Hakika anajua kuwapa moyo fake wasanii wachanga

Hakika anajua kuwapa moyo fake wasanii wachanga

Kwa Zomboko wimbo ukiwa mkali utamuona tu anavyoonge. Pia ukiwa kimeo utamjua pia. Anausifia kwa shida. Hata video huzitetea japo hawezi sema ni mbaya
 
Sijawahi ona msanii alipita hapo akatoboa,
Wapo, km fm academia "wajelajela" ya kina ndanda cosovo, malu stonchi, Pablo masai, nyoshi El sadaat kabla ya kuvunjika ilitokea hapo...
Beta Musica ya kina Mangustino pia wimbo wao kwanza "bana beta ulitokea hapo, wapo wengine wa bongo fleva walianzia hapo..

Sema wengi wao huwa hawarudi au kutoa compliment kwamba walipita hapo
 
Kuna muda ukweli usemwe kama sina kipaji na hilo eneo bora niambiwe tungeokoa muda na pesa kwa vijana wengi sana...
Unafki uliopitiliza sio mzuri
Kama Master J alivyosema ukweli kwa Harmonize kuwa music si talanta yake bali akatafute shughuli nyingine ya kufanya?
See what Diamond did to Harmonize, unadhani ni vipaji vingapi vinapotea kwa kukatishwa tamaa.
 
Huyu jamaa anamoyo wa kusifia na anasifiwa hata nyimbo ambazo ukicheck unaiona what the hell is this 🤔
Hakika kama hakika🙌
 
Hahahahaha

Mleta uzi umenifurahisha sana

Iko kipindi huwa nacheka sana nikikikuta maana mwamba anajua kufariji wasanii

Ukikutana na yule mtangazaji hata kama ulikuwa umepanga kuacha mziki au uigizaji basi utaahirisha.
 
Ulitaka awavunje moyo vijana?
Na izingatiwe kuwa hadi anapohojiwa wimbo uliishasikilizwa/tazamwa na wakajiridhisha kuwa kati ya wengi walioleta kazi zao huyo anayehojiwa ana vigezo vyote!
 
Kama Master J alivyosema ukweli kwa Harmonize kuwa music si talanta yake bali akatafute shughuli nyingine ya kufanya?
See what Diamond did to Harmonize, unadhani ni vipaji vingapi vinapotea kwa kukatishwa tamaa.
BSS sio Majaji wazuri kwasababu

1) Wanawavunja moyo vijana

2) Hawajui kujudge na kutoa matokeo sahihi

3) Wanajivunia anguko la Msanii stejini

Ukisomea ''Music'' deeply kama wanavyosomea Tumaini University for 3 full years utajua music ni nini hasa kuanzia Vocal, Sound, tunes, kutumia vyombo vya aina zote, kupishana sauti n.k

Kwa Tanzania kuna bwana mmoja anaitwa Innocent Nganyangwa, anajitahidi kumjudge Msanii na anajua Muziki

Nikikuambia kuwa Prof. Jay sio Msanii Mzuri ila ni Mtunzi mzuri wa scenario na kuielezea unaweza kunipinga ila ndio uhalisia huo

Nafuu wakina Barnaba na wengine waliopitia THT

Music ni sanaa pana sana
 
Kabla ya kuingia studio huwa anawasikiliza na wengine anawarudisha wakajipange. Na nje ya kipindi anakuwa anawapa maeneo ya ku improve etc. Itakuwa ajabu kwake kuwaongelea vibaya live kwenye TV wakati anayo hiyo nafasi nje ya TV.

Pia lengo la kipindi ni kuwa promote, watu wawaone wafanye nao kazi...sasa unaweza kuingiza kitu sokoni halafu ukakiongelea vibaya?
 
Back
Top Bottom