Hakika Shilole ni kirusi cha jamii

MC Chere

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
586
Reaction score
400
Nilipata kumsikia one day akihojiwa kwenye kituo x cha redio akisema "you know,mimi ni kioo cha jamii"
Hivi wewe binti unaelewa maana ya kioo cha jamii?

Kuonesha miguu yako ya rangi mbili mpaka matusini ndo ukioo wenyewe? Kuimba chuna buzi?Kucheza ukiwa uchi huko Belgium na unasema ilikuwa ni bahati mbaya?

Wewe unajitangaza kwa biashara nyingine na sanaa ni mwamvuli tu.Na wenzako wengi wa bongo muvi sijui,kazi yenu ni kutuonesha mapaja tu.Nyambafu yenu.

Hivi huwezi kujifunza kwa dada yako Jide?Vipi Shaa hawezi kuwa shule kwako?,ebu jiheshimu.Wapo wengi sana wakuitwa kioo cha jamii lakini sio wewe.

Angalia akina Fid q,Profesa Jay,Mwana Fa,Jide,Shaa,Banana Zoro na wengineo wengi tu. Kwanza wanaimba nyimbo za kuelimisha lakini si ufuska wenu huo.
 
Ngoja nimshtue Shishi kua kaanzishiwa uzi hapa JF ili aje akujibu.
 
nilimsikia akisema annatumia laki moja kila siku, anasomesha watoto wawili kila mmoja milioni tano kwa mwaka pango ya nyumba milioni saba kwa mwaka, ama hakika mapato yake kwa kazi hiyo si haba...
 
Ngoja nimtetee maana naona hajawa na mitimu yenu angeweza kutetewa,Shishi baby ni bonge la msanii na anakielewa anachokifanya si kwamba ni mwendawazimu ila KILICHOTOKEA NI AJALI KAZINI.Hivi nyimbo za akina LIL wayne,Lady Gaga,Eminem na wengine wengi munazozipiga kila siku muda wote munajua wanachokiimba au lugha ndo tatizo ndo mana hamuoni jinsi wanavyotukana tena matusi ya chumbani na bado munawasifia je hao si vioo vya jamii??????????? acheni hizo muziki wasasa umebadilika na hata vya kuviimba navyo vimebadilika hizi sio enzi za akina Mbaraka Mwinshehe au wakina Marijani Rajabu na hata hawa wangekuwepo wangeshabadili vya kuviimba.Piga kazi Shishi Baby achana na hawa wapiga majungu kuna wengi wanatamani maisha yako ila ndo ivo hawawezi kuyafikia mimi ni shabiki wako.
 
Huyo demu mjinga nashukuru familia yangu hatujawah kumshabikia
 
nilisikia alikuwa anataka kugombea ubunge.
 

Namuongezea Na Tusi La Kithungu "Stupid Gal"
 

Nna wasiwasi na brain capacity yako! Khaa:thumbup:πŸ˜•πŸ˜•πŸ˜•
 
Nna wasiwasi na brain capacity yako! Khaa:thumbup:πŸ˜•πŸ˜•πŸ˜•

Mi naona mnatumia nguvu nyingi mno kumshambulia kuliko kumsaidia kwani nae ana positive zake. Nilivyoanza soma thread nikajiuliza Shilole kafanya nini tena wakati amefungiwa kumbe mambo yale yale. Ni kijana aliyejituma kujitafutia maisha ambao wengi yanawashinda. Ni msichana ambae ameamua kutumia nguvu zake mwenyewe na sio kutegemea mtu mwingine zaidi ya kutegemewa na wengine. Hivyo hiyo ajali isiwe justification ya kumponda kiasi hiki. Sidhani kama ni haki!
 
Mgombea ubunge huyu ..aliahidi akishinda atashigulikia mama ntilie wasisumbuliwe..akili zake kama Dr Abisereeemaaaa
 

Humu wengi ni wivu tu mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…