Hakika kilimo na ufugaji ndo mpango mzima .. .

Hakika kilimo na ufugaji ndo mpango mzima .. .

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,598
Waungwana habari zenu!
Umemaliza masomo - ajira huna ...
Ulijitahidi kutengeneza documents za kughushi - umetumbuka
Umeshindwa kuelewana na wafanyakazi wenzio - umetumbuka
Umekuwa kimbelembele kama .... - umetumbuka
Soma tena kichwa cha habari ... hilo ndo suluhisho la kila siku....
Maisha hayaendi bila kula, kuvaa na kulala ... mengine ni nyongeza .. kikubwa zaidi ni kula kwani bila kula afya yako itakuwa mgogoro.
Lima tu - utapata chakula cha kila aina
Fuga tu - utapata kila kitoweo
Ziada ya hapo - utauza na kupata fedha kwa ajili ya mambo mengine ...
Waungwana .... hacheni kuilaumu serikali, jilaumu mwenyewe kwanza kwa kutotafakari miaka nenda rudi.
Hivi kama ungelikumbuka mnamo mwaka 2010 wakati unaangaika na wanasiasa, ukatenga muda na ardhi na kupanda miti ya mbao ipatayo 50, hivi - baada ya miaka mitano ya kisanii (maisha bora kwa kila mtanzania) ungevuna hiyo miti ungekuwa na kiasi gani cha pesa?
Mwaka huu usiishe kabla ya kupanda miti kwenye kaplot kako ili ifikapo 2021 uweze kuvuna ..
Mwanasiasa hana mpango wa kukukomboa hata siku moja ... kazi yake ni kujitangaza tu. Siasa ni kazi za kudanganya wananchi, na sina uhakika kama kweli kuna mwanasiasa ataiona paradiso.
 
umenena mkuu hakuna mwanasiasa atakae iona paradiso hasa huyu anayejiita malaika mkuu..hajaribiwi.
 
That 's true
Umeona ..???
Tatizo ubitoz ndo shida kwa wabongo walio wengi. Kuna jirani yangu yeye mwaka mzima huwa ana hela.. anaendesha kilimo cha bamia .. wamama kila siku wanapanga folen kununua bamia .. lakini wasiojua wanamuona kama mshamba flani vile....
Kama mnataka mali mtaipata shambani ... hali ikishakuwa ngumu, wenye kipato kidogo hukimbilia kwenye mbogamboga; Tengeneza ya kukusanya pesa toka potepote - kwa wenye kipato kidogo na kikubwa pia.
umenena mkuu hakuna mwanasiasa atakae iona paradiso hasa huyu anayejiita malaika mkuu..hajaribiwi.
Tena huyo ... dah! sina neno .. mtu anakukuta una shida then anakwambia ukome! Anakupaka pilipili kwenye kidonda kibichi .... Eti pesa zitaendelea kukauka mifukoni ... basi ... asiyesikia la mkuu ...
 
Wazo lako zuri, but mazao yakulima yako mengi lakini je! Kilimo gani kati hiv kinalipa? Migomba, tikiti maji, mbogamboga, miwa.
 
umenena mkuu hakuna mwanasiasa atakae iona paradiso hasa huyu anayejiita malaika mkuu..hajaribiwi.
Hata mfalme sulemani? au yusuph?? Ukweli ni kwamba kwa sisi wa kristo biblia ina visa vingi sana vyenye mafunzo, mfano kuna kisa cha sodomana gomola mahasi na uovu ulizidi kiasi cha binadamu kutamani kuzini na malaika Mungu alipoamua kuichoma Sodoma na Gomola ambayo ilichafuka kwa kiasi kikubwa kiasi cha kuamini hakuna binadamu waliokuwa safi ila katika uovu na uchafu huo Mabinti wa Ruthu hakuwajua wanaume kwa lugha ya kileo walikuwa bikra. Na sodoma na Gomola Mungu aliiteketeza akajiokoa Ruthu na kizazi chake. The same applies kwa Nabii Joshua au Elisha ambaye alipopewa kwenda kutangaza neno la Mungu alijiona mtakatifu ni yeye tu Mungu akamuonyesha kuwa hakuwa peke yake

Ninachoweza kukwambia katika hali hii hii ya ubinadamu ambayo imajawa na udhaifu na hali ya kuanguka pindi inapopita katika majaribu wapo watu bila kujali nafasi zao, Elimu, kabila au hali zao za kiuchumi huheshimu natural laws of Justice Hawadhurumu,Hawasemi Uongo,Hawaibi cha Mtu,Hawazini, Wanaheshimu wenzao na wanaheshimu maadili ya kazi zao. Ni kweli wnaweza kuwa wachache sana ila hoja ya msingi wapo, Ni kama tunavyoamini mabinti bikra hawapo yawezekana mazingira ya sasa yamekuwa changamoto kwa sisi vijana kujitunza na hii inapelekea wengi kujamiiana katika umri mdogo ila hii haiondoi ukweli kuwa mabinti wasiojua wanaume kabla ya ndoa wapo unaweza usiwaone ila wapo. Na sometimes Mungun hutupa tunachostahiri.
 
Wazo lako zuri, but mazao yakulima yako mengi lakini je! Kilimo gani kati hiv kinalipa? Migomba, tikiti maji, mbogamboga, miwa.
Mkuu kilimo ni kilimo tu hata kiwe cha kujikimu. Katika maisha unaposhindwa kujikimu huwezi fanya lolote. Utakufa na njaa tu. Nikupe kisa kidogo tu!
Mwezi wa nane nilipohudhuria maonesho ya nanenane - Nyamhongoro jijini Mwanza, nilikutana na kikundi cha akina mama wanatangaza kilimo cha viazi lishe. Viazi hivyo ni aina ya viazi vitamu na vinatumika kupata unga ambao unaweza kuutumia kutengeneza maandazi, keki, mikate n.k. Hapo hapo walikuwepo wadada wanatengeneza hayo maandani, na walikuwa na keki zilizotengenezwa kwa kutumia unga huo.
Wabongo walivyo wa ajabu walikuwa wanakimbilia kununua keki na andazi. Mi nilinunua keki na kuwaomba wanipatie mbegu za hayo malando. Mama mtu mzima - kiongozi wao alinambia tangu amehudhuria maonesho yapata miaka mitano iliyopita anashangaa watu hawahitaji kununua mbegu.
Siku iliyofuata aliniletea mbegu 15 nikapeleka nyumbani na kuzipanda kwenye ndoo kama maua tu. Jana nilijaribu kutifua kidogo nikakutana na kiazi kikubwa sana kwenye ndoo, ni kiazi cha aina yake, kitamu sana kikipikwa, kina unga wa kutosha. Nilipompigia simu akaniambia nisubiri hadi miezi mitatu ndo nitafurahia hiyo mbegu ya viazi lishe.
Pointi yangu ni kwamba kwa mbegu hizo, nitakuwa nimeokoa Tshs. 1200/= pesa ambayo huwa naitumia kwa ajili ya mkate wa breakfast kwa siku zote nitakazotumia hivyo viazi lishe kama breakfast.
So; kilimo kwa kiwango chochote kina faida tu!
 
Waungwana habari zenu!
Umemaliza masomo - ajira huna ...
Ulijitahidi kutengeneza documents za kughushi - umetumbuka
Umeshindwa kuelewana na wafanyakazi wenzio - umetumbuka
Umekuwa kimbelembele kama .... - umetumbuka
Soma tena kichwa cha habari ... hilo ndo suluhisho la kila siku....
Maisha hayaendi bila kula, kuvaa na kulala ... mengine ni nyongeza .. kikubwa zaidi ni kula kwani bila kula afya yako itakuwa mgogoro.
Lima tu - utapata chakula cha kila aina
Fuga tu - utapata kila kitoweo
Ziada ya hapo - utauza na kupata fedha kwa ajili ya mambo mengine ...
Waungwana .... hacheni kuilaumu serikali, jilaumu mwenyewe kwanza kwa kutotafakari miaka nenda rudi.
Hivi kama ungelikumbuka mnamo mwaka 2010 wakati unaangaika na wanasiasa, ukatenga muda na ardhi na kupanda miti ya mbao ipatayo 50, hivi - baada ya miaka mitano ya kisanii (maisha bora kwa kila mtanzania) ungevuna hiyo miti ungekuwa na kiasi gani cha pesa?
Mwaka huu usiishe kabla ya kupanda miti kwenye kaplot kako ili ifikapo 2021 uweze kuvuna ..
Mwanasiasa hana mpango wa kukukomboa hata siku moja ... kazi yake ni kujitangaza tu. Siasa ni kazi za kudanganya wananchi, na sina uhakika kama kweli kuna mwanasiasa ataiona paradiso.

hiki ndicho alichowakifanya MASELE pale shinyanga
 
Back
Top Bottom