Wanajaribu kufanya kazi nzuri kukuza elimu lakini tungeanza na HakiElimu wenyewe. Ujumbe ulio mbele ya tovuti katika link hiyo unaonyesha Rajani amewaacha hali yao mahamumu.
Wanajieleza, "HakiElimu works to realize equity, quality, human rights and democracy in education." Lakini chapa lao linalopanda tovuti linasema "People Making Difference in Education and Democracy."
Kwa ujumbe wa chapa yake, taasisi imejinadi kama ni chombo cha kujihusisha na harakati za kukuza demokrasia na elimu, kitu kinachotofautiana na kile wanachokisema katika sentensi ya kwanza wanapo tambulisha malengo yao wakisema "...kutafuta kukua kwa demokrasia katika elimu." Big difference. Wanaweza wakakosa support ya watu ambao wanataka kukaa mbali na mambo yanayofanana na siasa kumbe lengo la taasisi ni kusaidia watoto wa shule, na sio siasa za demokrasia. Big difference.
Wakachemka zaidi. Kinachofuata baada ya hapo kinasema "HakiElimu's Vision is that every person in Tanzania is able to enjoy his or her right to basic quality education in schools that respect a person's dignity..." Ni nini hapo wanachosema wanataka ki respect a person's dignity? Ni right, ni education, ama ni schools? Kama ni right ama ni education ilibidi waseme "respects." Kama ni schools wanahitaji mpangilio mpya wa sentensi.
Huwezi ukajiita taasisi ya elimu halafu usitilie maanani, uvuruge, mpangilio wa sentensi na sarufi.
Huwezi ukachemsha hata kuandika propaganda ya mission statement! Mpaka kwenye kauli mbiu ya taasisi?!
Kauli mbiu inasema "People making difference..."! Making difference?