Haki ya watoto wa nje ya ndoa kurithi mali

Joined
Sep 17, 2014
Posts
5
Reaction score
1
Kutokana na sheria za mirathi za kila aina tukianza na ile ya India ya mwaka 1885 na sheria za kimila pamoja na sheria za Kiislaam hazimpi mtoto wa nje ya ndoa uhalali wa kurithi mali.

Maoni yangu ni kwamba kwa kua watoto hawana makosa na wanaachwa katika mazingira magumu hauoni kwmba wakat umefika izo sheria zirekebishwe na uwepo utartibu ambao utamwezesha huyu mtto kupata angalau asilimia fulani ya mali ya marehemu.

Wewe unasemaje?
 
Sheria ya Islamic, inaruhusu watoto nje ya wedlock kupata urithi wa 1/3 ya mali za marehemu endapo aliandika will.
 

Inaonekana kama uko first year tulia na usome vizuri hizo sheria! Pia usisahau sheria za kimila na sheria ya mtoto
 
Kama umesoma islamic law, tofauti kubwa kati ya sheria za kiislam na sheria hiz za nchi na za kimila ni kwamba,
(1)sheria za kiislam ni maamrisho ya mungu
(2) hivyo sheria za kiislam hazifanyiw amendment na binadamu
kuhusu mtoto wa nje uislam hamkandamiz huyo mtoto na umeonya wagawa urithi kwenda kinyume na maamrisho hayo na kujifanya wana huruma kuliko sheria ya kiislam kwa kumpa urithi usiomhusu.
MTOTO WA NJE YA NDOA ANAPATA NINI?
sheria za kiislam mtoto wa nje ya ndoa hamrithi baba bali humrithi mama, hivyo urithi wake uko kwa mama yake.
ama baba yake akitaka asimwache hiv hiv bas ampe hicho kitu au sehem ya mali akiwa hai kabla baba hajafa inakubalika, lkn akifa tu baba huyo mtoto hatapata kitu.
SULUHISHO
ni kuacha zinaa kabla ndoa na kuepuka michepuko kwan hakuna amendment itayofanywa na binadam ktk islamic law, kufanya hivyo kidin ni kuacha amri za mungu na kuingiza fikra za kibinadam jambo ambalo haliwez kubalika
 

Ok, ulicho kisema Ni sahihi, ila kuna vitu viwili we must consider
1. Sheria ya kiislam Ni moja ya sheria ambazo naziheshemu kuwa very perfect linapokuja swala la mirathi , maana inatoa jinsi gani Mali zinaweza kugawanya.
(i). Baba anaruhusiwa kugawa 1/3 ya Mirathi yake kwa mtu yoyote yule, wakati 2/3 ndio inakwenda kwa warithi halali(mgao wa Quran ). This is according to Surah Nisa of the holy Quran,
(ii) kama hajaandika urithi hapo ndipo penye tatizo maana hao watoto hawataweza kupata chochote.
2. Kwahiyo inadepend na swala la kuandika will, NOTE. Quran inasisitiza sana watu kuandika urithi.
 
Sheria ya Kiislamu SIO maamrisho ya Mungu, ila watu fulani wanaamini kuwa ni maamrisho ya Mungu.
 
Hyo sheria ya India sio 1885, ni mwaka 1865 ambyo ni applicable tanzania....
The position of illegal children over succeeding the deceased estate through interstate from the legal provisions of Indian Succession Act and Customary Laws tend to go against the current trend of human rights. in considering the amendments, to my side it will be very difficult as the customary rules comes from different tribal customs in Tanzania which stands as the trditional recognitions throught the tribes sasa in changing them it will be difficult as itabidi kuconsult all tribes in Tanzania ukizingatia na kukumbuka kwmba Customary declaration imetokana na common norms and rules za tribes nyingi zinazofanana.
Ukija kwa upande wa Indian Succession Act, i think the law is clear as to exlude the illegal children na ukiangalia hii ni provision inayoumiza vichwa watu wngi. Katika kiapo cha ndoa, kwa upande wa wakristo yapaswa kuwa na mke au mume mmoja say ndoa yko iwe ya kisheria au ya kidini. From that simple provision, going against that general rule inakuwa ni illegality. Though exception ya hyo n kwmba hyu mtoto anaweza kurithi mali km ataandikwa kama mrithi kwnye wosia au km wazazi wote wawili wamekubaliana kuishi na kumtunza huyu mtoto.
All in all, hyu mtoto aliye nje ya ndoa atarithi mali toka kwa mama yake na si kwa baba yake in case of intestacy.:A S check_03:
 
waweka sheria hizi walikuwa na agenda zao. Yaani mtotot wa kwangu, mali nimetafuta mimi. Ninarithisha nitakavyo mimi. Eti apate moja ya tatu, mtoto wangu!!!! labda kama nilisingiziwa, Sheria zingine kama hizi ni kandamizi. Eti atapata kwa mama yake, kwani alimpata huyo mtoto akiwa pekee yake. Tuache unyanyasaji kwa watoto, jamani
 

Bwana mwakaboko, kuna njia nyingi za kumrithisha mtoto wa nje ya ndoa zaidi ya 1/3 hata kama wewe ni muislamu. The only thing is to consult a lawyer.
 
Bwana mwakaboko, kuna njia nyingi za kumrithisha mtoto wa nje ya ndoa zaidi ya 1/3 hata kama wewe ni muislamu. The only thing is to consult a lawyer.
Tuwe wakweli kuna mtoto anayepatikana kwa bahati mbaya!!!!! Sasa mtu unafanya mapenzi bila kizuia mimba/kondomu, unatarajia nini zaidi ya mimba!!! Kusema kuwa kuna utaratibu, huo utaratibu anapanga mtafutaji sio mtoto. Baba lazima sio ombi uweke mazingira mazuri kwa ajili ya watoto wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…