Haka kadude kaliwahi kukuachia historia gani ambayo hautakuja kuisahau maishani mwako?

Haka kadude kaliwahi kukuachia historia gani ambayo hautakuja kuisahau maishani mwako?

Boarding school hiyo, mwanangu mmoja alipewa kachumba kama kiongozi wa ulinzi, so tukawa tunatumia hii kitu kuchemsha mahindi humo kwenye kichumba. Ipo siku kilipiga shot mpaka nyaya za umeme kwenye kile kichumba zikawaka moto. Ilikuwa tafrani ndo ikawa mwisho kuchemsha mahindi.😂😂
Nimesoma huu Uzi,kuungua Kwa mabweni,Kuna sababishwa na wanafunzi.
 
Alinunua mama
kipindi cha baridi yeye ndio alikua anatumia kupashia maji kwenye ndoo
Sisi watoto alitukataza

Sasa mimi siku hiyo mama hakuepo nadhani ilikua 2013 kama sikosei 🤣

Nikaweka maji kwenye ndoo nikadumbukiza hiyo heater
Baadae kidogo nikataka kujua kama maji yamepata moto nikadumbukiza vidole Alooooooooooooooooo nilitetemeshwa sitakaa nisahau maisha yangu yote

Na mpka leo sivutiwi wala sipendi kuoga maji ya moto umenikumbusha mbali sana mkuu
 
Unafahamu heater ya umma mbili wewe huko sekondari? Nikikumbuka hiki kisanga, ngoja ninyamaze
Sisi tulikuwa tunajitengenezea wenyewe hizo heater. Ila ukikutwa ma shule ndiyo basi. Yaani ni asi na chanya ndani ya maji, hatari na nusu
 
Alinunua mama
kipindi cha baridi yeye ndio alikua anatumia kupashia maji kwenye ndoo
Sisi watoto alitukataza

Sasa mimi siku hiyo mama hakuepo nadhani ilikua 2013 kama sikosei 🤣

Nikaweka maji kwenye ndoo nikadumbukiza hiyo heater
Baadae kidogo nikataka kujua kama maji yamepata moto nikadumbukiza vidole Alooooooooooooooooo nilitetemeshwa sitakaa nisahau maisha yangu yote

Na mpka leo sivutiwi wala sipendi kuoga maji ya moto umenikumbusha mbali sana mkuu
Kiranga kikaisha hapo hapo🤣
 
Sisi tulikuwa tunajitengenezea wenyewe hizo heater. Ila ukikutwa ma shule ndiyo basi. Yaani ni asi na chanya ndani ya maji, hatari na nusu
Uma (fork) mbili au vijiko viwili au tulitumia spring za vitanda vya vyuma kutengeneza heater ya mchongo mabwenini boarding school.
Mungu mkubwa hatujafa Wala hatujachoma mabweni.
 
Niliingiza mkono ktk ndoo ya maji ili kupima joto wakati nachemshia hiyo heater. Kilichotokea sitasahau
 
Back
Top Bottom