Hakika:Sitokuja kuisahau hii siku..

Hakika:Sitokuja kuisahau hii siku..

Sheikh23

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
1,175
Reaction score
1,934
Ilikuwa ni jumapili tulivu,isiyo na pilika pilika jijini Da'slam,hakika ilikuwa ni j'pili iliyohitaji sehemu tulivu ili kuondoa msongo wa mawazo na pilika za hapa na pale.
Majira ya mchana,natoka zangu home Kimara nasaka kampani ya mshikaji wangu mitaa ya Sinza,si unajua bata bila ya kampani haliendi..
Nafika kwa mshikaji,nampa wazo analipokea kwa furaha,tunakula muvi mbili tatu kusogeza muda,mjini bata tamu lianzie jioni flani hivi,mixer saa Kumi na mbili au saa moja moja na kuendelea au vp!
Time zinasogea,uzuri mshikaji baada ya ajira priority yake ilikuwa ndinga,so usafiri wa kudakia totoz na kumpeleka hapa na pale anao,mimi wa first priority nyumba mjini daladala,bodaboda huwa zinanihusu.
Tunawasha ndinga,sheli kidogo kunywa wese,tunaunga foleni atm kidogo kuzishibisha waleti zetu ili tukianza kugawa route kwa ma_weiter na watu wa jikoni zisikatike kama safari za dreamliner na bombadier..
Mshikaji anshauri tuongeze kampani,tunakatiza K'nyama kumsomba mwana flani hv,hana pesa ila ni mtoto wa mjini,bishoo flani totozi zikimwonaga hua zinaingia bleed bila kupenda.
Kampani iko full sasa,orodha ya viwanja inamwagwa na kupigiwa kura ya turufu,penye wengi hapaharibiki jambo,tunaingia kiwanja flani mixa ndinga za ukweli kwenye parking,ndani sasa ndio balaa,madhari kama upo Ulaya kama sio fukwe za Brazil,Barmaid full uniform,dizaini kama meneja kigezo ni barmaid awe na nyungu kubwa,mizigo imejaza nyuma kama haiendi haja,Dar raha jamani..
Flat screen za kutosha nje,waangalia mpira huku,habari kule,miziki kule,muvi pale hakuna kukaa kwenye runinga inayoonyesha kitu ambacho sio hobby yako,uwekezaji wa hapa ni Billions of Money.
Uzuri kampani hii wote ni walevi kindakindaki na soka la Uingereza,tunajisogeza kati ya moja ya flat screen 50+ inch kama sikosei,hakika ni raha kucheki soka kwenye tv ya sampuli hii,sio tv anayeonekana na mpira ni mchezaji mmoja,tv unafumba jicho moja ili uone vizuri kama unalenga shabaha.
To Be Continued...ITAENDELEA
 
Hizi kampani pia tujifunze kuzitumia kutafuta hela zisiwe za kutumia tu hela. ni rahisi mtu mweusi kukutafuta mtumie lakini siyo kuunda partnership ya kuwekeza! Tujifunze
 
Back
Top Bottom