Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kama wanaume wangekuwa waadilifu, wenye Haki, upendo, Akili na kupenda UKWELI. Ni wazi Wala tusingekuwa na vuguvugu na harakati za kumkomboa Mwanamke, sijui Haki za Wanawake. Kusingekuwa na mambo ya women empowerment.
Lakini baada ya wanaume wengi na Wala sisemi wote. Wakageukia dhulma, ukatili, unyanyasaji, ushenzi na kujipendelea kuliko pitiliza hii imepelekea mambo tuyaonayo hivi Leo.
Sijasema, wanawake wote ni Wema. Ila ninahakika kuwa Wanawake wengi kama wangetendewa Haki wangekuwa zawadi iliyokusudiwa kwa Sisi Wanaume.
Watibeli na wanaume wote wenye Akili, Haki, upendo na wapenda KWELI yote tunajua kuwa Wanawake ni viumbe Kamili vyenye Haki yna Uhuru wa kujiamulia mambo Yao. Sisi wanaume sio wamiliki WA Wanawake. Na Wala wao wanawake sio wamiliki wetu.
Kuoa mwanamke hakukufanyi ummiliki huyo mwanamke. Na Kuolewa na mwanaume hakukufanyi ummiliki huyo mwanaume. Sisi Watibeli tunajua kuwa mtu hamilikiwi.
Ni kosa na dhulma kummiliki mtu Kwa sababu huko ni kumkosea Haki zake. Na watu wasio na upendo ndio hufanya hayo.
Mtu ni kiumbe Huru. Tangu mwanzo Watibeli wanajua UTU ni nini. Ndio maana haununuliwi. Sio ajabu WATIBELI hatutoi Mahari Wala Binti zetu hawatolewi MAHARI kwa Sababu tunajua fika huo ni unyonyaji, ukatili na dhulma, matusi na dhihaka kwa kiumbe Chenye hadhi ya kuwa MTU.
Umiliki ndio chanzo cha yote haya. Utumwa, ukatili, ukandamizaji na dhulma. Ule mtazamo wa kufikiri Mkeo unammiliki ndio chanzo cha ukatili wenyewe.
Matokeo yake utajiona unahaki zaidi yake. Upo juu yake. Na unaweza kumuamulia Jambo lolote hata kama ni Baya na linalomuumiza.
Taikon Master mara zote nimekuwa nikiwaambia Wanawake wafanye Kazi na kuzuia wanaume kutokuhonga na wanawake wasipende kupewapewa vitu burebure kwani huo sio UTU.
Mtu hauruhusu vitu vya burebure. Huko ni kujidhalilisha na kufungua Mlango wa kumilikiwa.
Mtu hawezi kukumiliki kama humtegemei.
Mtu hawezi kukumiliki kama haupokei vitu kutoka kwake burebure.
Kufikia hapo, utagundua maisha ni ya Mtu mwenyewe. Na Hilo ili litimie Basi mtu huyo itampasa ajitegemee kwa kufanya Kazi na kuweza kujilisha na kujitunza.
Maelezo yote hapo juu yanaeleza msingi Mkuu wa wanaume wengi kuwa Wakatili na wenye kudhulumu kutokana na wanawake kushindwa kujitegemea kwa kufanya Kazi Zao za uzalishaji ili wajimudu kimaisha bila kumtegemea yeyote Yule.
Ikafikia wakati wanaume ili waendelee kuwaonea wanawake wakawazuia baadhi ya mambo nyeti katika maisha kama kumiliki Mali muhimu kama ardhi na Kupata Elimu.
Kuwanyima Kupata Urithi na kutengeneza dhana bandia ya kikandamizaji kuwa mwanamke awe nyumbani kama Mtu wa kuhudumiwa.
Mapokeo hayo ambayo sio ya Asili, yakafanyika kuwa Sheria na wengi wakaona ni Asili ya mwanamke kuhudumiwa jambo ambalo Halina ukweli wowote. Ni mapokeo tuu.
Sheria ya 50*50 ni muhimu kwa Jamii zenye utapeli. Watibeli tunaiunga Mkono Sheria hizo ingawaje kwenye ulimwengu wa watibeli Sheria hiyo haifanyi Kazi kwa Sababu Sisi Watibeli wanawake zetu ni WATU.
Hawakuwahi kuuzwa Wala kununuliwa. Hawakuwahi kuwa Watumwa. Hivyo hawahitaji kujikomboa kutoka kwa yeyote.
Ni Sheria ya 50*50 ndio inalenga kuwakomboa wale wanawake waliokuwa Watumwa na Mateka wa wanaume katili na wenye dhulma.
Hata hivyo Taikon Master, ninashangaa watunzi wa Sheria hizo wanarudia kosa lilelile walilolifanya watunzi wa sheria za mfumo Dume kandamizi. Kwani Sheria ya 50*50 inawapendelea zaidi Wanawake na kuwaonea kiwango Fulani wanaume.
Jambo ambalo linafanya sheria hiyo ya 50*50 kuwa Sheria ya dhulma na katili na kandamizi kwa Wanaume.
Tunatarajia kuwa ikiwa Sheria 50*50 itafanya Kazi. Kama wanaume na wanawake wanafursa Sawa katika Ajira na malipo ya Mwanaume na mwanamke ni Sawa kama wapo level Moja. Tunatarajia kwenye majukumu ya kifamilia pia kuwe na ule usawa.
Sasa wote wanalipwa mshahara kwa Sheria ya 50*50 lakini kuna Sheria kandamizi inayomlazimisha mwanaume kutunza familia kilazima. Huo ni Utapeli.
Sisi Watibeli tunabaki kuwacheka tuu tunajua ni Sheria za kishetani kwa Sababu hazina AKILI, hazina upendo, Wala Haki na hazizingatii UKWELI.
Acha nikalale
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam