Roya Roy, kwanza tuanze na mjane kama mjane kabla hajaolewa tena manaake kama akiolewa tena huyo si mjane ni mwanandoa kama walivyo wengine. Mjane wa kike kama walivyowajane wengine anazo haki katika ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka,1971. Anayo haki ya kuendelea kutumia jina na mume wake(right to surname),anayohaki ya kuishi kwenye nyumba ya marehemu mume wake,kuiangalia na kuwatunza watoto na mali za marehemu kwa niaba yao,Vile vile yeye kama warithi wengine ana haki ya kupata mgao wa mali toka kwa mumewe kwa matumizi yake yeye(si kama mwangalizi wa familia) kwa kuwa katika hiyo mali ya mumewe yeye pia amechangia upatikanaji wake.Hapa watu watasema hapana hiyo haki ni ya wakati wa talaka tu,hapana hiyo ni termination right,kwa kuwa talaka inafanya ndoa iterminate na kifo pia vilevile.
Haki ya mjane huyu si asilimia 50 kwa hamsini,kwanza inategemea ushiriki wake katika kuchuma,na pia hata wosia aliouacha marehemu.Sehemu hii kwa kawaida huwa ina utata sana hasa pale marehemu ambapo hakumtaja kabisa mkewe kuwa mrithi lakini hata hivyo wosia huo huwa hauna nguvu kama haukushuhdiwa na watu wawili,na au haukusajiliwa.kikubwa na kushuhudiwa na mwenye kuandika awe wakati anaandika alikuwa na akili timamu.Hata hivyo kisheria unaweza kuchallenge wosia hasa kama hakukuwa na sababu za msingi za kukutenga.
Mjane huyu akiwa msimamizi wa mirathi cheo hicho si milele kinaisha pale akishamaliza kugawa mali zote na kukabidhi orodha ya ugawaji wake mahakamani(inventory).baada ya hapo akiolewa endapo alikuwa akiishi kwenye nyumba ya watoto anaondoka kwenye ile nyumba na kwenda kwa mumewe na kama ilikuwa ni nyumba alioirithi bado atakuwa na haki ya kuendelea kuishi kwenye hiyo nyumba.
Kwa leo ngoja tuishie hapa