Haki mwa Milengo ya Jinsia - Asha Rose Migiro sijamuelewa

Haki mwa Milengo ya Jinsia - Asha Rose Migiro sijamuelewa

kibananhukhu

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2009
Posts
366
Reaction score
163
Akiongea kwa hisia, akionesha kuwa kama siyo "Gender" wanawake ndo basi, kanikatisha tamaa. Nilikuwa ninamfikiria ni shupavu, mwenye uwezo wa kushika wadhifa wowote nchini kwa uwezo wake, Mhe. Asha Rose Migiro amenikatisha sana tamaa jinsi alivyokomalia wanaweke wabebwe.

Kuna wanaweke wenye uwezo hata wa kuwa maraisi bila kubebwa, kwa nini Asha haoneshi kujiamini kwa hilo? Ni kweli wanawake watanzania hawana uwezo wa hata kugombea naafasi tu za uongozi wa Bunge. Hali hii haitatufikisha mahali pa kusema kuwa kama kipindi hiki Rais ni Mwanaume kipindi kijacho raisi awe Mwanamke?

Asha rose aliongoza kampeni za kutaka kama Mwenyeki wa Bunge akitoka bara, makamu awe mwanamke na kama mwenyekiti akitoka Visiwani Makamu awe mwanamke.

Nadhani hii haina tofauti na viti maalum ambavyo katika katiba mpya havipo au vimeboreshwa kwa kuwafanya akina mama wagombee. Hoja hii haikuwa ya kutetewa na Migiro.
 
Nadhani hutaweza kumuelewa kama alivyoshindwa Mzee Kimoon.
Endelea kumfuatilia sio ajabu ukasikia akisema kuwa Tanzania nayo ipewe upendeleo kwenye tuzo za Oscar ili nasi tumpate Lupita wetu!
 
Hata jana Asha-Rose alipigwa kijembe na mwalimu Oluoch, kwamba mtu anajidai kuwa na PhD ya sheria halafu anatoa hoja isiyo na tija kwa kung'ang'ania eti kanuni lazima ziandikwe kwa mtiririko zieleweke, wakati uandishi wa sheria unaweza ukafanyika vyovyote tu ili mradi mtu azisome zote na anaweza kuzisoma sambamba kwa kurejea mahali popote zilipo!
 
Kweli Tz ni vituko. Hivi tutakuchaguaje kwa jinsia? Leo hii tunapambana 50/50 Afrika, nenda kwao walio tuletea mambo haya kama wanafanya hivi tunavyo fanya. Hakuna kitu kama hicho.

Wanawake ni kupata elimu hili kuweza kupambana na mazingira sio kupewa upendeleo tu kisa mwanamke. HIvi wabunge kina mama bungeni tangia waingie hadi leo hii wamepigania haki gani katika jamii kama kuzuia kabisa wajawazito na watoto kufariki? Nenda hospitalini ndio balaa hakuna vifaa, madawa, wao wapo tu. Nenda shuleni hasa za msingi bado watoto wanakaa chini lakini wao wapo wanasema haki sawa kweli? Leo hii hatuoni muungano wao kama kina mama kupambana na rushwa katika nchi yetu kweli?

Nina imani kubwa sana kama wakina mama wakiamua kuwa wamoja bila kujali vyama vyao, Tanzania mabadiliko ya kweli yatatokea. Angalia familia nyingi kama mama atakuwa na msimamo mzuri wa maadili watoto watasonga mbele hata kama baba atakuwa sio mwadilifu.
 
Huyu mama kwa kupokea kwake tu hizi teuzi alizopewa kaonyesha jinsi asivyo na uwezo kiakili.
 
Huyu anajisumbua tu na hatapata huo uraisi
 
Vichwa vipo kibao asee ila havijaingia katika siasa sababu kama hizo za kusema ili ushangiliwe!!!!!!!
 
Kuna clip ya Mugabe interview prior to 90 yrs birthday part 3 kama sikosei, yeye kasema kwa wanawake hakuna quality so hawezi kutoa madaraka kwa sababu mtu ni mwanamke, he have to know who is behind that skirt or gown, usa na uk je wametimiza hiyo 50/50 na ndio walio endelea kuliko sisi.
 
Vichwa vipo kibao asee ila havijaingia katika siasa sababu kama hizo za kusema ili ushangiliwe!!!!!!!
Hata hivyo vichwa unavyovisemea mkuu havijaingia huko kwa sababu havijiamini katika sera ya ushindani, period!! Vinasubiria viti vya upendeleo wa kutumia shimo!! Wanawake bure kabisa, ujasiri wa kushindana hawana, wabaki tu kuwa wasaidizi wetu kama walivyoumbwa tangu enzi ya Adam na Eva!! Mwanamama hata awe na PhD 10 (kama zipo) utakuta anagaragazwa na darasa la saba au form IV failure!!

Sasa eti watu nao walikuwa wanamwona Asha-Rose kuwa mgombea sahihi wa u-Rais?? Ataweza wapi kushindana huyu? Labda nako tupitishe sheria ya Jinsia (kuwa 2015 ni zamu ya wanawake). Mama huyu dhaifu sana sijui kwa nini bwana!!
 
Uko njia potofu saaana ila pia inaonesha jinsi gani unaichukulia dunia na maisha kwa ujumla!!!!!!

Jua wapo wanawake katika nafasi za utendaji wana akili kuliko wanaume wengi sana, wana busara na wanaweza kufanya mambo yakaonekana na kukubalika ila tu hawaingii huko sababu ya mfumo unaotaka akili yako kuongozwa kwa matakwa ya chama au kundi fulani, hawa huwezi wakuta karibu na siasa!!!!!

Kwenye hili tukubali kutofautiana mapema kabisa; wapo wanawake vichwa sana tuuu!!!!!!!!!

Ngoja nikuitie wachache hapa gfsonwin, AshaDii, Kaunga, Ennie, Heaven on Earth, Karucee, Kongosho, Preta, King'asti, Evelyn Salt majina yanagoma hebu anza na hawa kuwaeleimisha kuwa wao wanategemea mashimo wao ni bure na hawawezi ushindani!!!!!
 
Last edited by a moderator:

Wanawake hoyeeee.
 
Mwishowe atakuja kutoa hoja jamani 2015 rais mwanaume,2020 mwanamke. Kwa rekodi yeye ubunge wake wa kuteuliwa tena na rais
 
Back
Top Bottom