sana, sbb ni wanaume wachache sana may be 0.00001% wanaweza kuwa na ujasiri km wake.
 
Huyo mchizi kuna kitu ana-plan kukifanya, na ni kikubwa tu. Kusamehee inawezekana kibinadam lakini kulea mimba na kisha mtoto wa mwanaume mwingine tena aliye hai? Ni ngumu.

Namshauri huyo mkewe asepe tu mapema kabla siku ya hiyo plan kuwa vitendo.

Otherwise mniambie mchizi kaongea tu hivyo mbele ya TV kufurahisha Umma
 
Kwa sasa ni rahisi kusema utasamehe au hutosamehe, lakini likikutokea ndo utaona ugumu wa jibu lako
 
Back
Top Bottom