Ndugu zangu Watanzania wenzangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,Nawasalimu kwa dhati.Pia nawapa pole wote waliotangulia mbele ya Muumba wao kwa vifo vya kinyama vilivyotokea.Mungu awape ujasiri wafiwa.
Pia bila kuwasahau wagonjwa, wafungwa & mahabusu (Hakuna aliye salama sana).
Nikirejea mada hapo juu; Ukisikiliza minong'ono na mijadala ya wazi au mitandaoni,unagundua kuwa vilio vimezidi.Mifano ipo mingi maana kuna vilio vya Uchumi mgumu,Tozo zilizokithiri,mauaji na utekaji wa Wananchi wenzetu.
Sakata la Serengeti limeniogopesha sana. Walianza na wanasiasa, wafanyabiashara, wasanii, Wamasai wa Ngorongoro na sasa ni zamu ya Panya Road, Majambazi na Udhalilishaji wa wanawake au wanaume.
Maovu haya yanaelekezwa zaidi kwa Serikali, POLISI na watawala wa CCM. Hofu ni kubwa mno.
Je, haya yamebarikiwa hapa Tanganyika? Je, nani wa kuwajibika kuhusu madhila haya?
Tudai Katiba Mpya ya Wananchi ili tuikomboe nchi yetu isiingie machafukoni.
Mwenye macho....