HakiElimu vs Govt: The saga

Akitoa mfano, Ndugai alisema kuwa hali inayofanana na hii, iliwahi kutokea huko Zambia miaka kadhaa iliyopita na kusababisha serikali iliyokuwa madarakani kung'olewa

kumbe shida ni kuogopa kung'olewa madarakani???
 
kaitwa au kapata ajali mbaya sana wakati anaelekea jimboni kwake... Namtakia maisha marefu
 
Jamani, Hili la HAKIELIMU na "sirikali" sasa limezidi. Gazeti la Tanzania Daima la jana Oct 23, limeituhumu HAKIELIMU kwa kutoa matangazo ya kiuchochezi kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Mwandishi Salehe Muhamed, amemnukuu Naibu waziri wa wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto, akisema "serikali haiwezi kuvumilia matangazo yanayotolewa na Hakielimu na tunawaonya waache kwani yanaleta chuki ndani ya jamii...." mafano alioutoa naibu waziri huyo ni lile tangazo linalohusu wizi wa fedha za EPA.

Nafikiri waziri amekurupuka, kwani kama angefikiri zaidi kabla ya kutoa vitisho angegundua yafuatayo:
1. watoto wa shule hao na jamii kwa ujumla wameshaichukia serikali kwa ajili ya mafisadi wanaoiongoza. Watoto wa shule waliwahi kuandamana wakiwa wameshika mabango yanayomuomba raisi kujiuzulu. Si tangazo la hakielimu lililowachochea bali ni hali halisi.
2. migomo katika secta mbalimbali katika nchi nzima (wafanya kazi wa NMB, walimu waimbao nyimbo za kukitukuza chama cha CHADEMA, na viashiria vingi vya mpasuko wa kisiasa ndani ya chama tawala, havijafichwa kwa watoto wetu. watoto wetu wanajua majina ya mafisadi wa nchi hii. ufisadi imekuwa ndo harufu ya nchi nzima. Si tangazo la hakielimu lililowachochea bali ni hali halisi.
3. Ni ukweli usiopingika mbinguni na duniani kuwa 133b zingeweza kufanya mambo makubwa kwa kuboresha viwango vya elimu Tanzania. Si tangazo la hakielimu lililowachochea bali ni hali halisi. Namshauri Dr Nkya aache siasa afanye kweli kama anaipenda chichi yake kwa sababu Si tangazo la hakielimu lililowachochea bali ni hali halisi.
4. Namshauri Dr Nkya asubiri October 31, aone mabo yatakavyokuwa kwa nchi hii kama mafisadi hawatashughulikiwa.
 
Kama Nkya alikosea atajaza mwenyewe. sisi tunafahamu kuwa yeye ni mwakilisi wa serikali. Nawatia moyo Hakielimu kuendeleza mapambano dhidi ya mafisadi.
 
Nashangaa HakiElimu kwenye kimbembe hiki cha JK wapo kimya, wakati wa Mzee Ben walimpeleka mbio sana Mungai hawa....
 
Wadau nauliza mwenye ufahamu wa hali halisi ya HakiElimu maana imekuwa ghafla mno kutoweka ktk masikio ya watanzania... Au vita ya mafisadi imewakimbiza pia? Nimepata data kwamba mkurugenzi mwanzilishi wa HakiElimu sasa yupo ktk shirika jipya liitwalo TWAWEZA. Je ina maana HakiElimu ilikuwa inategemea uwepo wa Rakesh Rajani au staff wake? 😕
Mwenye data amwage hapa
 
Rakeshi Rajani alishaondoka HAKI ELIMU akaja mkurugenzi mpya mwanamke ,jina limenitoka
 
Hakielimu is it a Non-Governmetal Individual [NGI) or Non-Governmetal Organisasation [NGO]?

TZ nyingi ni NGIs na ndo maana mara nyingi hazidumu!
 
hata mimi nashangaa, huyu rajani alifanya haki elimu ikawa juu, pengine kaondka na vyake na maana haki elimu imefika hapo.
 
Ngo nyingi si zinaendeshwa na wafadhili labda mambo ya muanguko wa uchumi duniani huo
 
Ukweli ni kwamba Rakesh Rajani, ni mtu ambaye yuko makini na ni mzalendo kweli. he was ready to push the boundary na alikuwa hatishiki hovyo, ingwa baadaye bodi yake pia ilimwambia asiwe confrontational, lakini hakuwa mwoga. Alisham-face down Mkapa na ubabe wake na Lowassa na ubabe wake! Huyu Dada Misokia ndo naona she is asleep at the wheel, hajui kazi yake ni nini na anataka kujionyesha kwamba anajua siasa kwa kuwa conciliatory. You never make a point by being meek and obedient especially if you aer an NGO.
Malengo ya HakiElimu ni nobel lakini currently it is lacking what our country generally lacks - LEADERSHIP!
 
Its simple,

RAJANI is a NATURAL BORN ACTIVIST, The new lady she is Carrier ACTIVIST..

omarilyas
 
Compa:

Hupo kwenye haki elimu pia. Hila achana na Ujamaa ni Imani. Vipi kazi za De Soto huko bongo? Ndio mna-implement Saccos? Na mamilioni ya JK?

Kamwe Mwafrika hataweza kuendelea bila kuwa na Imani yake mwenyewe ya kumwongoza kujiletea maendeleo yake mwenyewe. Na msingi wa maendeleo hayo ni Ujamaa. Hapana sipo HakiElimu. Ila bado nipo nipo katika kuwakubali.

De Soto yamemshinda. Alikuja na kutengeneza makabrasha kibao kuhusu taratibu zetu zisizo rasmi. Watanzania tukasema hayaelezei vizuri jamii yetu. Tukaunda timu yetu wenyewe. Sasa inatekeleza MKURABITA huko mikoani.

Hizo SACCOS na Mabilioni ya Bwana Fulani bado haziendani na De Soto. Huyo jamaa alikuwa anataka kutumia taratibu zetu zisizo rasmi kutengeneza mfumo wa utawala wa sheria utakautuwezesha kuendelea. Ila sisi bado Wajamaa!
 
Its simple,

RAJANI is a NATURAL BORN ACTIVIST, The new lady she is Carrier ACTIVIST..

omarilyas

Well! the work of Natural Born Activist won't be meaning full if there is no continuation of his work. I found it ironic, for him to make the public pay attention with Kayumba, make HakiElimu invisible with his departure. I think the beauty of starting anything, it to see it grow.

I wonder, if he natured anybody to take his role! He should have! I think our Madam is doing great; at least the organization is not bankruptcy. She will find her way!

Let’s stop praising individuals alone, let look into institution mechanism they left behind!
 

Think I sniffed something here...
Seems Rajan initiatives towards HAkiElim was for him-to-grow not for the organizational stabilty. Any clues pls?
But I have to ask... Was he involved with HakiElimu bankruptcy? where and when?
Wanabodi mnadhani HakiElimu inahitaji Backup au ndo let it be like those organization which met their fate naturally?
 
Its simple,

RAJANI is a NATURAL BORN ACTIVIST

So what, ndio HAKIELIMU ife because of his naturality........ Activists wako wengi mno hapa bongo siku hizi...nikupe mifano nenda TGNP, HAKIARDHI, LHRC, WLAC, LEAT etc...........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…