Haki ya Dhamana kwa Mtuhumiwa na maana yake

Haki ya Dhamana kwa Mtuhumiwa na maana yake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Dhamana ni haki inayopata msingi wake katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ambayo ina dhana inayotamka kwamba mtu hatochukuliwa kuwa mwenye hatia mpaka tuhuma zithibitishwe dhidi yake, Ibara ya 13(6) (b).

Ili kuzingatia dhana hii ni muhimu kumruhusu mtuhumiwa kwa kumpa dhamana apate kuwa nje ya kizuizi mpaka hapo tuhuma zake zitakapothibitishwa na Mahakama.

Kwa mantiki hiyo, dhamana ni haki ya mtuhumiwa na wala sio upendeleo au zawadi kwake.

Nani anayetoa dhamana?
Dhamana inaweza kutolewa na Jaji au Hakimu; hali kadhalika Mkuu wa Kituo cha Polisi, ambako mtuhumiwa anashikiliwa.

Hata hivyo, yapo baadhi ya makosa ambayo kisheria hayaruhusu dhamana kutolewa, kama yafuatayo:

Kosa la kuua kwa kukusudia; Kosa la uhaini; Kosa la unyang’anyi kwa kutumia silaha; Kosa la ugaidi; na Kosa la kunajisi; na kadhalika.

Kifungu cha 148(5) (a) – (e) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1985.

Hali kadhalika, mtuhumiwa anaweza kukosa dhamana kutokana na mazingira kadhaa kama yafuatayo: Endapo mtuhumiwa alishapewa dhamana, akakiuka masharti aliyopewa; Kwa minajili ya usalama wa mtuhumiwa mwenyewe; usalama wa jamii; Kwa kuchelea kumwachia nafasi ya kuvuruga/kuharibu upelelezi; na sababu nyingine, yoyote ya msingi kisheria na kiusalama, kama atakavyoona mkuu wa kituo.

Aina za Dhamana
Dhamana zipo za aina kadhaa kama zifuatazo:
Dhamana ya Mkataba wa Maandishi: Huu ni mkataba kati ya mtuhumiwa au mdhamini kujifunga kwamba, mtuhumiwa atahudhuria Baraza la Mahakama siku iliyotajwa. Iwapo mtuhumiwa asipotokea mdhamini huyo atalazimika kutekeleza masharti fulani au hata kifungo.

Dhamana ya Mali: Iwapo mtu hana kiasi cha fedha, anaweza kuweka dhamana kwa kukabidhi mali zake zinazohamishika.

Dhamana ya kutambuliwa: Aina hii ya dhamana humtaka mtuhumiwa au mdhamini kuweka sahihi ikiwa masharti ya mkataba wa dhamana yamevunjwa. Aina hii huonekana kama yenye unafuu kidogo.

Dhamana ya kuweka fedha:
Hii ni aina ya dhamana ambayo mtuhumiwa, rafiki au ndugu hutakiwa kutoa kiwango fulani cha fedha na iwapo hatahudhuria Mahakamani fedha hiyo hutaifishwa na Serikali.

Nani anaweza kuomba dhamana?
Mshtakiwa, ndugu au rafiki wa mshtakiwa, pamoja na wakili wa mshitakiwa.

Wakati wa kuomba dhamana:
Muda wowote wakati kesi inaendelea na wakati rufaa ikisubiriwa; Wakati mashtaka yanaandaliwa na polisi au kabla ya hukumu kutolewa au rufaa kuamuliwa.

Kukataliwa au Kunyimwa Dhamana
Kifungo cha 67 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1985 kinaeleza kwamba, mtuhumiwa aliye chini ya ulinzi wa Polisi anaweza kukataliwa maombi yake ya kutaka apewe dhamana.

Hii ni kwa kuzingatia masuala kama vile, Polisi kujiridhisha kwamba mtuhumiwa atatimiza masharti ya dhamana atakayopewa, ikiwamo kufika siku na saa atakayoamriwa.

Zaidi, kujua makazi, ndugu na jamaa, ajira na hata ikibidi hali ya maisha ya mtuhumiwa na familia yake, kumbukumbu za kihalifu kama zipo.

Kufutwa kwa Dhamana
Baada ya mtuhumiwa kupewa dhamana ya Polisi inakuwa huru, dhamana hiyo inaweza kufutwa na mkuu wa kituo cha Polisi, chini ya Kifungu cha 68 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1985. Baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha uamuzi wa kufuta dhamanani:

Kubainika kwamba mtuhumiwa anapanga mipango ya kutoroka; na/au

Kwa makusudi anakiuka au yuko karibu kukiu kama sharti ya dhamana

Adhabu kwa Kukiuka Masharti ya Dhamana

Dhamana inayotolewa na Polisi kwa mtuhumiwa anayekabiliwa na kosa la jinai inapaswa kuheshimiwa. Kifungu cha 69 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1985 kinaelekeza adhabu kali kwa mtuhumiwa na mdhamini au wadhamini wanapokiuka masharti ya dhama na waliopewa.


Muhimu
Dhamana inatolewa bure, hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana.

Jambo la msingi ni mtuhumiwa kuomba apewe dhamana na kutimizaji taratibu kwa muijibu wa sheria.

Ni muhimu mtuhumiwa kuwa nje kwa dhamana, ili aweze kujiandaa kukabiliana na tuhuma zinazomkabili kabla ya hajafikishwa mahakamani, mfano kupata msaada wa kisheria.

Mwisho kabisa, kwa kumalizia, dhamana ni haki ya kikatiba ya kila mtuhumiwa, kwa hiyo mtuhumiwa ana haki ya kuomba dhamana wakati wowote kabla hajapatikana na hatia au baada ya kukata rufani kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yake.

Pia dhamana ya polisi haihusishi fedha taslimu, hutolewa bure. Ni kosa kwa askari polisi kupokea fedha/rushwa katika zoezi la utoaji wa dhamana na katika utendaji kazi wake.
 
ndiyo kama ni mtu maarufu au kama anashtakiwa kwa makosa ya kifedha mfano wizi wa fedha anaweza kulipa kiasi anachotuhumiwa kuiba kama dhamana pia
Hivi mtuhumiwa anaweza kunidhamini yeye mwenyewe?
 
Je,mtuhumiwa anaweza kumshitaki aliyemtuhumu kabla kesi yake hajasikilizwa?

Mfano umshitaki mtu polisi au kama ni mtumishi kwa mamlaka yake ya nidhamu alafu yeye akushtaki mahakamani before kesi ya kwanza kusikilizwa?
 
Back
Top Bottom