Haka kamjengo kanaweza kugharimu shilingi Ngapi?

Haka kamjengo kanaweza kugharimu shilingi Ngapi?

Samahani wakuu, kwa wale wenye uzoefu na mambo ya ujenzi, je? Haka kamjengo kanaweza kugharimu sh. Ngapi hadi kanaisha?
View attachment 872767View attachment 872768

ukiweza kuweka vipimo ata roughly, wakuu wataweza kukadiria vizuri zaidi. na partitions za ndani zikoje?
japo kwa macho imekaa kama mita 6 kwa 3 jumla.. ujenzi halisi itakua kati ya 5-7mil. haiwezi kua chini ya 3. na ikizidi 8 umepigwa.
 
Mkuu tuchukulie ndani hakujasakafiwa wala rangi haijapigwa. Kifupi nataka nijenge kibanda cha kijana nitake muweka site mkuu
 
Mkuu umejibu ukiwa na usingizi
Yupo sahihi sana. Nimejenga kubwa ya hapo kwa 1.5m ila kuezeka nikapiga "slope" kama wengi wanavyoita ya mita 3x9. Makadirio mengi ya watu hapa ni nadharia tuu. Kwenye ujenzi unaweza tishwa hadi ukaogopa kuanza. Unamuuliza mtu nyumba yako hii umejenga kwa sh ngapi anakwambia million 150 kumbe hata 30m haifiki.
 
Ukisimamia ujenzi mwenyewe milion 3 zinatosha.

Kama unamtumia fundi pesa ananunua material yeye andaa miluon 4 mpaka 4.5
 
Hapo ni chumba na sebule, max ni tofali 1000 kuanzia msingi hadi juu, bati sita kila upande jumla 12, milango miwili, madirisha mawili, mbao 4×2 sita na 2×2 nane, mchanga Lori na kokoto nusu lori, cement mifuko 20, vitasa viwili, komeo mbili za ndani, misumari ya bati kilo2 na ya 4" kilo2, bawaba za milango 6, mafuta gharama yà kila kimoja hapo jumlisha usisahau hela ya fundi sijui vinasimamia ngapi vitu hivyo
Kwa mwonekano wa hako kadirisha inaelekea kuna choo humo ndani... Afu umesahau nondo hapo.
 
Back
Top Bottom