Haki: Ni heri kumsamehe mwenye makosa kuliko kumuadhibu asiye na hatia

Haki: Ni heri kumsamehe mwenye makosa kuliko kumuadhibu asiye na hatia

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,186
Reaction score
7,492
Katika utoaji haki kuna njiapanda mbili zinaweza kujitokeza.

Moja ni uwezekano wa kumuadhibu, kumdhuru au kumuumiza mtu asiyekuwa na hatia amma kwa makusudi au kwa kudhani bila ya kuwa na ushahidi.

Mbili ni uwezekano wa kumsamehe au kumuachia huru mkosaji kwa kutokuwa na ushahidi wa kutosha.

Binadamu mwenye hekima, anapojikuta katika njia panda ya namna hiyo, ni heri kuchagua njia ya pili kwa kuwa moja ya visababishi vya mikosi, ni kuhukumu na kuwaumiza wasio na hatia.

Ni kwa mantiki hiyo, mamlaka zinapaswa zitizame upya utaratibu wa kukamata watu na kuwaweka ndani halafu ndio wakatafuta ushahidi, na kinyume chake wawe na ushahidi ndio wakamate mtu. Vinginevo kunaweza kuwa na dhulma nyingi ambazo matokeo yake ni mikosi mtambuka.
 
Back
Top Bottom