Magufuli si mpumbavu kwa sababu ya kuchunga ng'ombe.Tafadhali tutake radhi wamasai maana tunachunga sana ng’ombe lakini tuko vizuri
Mtaje Mtanzania aliyenunua ndinga 0km wakati wa huyu mtu..Kwaiyo Lissu ndio atakununulia Nguo?
Jitume tafuta pesa kwa Akili na jasho lako, Watu wananunua ndinga mpya kila siku wewe unafikiria Lissu atakupa nafuu ya Maisha.
Pamoja na kuubana vilivyo upinzani kwa miaka yake mitano madarakani, haamini kuuona ukiwa na nguvu kwa namna hii hadi kuomba msaada wa wastaafu. Pamoja na kuuaminisha umma, tangu kuingia kwake madarani, kuwa anapendwa, anakubalika, anaheshimika na anaaminika kuliko yeyote yule kwenye uongozi, Dr. Magufuli haamini kuona wananchi 'wakitamani' kumuondoa madarakani kwa kura zao Oktoba 28.
Pamoja na 'mikwara' yake kwa makada wa CCM walioachwa pembeni wakati wa kura za maoni kuwa ni LAZIMA wawaunge mkono wagombea waliopitishwa na CCM yetu, Dr. Magufuli haamini macho yake anaposhuhudia sura za kukasirika na ghadhabu za makada hao. Makada wa maelfu nchi nzima wamejipanga kuwapigia kura wapinzani kwakuwa walioletewa hawakuwachagua.
Pamoja na kutumia jukwaa la Urais kwa miaka mitano kujinadi, kujiaminisha na kujitamba mbele ya watanzania, Dr. Magufuli hayaamini macho yake anapoona watanzania hawamulewi kwenye kampeni zake na hata hawasisimuliwi na ahadi zake tena. Wamejaa uchungu mioyoni mwao; wamepoteza matumaini kuliko kuyapata. Watanzania wanataka kuanza upya. Wanataka mabadiliko. Wanashindwa kumuelewa Dr. Magufuli.
Hakika, Dr. Magufuli haamini anachokiona. Ametarajia A, anaona B. Wako wapi wale waliokuwa wakimshabikia miaka yote mitano? Wako wapi waunga mkono juhudi? Ni wazi, tafakari atakayoifanya Chato kuanzia jana hadi tarehe 14/9/2020 itajikita katika kujiuliza: amewakosea nini watanzania hadi wampe 'surprise'hii ya kiuchaguzi? Atakapoanza na Kagera, ajirekebishe na ikibidi aombe radhi kwa kuteleza kwake kwa hili na lile.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kahama, Shinyanga)
Huo ni mtazamo wako bwashee.... Lakini kule field Dr Magufuli na CCM wanakubalika sana.
Naibariki siku ya uchaguzi 28/10/2020
BashiteMtaje Mtanzania aliyenunua ndinga 0km wakati wa huyu mtu..
Kumbe Ufipa kumejaa wapumbavu, Robert Amsterdam ni nani kwa taifa kubwa kama Tanzania? Think tank ya Ufipa ni majanga.