Chukua samaki wako mpasue, mtoe makolokolo yote ya ndani muoshe vizuri kwa maji safi na salama. Baada ya hapo sasa mtie ndimu ya kutosha, mtie tangawizi ya kutosha, mtie kitunguu swaumu cha kutosha pamoja na viungo vingine vingine then mdumbukize kwenye mafuta yako sasa. Mkaange vizuri aive na viungo vyake, hakikisha unapompelekea mgeni wako baada ya kula asikusahau kwa chakula kitamu ulichomuandalia.