Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
HAKI YA USAWA WA KIKATIBA.
Ibara ya 12 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema binadamu wote ni sawa na kiila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
Kila mtu anayo haki ya kupata heshima na thamani inayostahili utu wake.
Ibara ya 13 inasema watu wote ni sawa mbele ya sheria. Kila mtu ana haki ya kulindwa na kupata haki sawa kwa mujibu wa sheria bila ya ubaguzi wowote.
Kwa mujibu wa ibara hizi, hakuna binadamu anayetakiwa kuonekana bora zaidi kuliko mwingine au kuwa na haki zaidi ya mwingine.
Kama ni haki ya kupata huduma fulani basi watu wote wanatakiwa kuipata huduma hiyo. Kama ni kuwajibika mbele ya sheria kwa kosa fulani basi wote wanatakiwa kuwajibika kwa kosa hilo.
Kutenda vinginevyo ni ukiukwaji wa haki ya usawa na ni kutaka kuonesha kuwa kuna binadamu ambao wao ni bora kuliko wengine.
Instagram: @tanzania_lawyers_forum
Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓